Nimetapeliwa nauli na mrembo niliyekutana naye mtandaoni

Nimetapeliwa nauli na mrembo niliyekutana naye mtandaoni

Sikuliwaza hilo mkuu
Mkuu mimi week iliyoisha pia ilitokea hvyo hvyo ila mm wa kwangu tunajuana sio wa mitandaoni baada ya kumtumia nauli siku tuliyokubaliana aje asubuh nampigia simu anasema kaamka vibaya

tumbo na kichwa vinamsumbua nikajua hapa nishapigwa tukio na mm nimeamua kumpotezea mazima hyo afanye mtaji asijichanganye akarudi na shida zake tena maana ana mizinga balaa.
 
Ameogopa picha zake kazichapa filter ila uhalisia yupo kama mfalme Zumaridi. Usije mkimbia bure.
[emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji2][emoji23][emoji23][emoji2][emoji2]
 
Ishanitokea hii Tena wakati mwingine unahisi amekudharau
Ila milima haikutani binadamu tunakutana
Mtoa Mada piga Moyo konde inote kwenye diary.
 
Mkuu mimi week iliyoisha pia ilitokea hvyo hvyo ila mm wa kwangu tunajuana sio wa mitandaoni baada ya kumtumia nauli siku tuliyokubaliana aje asubuh nampigia simu anasema kaamka vibaya

tumbo na kichwa vinamsumbua nikajua hapa nishapigwa tukio na mm nimeamua kumpotezea mazima hyo afanye mtaji asijichanganye akarudi na shida zake tena maana ana mizinga balaa.
Huyo fungiaa mpaka madirisha asipate kwa kupita
 
Mnavyojua tena, maisha ya harakati huwa hayana mwisho. Wiki tatu zilizopita nilikuwa nachat na mrembo mmoja matata, niliyekutana naye katika mtandao mmoja wa kuonyesha sura.

Nilitokea kumpenda sana huyo binti, na tukafahamiana vizuri tu. Yeye yuko kwenye mambo ya mitindo.

Tatizo yeye anaishi mkoa tofauti na niliopo mimi; nikawa nimemjulisha wikiendi ijayo tuweze kuonana, na tukawa tumeafikiana. Sasa leo asubuhi, akawa amenijulisha anataka aje kuniona; mi nikaona sawa tu hakuna shida.

Akaomba nauli, nami nikamtumia mara mbili yake. Kilichonishtua zaidi, kuwa nauli imeliwa, alianza kuniambia nitume na hela ya mafuta fulani kwa ajili ya massage, yanagharimu 50,000; nikatafakari, nikamwambia tutayanunua huku huku ukishafika.

Baada ya hapo, nikipiga simu haipokelewi, meseji hazijibiwi, w/app hajibu. Imebidi ni hitimishe tu; nauli yangu imeliwa. Ingawa angekuja ningetumia zaidi pamoja na posho ya kwake, lakini kilichoniuma zaidi ni kutokuwa muaminifu.

Wakuu, nimfanyeje huyu mkulungwa?
Mapenzi yamekua mateso kwa sasa[emoji3064][emoji3064][emoji1787]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ebwana filter zinaharibu kinyama juzi kuna jamaa yangu kaniomba nimaindikize akakutane na demu waliojuama mtandaonii akanionyeshaa tukaenda tulichokutana nacho sikuaminii mwamba aliishiwa pozii
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Umekwisha[emoji23][emoji23][emoji23].
Wanakaaga mahali wanakuzoom kwanza, kisha wanazima simu wanaondoka. Tena usiombe kama alikuja na mshikaji wake amtambulishe kwa shemeji.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Tena huyo dada bora asije tu.
Uliona thread ya yule mtu alifungua mada ya hivi kisha yule mwanamke akafika?
Yaani alimpiga picha kila tukio akatuwekea[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
[emoji1]wakati mnagaiana hela ulituomba tukuombee [emoji1][emoji1]

endelea kutesekea pande hizo baada ya kumtumia nauli mwanaume mwenzio[emoji1][emoji1][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
Huu mtindo wengi wanaliwa sanaaa, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom