Nimesikitika baada ya kuona Nigeria ina GDP karibu mara tano ya Tanzania

Population sio issue sana nyakati hizi za technology na uwezo mkubwa wa kifanisi maeneo ya uzalishaji.

Zamani ulihitaji kuwa na mafundi 5 site na vibarua 50 kujenga nyumba ya ghorofa 10 tu ila sasa mashine moja inafanya kazi ya vibarua 50 na inamaliza kwa uharaka zaidi na mapema zaidi kwa ubora zaidi.

So productivity ya taifa kwasasa usilalie tu idadi ya watu.

Unaweza zalisha bidhaa ambayo 80% ya mzigo unauza nje na sio kwa watu wako na ukapata mapato mengi sana.


Shida sisi tumeweka vichwa maji katika uongozi watu wanaopenda kutapanya pesa na rasilimali as if hazihitajiki kwenye matumizi ya kipaumbele.
 
Nigeria wana GDP kubwa lakini kimaisha bado sana na wao kama sisi. Ww fikiria lagos ina population ya 30+ mil people. Yani mji mzima ni kelele tu sokoni, barabarani yan vurugu mechi.
 

mbona nasisi tunaongoza kwa Tanzanite Africa, tuna mbuga za wanyama ambazo Nigeria hawana, tunamiliki gas ya kutosha nchi kavu na baharini, tunamiliki dhahabu na Almasi ambavyo Nigeria hawana, tunamiliki graphite yakutosha na makaa ya mawe.. nk hivyo havitutoshi kuwa na uchumi mkubwa??
 
Acha upuuzi wako,hivyo vimapambo utalinganisha na mafuta? Umewahi sikia uchumi wa Dunia ukayumba Kwa sababu ya kukosa Tanzanite?
 
Acha upuuzi wako,hivyo vimapambo utalinganisha na mafuta? Umewahi sikia uchumi wa Dunia ukayumba Kwa sababu ya kukosa Tanzanite?

Kwenye top 15 ya gas Tanzania haipo

Kama Tanzania Kuna Almasi Botswana,Angola na South Africa watasemaje?

Kwa taarifa Yako tuu kati ya vyote ulivyotaja hapo Nigeria hawana Makaa ya Mawe tuu ambayo ni useless Duniani.

Tanzania inajitahidi kwenye dhababu tuu lakini Dhahabu sio hitaji la lazima kwenye uchumi wa Dunia kulinganisha na mafuta na hiyo Dhahabu ipo karibu Kila Nchi.
 
Acha upuuzi wako,hivyo vimapambo utalinganisha na mafuta? Umewahi sikia uchumi wa Dunia ukayumba Kwa sababu ya kukosa Tanzanite?

Kwa hiyo kuwa na GDP kubwa mpaka uwe na mafuta? sio mataifa yote tajiri duniani yana mafuta au yanategemea mafuta.

Hata kama si mahitaji muhimu lakini ukivicombine vyote na kuvisimamia vizuri unaweza kuwa na GDP kubwa tu maana zipo nchi zinategemea utalii tu na bado zimetoboa na kuwa na GDB nzuri.
 
Wapo milioni 220 Nigeria, kumbuka kuwa wingi wa watu ni mtaji tosha.
Wingi wa watu unakuwa mtaji endapo tu nchi husika imewekeza katika watu wa nchi hiyo, katika nyanja za elimu, afya na siasa safi. Hapo utapata watu wenye uwezo wa kutafiti, kuvumbua na hatimaye kuzalisha. Kama haukuwekeza kwa watu katika nyanja hizo, population kubwa haitakuwa na positive impact kwa uchumi wa nchi husika.
Thus why India ina population kubwa lakini inazidiwa GDP na USA.
Unakuwa na population kubwa halafu watu wanakuwa kama kuku wa kienyeji tuhukui wanatibiwaje, wanasomaje, "non sense" !
 
Unabisha nini Sasa Mzee? Kulisha population kubwa kama hiyo unadhani wanahitaji uzalishaji kiasi gani? Automatically tuu GDP itakuwa kubwa.

Pili idadi hiyo ya watu inakuhakikiahia soko ambalo ndio kitu Cha muhimu kabisa
Hao watu wana uwezo wa ku- purchase?
Halafu kumbuka mkuu, GDP inaweza hisiwe na positive impact kwa maisha ya watu kwani hilo pato hawagaiwi watu kama posho. Manake unataka kuchanganya GDP na maisha ya watu..... hapana.
Impact yake itaonekana katika social welfare services lakini kama nchi Ina ufisadi' nk. GDP Haina maana yoyote mkuu.
 
Baba ana nafasi kubwa sana na tena mno kutengeneza future ya mtoto wake.
Aki mercy up a haki yake kulaumiwa.
 
Hoja ni Ukubwa wa GDP na sio impacts ya GDP kwenye uchumi.

Uchumi wa Nigeria ni mkubwa mara 6 ya Tanzania.
 
Hii imenikumbusha baadhi ya colleagues wangu ambao ni Wahindi kutoka India kabisa na wengine ni wenye asili ya Kihindi lakini waliozaliwa nchi za magharibi.

Miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakitamba sana kuwa India sasa ipo tano bora ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani [trillion dollar economies].

Wanajivunia sana kuwa sasa wana uchumi mkubwa kuliko hata Uingereza, taifa lililowatawala.

Lakini kama ulivyosema, hesabu ya GDP ukiiangalia kwa juu juu, inaweza kukupotosha sana.

Ndiyo, India ina GDP kubwa kushinda nchi nyingi tu za Ulaya magharibi.

India ina GDP kubwa kuzishinda Canada, Australia, na New Zealand.

Lakini licha ya kwamba India ina GDP kubwa kuzishinda hizo nchi, ikija kwenye GDP per capita, hiyo nchi haipishani sana na nchi za Kiafrika.

Viwango na ubora wa maisha kwenye nchi za Scandinavia ni vya juu sana kushinda India. Wastani wa kipato cha mtu mmoja mmoja nao ni mkubwa mno kiasi kwamba huwezi kabisa hata kujaribu kulinganisha.

Ukubwa wa GDP si wa kuuangalia tu na kuishia juu juu na kutoa hitimisho.

GDP ya nchi inaweza ikawa kubwa lakini watu wake wengi sana wakawa bado ni mafukara.

Nigeria, Egypt, na Afrika Kusini, licha ya kuwa ndo nchi zenye uchumi mkubwa barani Afrika, lakini ikija kwenye GDP per capita, zimeachwa mbali na vinchi vidogo kama Seychelles, Equatorial Guinea, Gabon, na Mauritius!
 
Endeleeni kutafuta machama ya kujifichia, GDP ndio SI UNIT ya uchumi, wenzetu wana export sana sisi tumebakia kusema ohoo wana population kubwa haya kenya wametuzid GDP sisi tuna population kubwa, eneo kubwa, rasilimali nyingi lakini tunachechemea, kuna mataifa kama south africa population sio kubwa kulinganisha na eneo lakini uchumi wao mkubwa interms of GDP.
 
Nchi gani Afrika inayoongoza kwa GDP per capita?
 
Ili uwe na per Capita kubwa ambayo in turn ita define welfare lazima ukuze GDP ni lazima sio ombi.

So Nigeria imetuzidi GDP na per Capita
 
1. Population sio hoja...Kuna nchi Zina small population Kama Canada na ni among the largest economies..
2. Kipimo gani unakitaka Cha muafrika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…