Nimepigwa Tsh milioni 8 kwenye biashara ya uwakala kupitia mfanyakazi mzembe

Hiyo pesa atailipa hadi lini Ili iishe?
 
Umepigwa laki 8, JF umeona uongeze sefuri mjomba. Kwa namna ninavokujua wewe ungepigwa M 8, hata huu Uzi usingeweza kuandika aise, mana ingekuwa umeshapigwa Dripp za kutosha hapo Hospital ya jirani.
 
Huyo mwizi hata namba hakuiona jina anavyoitumia pesa?

Hii michezo ya wafanyakazi wakishirikiana na matapeli. Ni sawa na zile sms za tuma pesa kwenye namba hii na wewe utume tu bila kushtuka..!!
 
Mafala hao uwachezee ila watu wako serious na maisha hata kukunyonga hawakunyongi wanakutandika chuma ukafie mbali..!!

Kwenye pesa za watu ogopa utani na mazoea hujui wamezitafuta kwa njia gani..!!
Sawa nimekuelewa mshangazi
 
pole sana mkuu, but hua,tunawaambia nyie maboss wa maduka ya wakala wa fedha kua muwaambie wafanyakazi wako mtu asipokee maelekezo yoyote kutoka kwako kwa sms, akipokea sms ya maelekezo yoyote kutoka kwa number yenye jina la boss wake akupigie simu kwanza asikie sauti yako umpe maelekezo kwa mdomo sio sms, cas watu wanaibiwa sana kwa njia hio, pole sana.
 
Kwanini usiongee na JB mshirikiane kutengeneza bongo movies maana kwenye kuandaa script uko vizuri sana
Sema kuna sehemu kichwa changu cha juu kimekuwa kigumu kuelewa pale aliposema "hadi sasa anampiga binti makofi wakati huo huo anaandika uzi JF"
 
Sema kuna sehemu kichwa changu cha juu kimekuwa kigumu kuelewa pale aliposema "hadi sasa anampiga binti makofi wakati huo huo anaandika uzi JF"
Huyo binti atume hela kwenye namba ambayo jina anaona kabisa siyo la boss wake na wakati ofisi za Mpesa zimejaa majina ya boss ukutani, na atume hela kwa awamu tofauti tofauti zaidi ya siku moja hadi ifikie 8M bila kushtuka wala kuuliza .

Ukifatilia uzi za huyu jamaa utajua ni mtunga stori mzuri tu wala usiwe serious sana na nyuzi zake
 
pole sana kiongozi kumtapeli mwanamke ni rahisi sana ndoo maana wamejazana kwa waganga na manabii feki
 
Upotevu wa pesa tofauti hahusiani na mshahara, huo ni mtaji kapoteza.
Hatujui mzunguko wao mpaka wanalipana hiko kiasi cha mshahara..!!

Hapo wazazi wake wauze shamba walipe gharama, hiyo ni kazi na ni pesa mtu kawekeza..!!
Hela za laana unatafuta hakuna hela za hivyo ujinga mfanye wenyewe huko unataka mzazi auze kiwanja hiyo pesa inaweza kupotea hadi na mtu kabisa...
 
Detective:walijua vipi jina lako?wakala alikusevu jina gani?wao wakakusevu jina gani??unajua software inaitwa atomic pack??
Mkuu wahalifu mpaka wamefanikiwa ujue walifanya uchunguzi na akapata taarifa zote za boss, ata wewe kama unafanya biashara watu kukujua jina lako siyo jambo ngumu matapeli wanaweza kukufatilia mpaka unspoishi na wakawajua watoto wako na mke wako au majirani sasa wakishafikia atua hii kukujua jina ni rahisi sana, au wanaweza kukufatilia kazini kwako na wakishapajua tu na jina lako watalijua, mkuu ogopa watu wakiamua kukufatilia bila wewe kufahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…