Nimepangiwa kazi Bunda Town Center, naomba kujua mazingira yakoje!

Nimepangiwa kazi Bunda Town Center, naomba kujua mazingira yakoje!

Wakuu hongereni na poleni kwa majukumu

Kwanza namshukuru Mungu kwa mema yote hadi nimefanikiwa kupata kazi serikalini. Mimi ni mwenyezi wa Mikoa ya Kusini ila kwa sasa nipo Arusha hivyo nitatokea huku kuja Arusha kuja Bunda

Sasa naomba kujua mazingira yakoje, hali ya hewa,huduma za kijamii nk aidha kodi kwa chumba inakuwa shingapi ili nijipange vema

Natanguliza shukrani za dhati nikiamini wenyeji watanisaidia kwa kunipa hints na tips

View: https://youtu.be/XWpkkbN2sEI?si=vtW4gZrm1nIWvfNC
 
Hali ya hewa safi, Mimi nilikuwa nakaa mtaa wa Bunda stoo, ulipo ukumbi wa halmashauri kwa chini kidogo...chumba na sebure ndani ya fensi nilipanga kwa mwezi elfu 40, maji yapo ndani na umeme ndani...ila choo kilikuwa kwa nje. Mwaka 2016 hiyo ...maisha ya kule safi, soko Kila jumanne lipo la kuhemea..stendi ya mabasi ya Bunda ndio soko kuu Hilo...jumanne panafurika bidhaa. Huduma za makanisa zipo tele mkuu ni wewe dhehebu lako tu, mji mdogo ila mzuri sana, gharama usafiri ni kama hakuna...ni ndogo sana
 
Tumuulize mbunge Ester bulaya
 
Mwambie na guesti zipo za kutosha.

Lami nyingi tu, maisha mazuri.

Ila Waikizu janjajanja za kuhuni. Kuwa nao makini kidogo tu.

Bunda Mwanza, Tsh 10,000 mara moja moja kutembea.

Bunda Mjini panafaa kuishi pazuri.
 
Mwambie na geati zipo za kutosha.

Lami nyingi tu, maisha mazuri.

Ila Waikizu janjajanja za kuhuni. Kuwa nao makini kidogo tu.

Bunda Mwanza, Tsh 10,000 mara moja moja kutembea.

Bunda Mjini panafaa kuishi pazuri.
Asisahau, asipende kubishana bishana jamaa wanakataga mapanga wakikasirika, kama ana sura nyororo kama ya mwanamke basi wale jamaa hawasiti kukutania inatakiwa asiwe na hasira. Kama mwanamke awe mwanamke kweli na kama ni mwanaume awe mwanaume kweli asichanganye mambo hapo..awe makini sana, 😀😀
 
Wakuu hongereni na poleni kwa majukumu

Kwanza namshukuru Mungu kwa mema yote hadi nimefanikiwa kupata kazi serikalini. Mimi ni mwenyezi wa Mikoa ya Kusini ila kwa sasa nipo Arusha hivyo nitatokea huku kuja Arusha kuja Bunda

Sasa naomba kujua mazingira yakoje, hali ya hewa,huduma za kijamii nk aidha kodi kwa chumba inakuwa shingapi ili nijipange vema

Natanguliza shukrani za dhati nikiamini wenyeji watanisaidia kwa kunipa hints na tips
Bunda ni pa kawaida au chini ya kawaida kulingana na mtazamo wa mtu tu wewe njoo na akili zako halafu u-adapt mazingira, siyo mji uliochangamka sana

Mzunguko wa hela ni wa kawaida au chini ya kawaida, wana score daraja C kwenye uchumi

Hapo Bunda mjini, unaweza tembea kwa miguu tu inatosha kuumaliza mji wote kuacha pembezoni mwa mji huko au kwa kutumia tu baiskeli inatosha
Nimemaanisha mji wa Bunda ni mdogo

Ukabila kwa hapo mjini siyo kivile maana kuna changanyikeni nyingi nyingi
Ila vijijini huko ukabila upo mfukoni sana.

Makazi kumudu ni nafuu naweza sema nafuu sana kulinganisha na kwingineko mfn huko Arusha
Chumba cha 50K ni classic nzuri mno ila kama hua unapenda kawaida , hata chini ya hapo bado ni kizuri tu.
Ukigusa vya laki kuendelea, ni kizuri kupitiliza.
Kwa kuanza, unaweza isizidi 50K-60K na bado unaishi sehemu nzuri kabisa.

Mahitaji ya msingi ya kila siku kama huduma za afya au chakula zipo za kutosha kwa hapo mjini

Cha mwisho, wewe nenda Bunda na akili zako kisha utajiongeza baadaye
 
Wakuu hongereni na poleni kwa majukumu

Kwanza namshukuru Mungu kwa mema yote hadi nimefanikiwa kupata kazi serikalini. Mimi ni mwenyezi wa Mikoa ya Kusini ila kwa sasa nipo Arusha hivyo nitatokea huku kuja Arusha kuja Bunda

Sasa naomba kujua mazingira yakoje, hali ya hewa,huduma za kijamii nk aidha kodi kwa chumba inakuwa shingapi ili nijipange vema

Natanguliza shukrani za dhati nikiamini wenyeji watanisaidia kwa kunipa hints na tips
Hongera MWALIMU kila la kheli Kwako bunda hapo town ni sehemu nzurii Sana hongera Sana.
 
Usile hovyo hovyo hadharani,watu wa huko hawana maana kabisa
 
Mda mwingine vijana mnajipa tabu bure!
  1. Unatafuta kazi kwa mbinde
  2. Ukipata kazi ujipe mzigo wa kuwaza mazingira, wakati kiwango cha fedha ulichonacho ni kile kile
Nakushauri , umeshajua sehemu uliyopngiwa ni Halmashauri ya mji, Nenda kaanze maisha kwa vipaumbele vyako binafsi. Kila sehem kuna watumishi kama wewe na watakupokea vizuri.

Kila la kheri.
 
Mkuu mjini kunatofautia na mtu aliipokulia kwa mfano kijana aliyezaliwa Dar ukimpeleka Mikoani uko kufanya kazi atapata shida sana kuzoea mazingira kwasababu ametoka sehemu yenye huduma zote za kijamii na kashazoea kutumia usafiri sehemu ya umbali mdogo na usafiri upo masaa 24hrs, Sasa kija kama huyu akienda kuishi uko mikoani kwanza atajifunza kukaa nyumbani ikifika saa tatu usiku na kuwahi kulala mapema, na atapata shida sehemu za kwenda kutembea. Na atakutana na aina mpya vya mavazi vya wenyeji wake.
Haya ni mawazo ya watu walioishi mijini miaka ya 199 huko. Siku hizi kila kitù kinapatikaa popote Tanzania dogo!
Una umri gani kwanza
 
Bunda sio pabaya na pamechangamka kuliko musoma. Mabinti wa kikerewe/kijita wa tele.
 
Back
Top Bottom