David Harvey
JF-Expert Member
- Jul 17, 2014
- 3,771
- 9,237
Duh pole mkuu,,an ukiwaza wao wanavotupuna harafu siku ukiwapuna hupati,,na nchi yetu ndio hivo tena hakuna msaada utapata ni huzuniParipesa mkuu
Paripesa mkuu
TrueNaona wafanyakazi wa pigabet wameshavamia jamvi.
Mmeambiwa kabisa walitaka wampe mil 3 ili wamalizane nyie mnakazania ni fixed game,kama ingekuwa ni fixed game hiyo mil 3 wasingempa
Insiders bongo wanazo hizo taarifa ingawa kwa uchache. Kenya hapo ligi yao vilevile, kuna Mrusi alikamatwa anapanga matokeo na Wakenya kadhaa. Uganda pia.Duh kumbe kazi yao inahusisha hadi kufanya fitina uwanjani?
Na hii inafanyika hadi kwenye timu za ulaya au ni bongo tu?
π π π We haya nikitekwa je?π Napenda sana unavyozikabia juu Lumumba Buku Saba.
Naitwa Silas John Charles. Nina malalamiko yangu dhidi ya kampuni ya Pigabet ambayo yamechukua muda mrefu bila kupata uamuzi, hali inayoninyima haki yangu ya kupata fedha ninazodai kiasi cha Shilingi milioni 27.7.
Tupe mfano wa fixed game event moja unayoijua ambayo either ilitiki then mshindi akanyimwa pesa yake au ililost akarudishiwa pesa yakeNdio fixed game hata ukilost,unarudishiwa pesa yako mkuu. Na kama wakisema waruhusu fixed game zilipwe hii biashara haitawezekana maana mtu atanunua game halafu atatia mpunga wa maana na bado ataisambaza watu maelfu wakitia mpunga wa maana tayari kampuni inafungwa ndio maana ikapitishwa sheria kuwa fixed game hazilipwi )Upangaji wa matokeo)
Mkuu hawa hatufanyi nao kazi wamezidi uhuni π€£Pigabet wamekupiga ...
Jamaa anajikuta mjuaji kwa wajuaji πππ, eti kwamba fixed game hulipwi ,nani ambaye hajui fixed game ni niniππHiyo 3M wako tayari kumpa ya kazi gani sasa?
Jamaa anataka kutuokota hapa mchana kweupe π ,watu tumeanza kubeti tangu tupo tumboni ππCha ajabu game ikiwa fixed ukiliwa pesa yako hairudishwi
Jamaa limekaa kitapeli au ndiyo mwenye pigabet anahofia hasara πππ i wonderOk. Nakubali ni maelezo ya upande mmoja na hayawezi kutufanya tuamue ni nani mkosefu. Swali: kwa nini wewe unataka tukuamini kwa haya haya maelezo ya upande mmoja? Yaani unaongea kama wewe ndiye hii kampuni! Kuna kitu unajaribu kuficha? Nina wasiwasi sana kwa sababu unavyotetea siyo kawaida. Kwa taarifa yako kulipa malipo ya waliopiga mil 600 siyo kigezo cha kuwa lazima wawe waaminifu. Anyways, nadhani ni vizuri mwanzisha thread atafute mwanasheria amsaidie.
Watu wanadhani biashara ya betting watu wanakurupuka. Ukizembea utafunga kampuni siku hiyo hiyo. Kuna ligi ambazo wahuni wananunua mechi utakuta ni ligi ndogo ndogo ,, kwenye mfumo kuna indicator wataziona kama ni fixed game na hizo game hata ushinde bilion huwezi kulipwa. Na wangekuwa wanalipa kusingekuwa na kampuni za betting . Kwa kawaida ukishinda mkeka kwenye kampuni za betting huwa wanafurahi kwasababu ni sehemu ya promotion na wanajua kabisa hiyo pesa utairudisha kwahiyo hakuna haja ya kutumia nguvu kukunyima ushindi . Huyo jamaa anoneshw huo mkeka kana usipokuta ni ligi za huko taiwan au huko itali sirie D jamaa wanalalamika kwamba nawatetea ila mimi najadili kuwa experience hakuna kampuni ya betting ya mabilion ya pesa itakayokubali kuchafuka kisa kushidwa kulipa milion 27 hilo halipo wakati mchins mmoja anayefanya analysis kwa mwezi mshahara milion 12π€£ halafu washindwe kulipa 27M ukishinda na usipolipwa ukienda gambling board na wakashindwa wanaweza kufutiwa leseni sasa jiulize kampuni ina miliki Las vegas casino , the gland casino na palm beach kasino na wanadhamni timu ligi kuu washindwe kulipa 27M ? Anyway aende mahakamani tutajua ukweli lakini Tanzania hii haina mtu aliyewahi kushinda kihalali kwenye kampuni iliyosajiliwa na asilipwe.
mzee tangu 2024 ndo unaomba msaada leo!!!Naitwa Silas John Charles. Nina malalamiko yangu dhidi ya kampuni ya Pigabet ambayo yamechukua muda mrefu bila kupata uamuzi, hali inayoninyima haki yangu ya kupata fedha ninazodai kiasi cha Shilingi milioni 27.7.
Tarehe 30/10/2024, niliweka beti yangu kupitia kampuni hiyo na beti hiyo ilithibitishwa na mfumo, ambapo nilipatiwa betslip pamoja na ujumbe wa mkataba. Baadaye, kampuni ilisimamisha mkeka huo bila kunipa taarifa. Nilikuja kubaini kuwa waliingia kwenye akaunti yangu na kuufuta (cancel) mkeka huo, jambo ambalo ninaamini ni kinyume na General Terms and Conditions zao wenyewe pamoja na Sheria ya Michezo ya Kubahatisha.
Tarehe 6/11/2024, niliandika barua kwa Gaming Board kuhusu suala hilo, na tarehe 15/11/2024 nilipokea majibu. Tarehe 13/12/2024, nilialikwa kwenye kikao cha usuluhishi kilichofanyika tarehe 16/12/2024. Katika kikao hicho, kampuni iliahidi kunilipa, lakini makubaliano hayo hayakuwekwa kwenye maandishi. Baadaye, tulipangiwa kikao kingine tarehe 17/1/2025, ambapo bado sikuwa nimepata malipo. Kampuni ilidai kuwa kiasi ninachodai ni kikubwa na kuniomba nipunguze. Nilikubali kushusha madai yangu kutoka milioni 27.7 hadi Shilingi milioni 20, lakini kampuni ilikataa na kusema ilikuwa tayari kunilipa Shilingi milioni 3. Nilikataa kwa sababu sikuona haki kupokea milioni 3 wakati madai yangu kutokana na beti hiyo ni milioni 27.7.
Baada ya hapo, tulisainishwa fomu ya kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindwa kufikia makubaliano. Tarehe 18/2/2025, Gaming Board ilinijulisha kuwa imeshindwa kufikia mwafaka kati yangu na kampuni. Niliamua kwenda mahakamani, lakini shauri langu halikuweza kuendelea baada ya Pigabet kuwasilisha pingamizi kwamba Gaming Board haikuwa imetoa uamuzi kuhusu suala hilo, hivyo ikahoji kwa nini nimeenda mahakamani. Mahakama ilikubaliana kwamba Gaming Board ilipaswa kutoa uamuzi rasmi, na si kufanya usuluhishi pekee.
Tarehe 13/5/2026, nilirudi Gaming Board kuomba kuongezewa muda kisheria na kusikilizwa upya. Niliwasilisha barua ya kuomba kusikilizwa upya, ombi ambalo lilikubaliwa, na baadaye niliitwa tena kwenye vikao viwili. Hata hivyo, mpaka sasa Gaming Board bado haijatoa uamuzi wa maandishi. Ninaendelea kuambiwa nisubiri bila kupewa muda maalum wa lini uamuzi utatoka.
Suala hili limeanzia mwaka 2024 hadi sasa mwaka 2026, lakini bado sijalipwa fedha zangu. Wakati huo huo, kampuni ya Pigabet inasisitiza kunipa Shilingi milioni 3 pekee, jambo ambalo silikubali kwa kuwa madai yangu ni Shilingi milioni 27.7. Pia, ninapowasiliana na kampuni hiyo kuhusu suala langu, nimekuwa nikijibiwa kwa lugha ambayo si nzuri.
Naomba mnisaidie kupaza sauti yangu ili mamlaka husika zilifuatilie suala hili na kuishinikiza kampuni ya Pigabet pamoja na Gaming Board kuchukua hatua na kutoa uamuzi wa haki. Nimejaribu kulifuatilia suala hili kwa muda mrefu bila mafanikio, na nina hofu kwamba likiachwa kimya kimya sitaweza kupata haki yangu.
Kaishiwa utetezi huyo π ,hoja yake ina mantiki kwenye sehemu isiyokuwa sahihi na ya mantiki tofautiNimekuuliza ili ujibu nikuelewe. Anyway kama hakuna majibu ni sawa tukimaliza kwa style hii ya kuelekezana kwenda mahakamani.
Mkamalia atajuaje kama ni fixed game?Ndio fixed game hata ukilost,unarudishiwa pesa yako mkuu. Na kama wakisema waruhusu fixed game zilipwe hii biashara haitawezekana maana mtu atanunua game halafu atatia mpunga wa maana na bado ataisambaza watu maelfu wakitia mpunga wa maana tayari kampuni inafungwa ndio maana ikapitishwa sheria kuwa fixed game hazilipwi )Upangaji wa matokeo)
Nilimuelewa mkuu.Kaishiwa utetezi huyo π ,hoja yake ina mantiki kwenye sehemu isiyokuwa sahihi na ya mantiki tofauti
Advance shingapi?Hii itakuja kufidiwa na hao wadaiwa. Wamemsumbua sana mwamba
Hiyo kampuni yako unayojaribu kuitetea ina janja janja nyingi sana kuanzia kwenye kuweka hela kutoa pesa, MfanoUdogo wa kampuni unapima na nini kwamba kuna kampuni inaanza biashara bila kuwa na mtaji hitajika ? Kuna vigezo kwanz nilazima uwe na mtaji kiasi kadhaa ndio usajiliwe pili . Kila kampuni ina kiwango maximum chakulipa na hawataruhusu ushinde zaidi ya hicho kiwango ,, hivyo kama wamwkubali wewe kustake maana yake wana uwezo wa kukulipa kama utashinda
Jamaa mbishi khaa ππTukiacha hii issue ya jamaa , haijalishi unajua au haujui ukiangukia kwenye mchezo uliokuwa fixed kwenye option hiyo hiyo hauwezi kulipwa,, mara nyingi hii michezo inafungwa odds, au kufutwa kabisa kama ulikuwa ushabeti ina<
Zipo nyingi tu. Tembelea kampuni za betting mara kwa mara ukiona game haijaanza halafu imefungwa odds au beti mara kwa mara ukiona timu mechi imeisha na imetolewa kwenye mkeka ndio mfano wa fixed game. Au pigia simu kampuni yeyote ya betting waulize huwa wanalipa fixed game? Watakujibu.Tupe mfano wa fixed game event moja unayoijua ambayo either ilitiki then mshindi akanyimwa pesa yake au ililost akarudishiwa pesa yake
We jamaa bhana aliyekwambia betting wanagawa hela za bure ninani? ,,, Ofa yetote lazima iambatane na masharti kama hutaki bonasi nibora usikubali ukikubali bonasi nilazima utimize masharti yote mfano kuna bonasi mpaka uibetie mara nne ndio uruhiswe kutoa . Hakuna hela za bure kwenye betting bwana mdogo. Hizo bonasi zinawekwa kuvuta wateja lakini zina masharti magumu kuna kampuni zinatoa bonasi hadi milion 4 ila kuipata nimapaka utimize hivyo vigezo vigumu walivyoweka. Ksma huna hela ya kubeti nibora upumzike kubeti kuliko kutegemea bonasiHiyo kampuni yako unayojaribu kuitetea ina janja janja nyingi sana kuanzia kwenye kuweka hela kutoa pesa, Mfano
Mwaka jana mwezi wa 3 walikuja na ofa ya promo code "CHUI" kwa ajili ya kupromote kampuni kwa kushirikiana ambasador wao Rayvany
βPigabet imekuja kivingine mwaka huu na kwa wote watakao jisajili kwa mara ya kwanza kwa kutumia kodi ya CHUI watapata bashiri za bure zenye thamani ya Sh30,000 kila mmoja,β amesema.
Amesema ili kushiriki katika promosheni hii wateja wote wa βkizazi cha wajanjaβ watacheza kwa dau la kuanzia Sh2,000 na kubashiri mechi mbili au zaidi, na jumla ya odds zisizopungua 2.5 ili kuingia kwenye nafasi ya ushindi kila wiki na katika droo kubwa ya mwisho wa mwezi."
View attachment 3670251
Watu tukaichangamkia kweli kweli tukawapuna haswaa kwa hizo freebets zao za elfu 30 ,30 ,baada ya kuona wanapunwa sana siku 5 baada ya kuanzishwa hiyo campaign ambao walikuwa wamebeti siku hiyo kwa kutumia freebets hela zao walizowin zikazuiwa kutoka baada ya masaa machache mbeleni na ofa ikafutwa kimya inshort hii kampuni inaonekana ni ya kijanja janja sana ,inakurupuka kufanya maamuzi ,na inaonekana inapata hasara badala ya faida maana hiyo promotion ilivutia watu wengi kubeti ila walivyozingua tu kwenye malipo na usumbufu kwenye kuweka au kutoa hela watu wakarudi zao betway ,betpawa na sportybety.
Kwa nini nasema wanakurupuka kwanza walikuja na ofa ambayo haijawahi kutokea π ya freebet ya Tsh 30,000 haijawahi tokea bongo ,cha ajabu walikuja na ofa ambayo hawakuwa na uwezo wa kuwalipa watu ππ .
Nisiwe muongo nilitumia laini zangu 2 za voda moja nikawapiga 180k ,nyingine 135k safi kabisa na ilikuwa mwanzo mwanzo so hela yangu nikaipata vzr kimbembe kilikuja kwa niliowashawishi wajiunge ili wapate ofa walivyozuiliwa kutoa hela zao ushindi na wengine kujiunga na kukuta ofa imefungwa ndani ya siku chache tu ππ
Jamaa mbishi khaa ππ
Hujaelewa swali ,sijaomba mfano wa fixed game nimeomba scenario moja ya uhalisa ambayo ilishawahi tokea ambayo either ilitiki then mshindi akanyimwa pesa yake au ililost akarudishiwa pesa yakeZipo nyingi tu. Tembelea kampuni za betting mara kwa mara ukiona game haijaanza halafu imefungwa odds au beti mara kwa mara ukiona timu mechi imeisha na imetolewa kwenye mkeka ndio mfano wa fixed game. Au pigia simu kampuni yeyote ya betting waulize huwa wanalipa fixed game? Watakujibu.