Nimetapeliwa nauli na mrembo niliyekutana naye mtandaoni

Mnavyojua tena, maisha ya harakati huwa hayana mwisho. Wiki tatu zilizopita nilikuwa nachat na mrembo mmoja matata, niliyekutana naye katika mtandao mmoja wa kuonyesha sura.

Nilitokea kumpenda sana huyo binti, na tukafahamiana vizuri tu. Yeye yuko kwenye mambo ya mitindo.

Tatizo yeye anaishi mkoa tofauti na niliopo mimi; nikawa nimemjulisha wikiendi ijayo tuweze kuonana, na tukawa tumeafikiana. Sasa leo asubuhi, akawa amenijulisha anataka aje kuniona; mi nikaona sawa tu hakuna shida.

Akaomba nauli, nami nikamtumia mara mbili yake. Kilichonishtua zaidi, kuwa nauli imeliwa, alianza kuniambia nitume na hela ya mafuta fulani kwa ajili ya massage, yanagharimu 50,000; nikatafakari, nikamwambia tutayanunua huku huku ukishafika.

Baada ya hapo, nikipiga simu haipokelewi, meseji hazijibiwi, w/app hajibu. Imebidi ni hitimishe tu; nauli yangu imeliwa. Ingawa angekuja ningetumia zaidi pamoja na posho ya kwake, lakini kilichoniuma zaidi ni kutokuwa muaminifu.

Wakuu, nimfanyeje huyu mkulungwa?
Hapo hakuna cha kufanya maana nauli imeliwa. Kwani ulimtumia shilingi ngapi?
 
haiwezekani aseee!!! ngoja niisafishe nyota kwa kula nauli najiona kuna kitu sijatimiza kwenye haya maisha 😂😂😂
Kula nauli naona kama ni utoto fulani hivi; kwa sisi ambao tuko 40+ nadhani ni busara kuwa muwazi tu, kwa sababu hakuna kipya.
 
Msanii tu huyo trust me! Ona umetuma ametoa excuse... ishaliwa hiyoo..hio next week ulotaka wewe aje atakupanga tena umtumie!!!!
Nilishajifunza sitarudia huo ujinga; nadhani pia umri kwake ni tatizo,ndio maana anafanya utoto.
 
Mnavyojua tena, maisha ya harakati huwa hayana mwisho. Wiki tatu zilizopita nilikuwa nachat na mrembo mmoja matata, niliyekutana naye katika mtandao mmoja wa kuonyesha sura.

Nilitokea kumpenda sana huyo binti, na tukafahamiana vizuri tu. Yeye yuko kwenye mambo ya mitindo.

Tatizo yeye anaishi mkoa tofauti na niliopo mimi; nikawa nimemjulisha wikiendi ijayo tuweze kuonana, na tukawa tumeafikiana. Sasa leo asubuhi, akawa amenijulisha anataka aje kuniona; mi nikaona sawa tu hakuna shida.

Akaomba nauli, nami nikamtumia mara mbili yake. Kilichonishtua zaidi, kuwa nauli imeliwa, alianza kuniambia nitume na hela ya mafuta fulani kwa ajili ya massage, yanagharimu 50,000; nikatafakari, nikamwambia tutayanunua huku huku ukishafika.

Baada ya hapo, nikipiga simu haipokelewi, meseji hazijibiwi, w/app hajibu. Imebidi ni hitimishe tu; nauli yangu imeliwa. Ingawa angekuja ningetumia zaidi pamoja na posho ya kwake, lakini kilichoniuma zaidi ni kutokuwa muaminifu.

Wakuu, nimfanyeje huyu mkulungwa?
Yaani umeshindwa kabisa kurudisha muamala?
 
Back
Top Bottom