Hali ya hewa safi, Mimi nilikuwa nakaa mtaa wa Bunda stoo, ulipo ukumbi wa halmashauri kwa chini kidogo...chumba na sebure ndani ya fensi nilipanga kwa mwezi elfu 40, maji yapo ndani na umeme ndani...ila choo kilikuwa kwa nje. Mwaka 2016 hiyo ...maisha ya kule safi, soko Kila jumanne lipo la kuhemea..stendi ya mabasi ya Bunda ndio soko kuu Hilo...jumanne panafurika bidhaa. Huduma za makanisa zipo tele mkuu ni wewe dhehebu lako tu, mji mdogo ila mzuri sana, gharama usafiri ni kama hakuna...ni ndogo sana