Nimepigwa Tsh milioni 8 kwenye biashara ya uwakala kupitia mfanyakazi mzembe

Huyo mwizi hata namba hakuiona jina anavyoitumia pesa?

Hii michezo ya wafanyakazi wakishirikiana na matapeli. Ni sawa na zile sms za tuma pesa kwenye namba hii na wewe utume tu bila kushtuka..!!
Ni mwizi kweli
Unatumaje pesa bila kuangalia jina?
Huyu ameshirikiana na wezi
Hela haina mzaha namna hiyo
 
Hela za laana unatafuta hakuna hela za hivyo ujinga mfanye wenyewe huko unataka mzazi auze kiwanja hiyo pesa inaweza kupotea hadi na mtu kabisa...
Hakunaga pesa ya laana, mafisadi na wauaji basi wangelaanika..!!
Hao wazazi wanafidia uzembe wa mtoto wao.

Hakuna watu wanauza asset zao ili kuokoa jambo lolote?
 
Huyu ni muongo.. watu wanajichosha tu kumpa pole.
 
Pole sana nakumbuka mwaka 2014 nimewahi kufanya kazi ya uwakala kiukweli nilipigwa shilingi laki moja na nusu mpaka waleo sidhani kama kuna tapeli anaweza kufanikiwa tena kunitapeli , kwanza sina imani na mtu yeyote tena .
Nasikia ili uwe mzoefu lazima utapeliwe na ukishatapeliwa ndiyo akili inakua Active kila sekunde na huwezi kutapeli tena.
 
Hiyo pesa atailipa hadi lini Ili iishe?
Hapa hoja sio ailioe hadi lini bali ni kumfundisha kwa kumuafhibu kidogo ili aone uchungu wa kupoteza pesa kwa uzembe,ila kwenye biashara loss ya hivi ipo tu,na muhimu ni kuweka bima ya upotevu wa pesa
 
Kujua jina sio shida kabisa,shida ni kwamba ,kama number ya boss wake kaisevu KAKA,au shemeji,au vyovyote vile,wezi walijuaje??huo ndio msingi wa swali langu
 
Kweli ata mimi nimejiwekea utaratibu wangu ikitumwa sms kwenye namba geni inasema niitumie pesa ata kama imetaja jina la Mama, mke au mtoto sijibu sms na naifuta kabisa nakua sitaki kuiona.
 
Wewe jamaa bhna kwa chai......vipi lakini yule dogo alieshinda mapesa ya kubeti mlimpa ushauri gani...!!?

Hzo case zipo ila kutuambia kwamba ndo wewe imekutokea ni ulongo huo...
 
Pole sana Aisee. Hii i anikumbusha Bwana Mdogo mmoja pale Posta mpua Jijini Dar. Jamaa alikuja akawa anataka kuweka milioni 1.

Wakati jamaa kampa ile milioni na dogo kuihesabu na kuona iko sawa kabla hajamaliza zoezi la kutuma, jamaa akamuambia hebu lete kwanza hizo hela ili nihakikishe namba. Dogo kamrudishia jamaa hela, kisha baada ya sekunde kadhaa jamaa akamrudishia dogo zile fedha na kumuambia "sasa tuma kwenye namba hii".

Baada ya muamala kufanyika na yule jamaa kupotea dogo anapanga panga zile hela anakuta loss ya karibu laki saba. Kumbe jamaa inaonekana alikuwa na bando mbili, bando la ukweli na bando lililochakachuliwa.
 
Hakunaga pesa ya laana, mafisadi na wauaji basi wangelaanika..!!
Hao wazazi wanafidia uzembe wa mtoto wao.

Hakuna watu wanauza asset zao ili kuokoa jambo lolote?
Watu watauza assets kwa ajili ya ugonjwa na mambo yao sio kwenda kuwanyang'anya wazee kiwanja huko inawezekana wewe ni mgeni na hela ndio maana unaweza kuongea chochote watu wengi wamepata matatizo na hizo hela..
 
Kuna mmoja alipigwa kizembe sana wamepiga cm kwa namba ya kawaida eti tutapita ofisini kwako na mabango pia tunamarekebisho hebu shika simu tukupe maelekezo,walimpa namba aweke hapo hapo 5m shwaaah tukasikia ngolo tu!!!
 
Wewe mwenyewe mzembe haiwezekani umkambidhi million 8 kijana aisiye na akili timam
Usihukumu kabla hujakutwa na jambo.
Float ya milioni 8 kwa maeneo yenye mzunguko mkubwa na biashara nyingi/kubwa watu wawili watatu tu wanaimaliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…