Nimeshazichoka vurugu za watoto, bora shule zifunguliwe



Mithali 23

13 Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.

14 Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu



Sijui we ni Baba au ni mama ila kama ni Baba umepwaya kwenye nafasi yako ya kuwalea hao Watoto kana Kwamba miti (i.e chanzo cha fimbo) haipo



Mahali ambapo hakuna Baba Watoto kamwe hawawezi kukua B'se Mama anamapenzi na watoto wake kwasababu ya kuwa na mguso nao tangu tumboni Ndio maana mama Hawezi kumlea MTOTO


Lakini kama Baba yupo na WATOTO hawasikii wala kutii Sauti ya mzazi ni HATARI sana, na Ndio Baba wengi waliojaa kwenye NDOA nyingi kimuonekano wa nje wanaonekana ni wababa ila NDANI yao hakuna mkao wa ubaba Ndio maana malezi ya watoto yanawashinda wanachojua wao ni kuhudumia tu, mtoto kaenda shule, amekula na kulala basi Lakini malezi ya watoto ni zero
 
Wenzako wakila lazima wakachunge mbuzi wewe unalazimishwa kulala? Hongera
 
Hawa watoto ni kama wanachajiwa na jua, yaani hawachoki! Na wakiharibu vitu, ukawauliza walikuwa wanatafuta nini, wanakutazama tu.

Bora warudi shule, walimu pia wakafaidi "battery life" yao!
 
MMkuu

Mkuu hao ni watoto wako vumilia kama vile walimu wanavyo vumilia.
 
Kuna siku nipo na jamaa angu, katoka kazini kachoka kapitiliza chumbani alale kumbe watu wadogo wapo dirishani kwake kelele hadi sio poa.

Nikasikia tu ameropoka kwa gadhabu, "Bwana eeeeh mkacheze barabarani huko.".
 
Ndo mkiambiwa muboreshe maslahi ya walimu muwe munaelewa.....

Kama wewe mwenyewe watoto wako wanakupa changamoto je walimu vipi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…