Nimwombe Rais Samia awaondoe haraka wanajeshi wetu kule DRC Congo. Mnapigana na nchi ya EAC

Rwanda na Tanzania ni mbingu na ardhi yule hawezi kupigana na jeshi la Tanzania watamchakaza vibaya sana
Nchi yenyewe sawa na mkoa wa Tabora
unaongea kwa hisia mkuu!!

Drc ni jeshi bora africa ni no 5/6
tanzania hata top ten haipo
 

ni kweli .wakenye walikuwa wanashirikiana ana M23 na PK kuendelea kuiba madini ya congo.

lakini tuwachekea nyani iko siku tutaokoata mabua. kama DRC congo haiko salama nchi za EAC haziko salama kiivyo.take my wards
 
Na Kagame siyo wa mchezo mchezo. Ni Putin wa Afrika huyu, akiamua kumung'oa mama jua halizami.

PK aliwahi kumwambia JK, I will hit you!. JK hakutia neno.
Huyo mthenge tutamtoa mapema hapo nchini kwake tuweke tunaemtaka
 
Kwani Kagame ni Rais wa Drc?
Wapi nimeitaja DRC
jitahidi kuunganisha mambo mkuu!! kwaiyo hujaelewa uhusiano!

M23/jeshi la rwanda ndilo linaloigalagaza kongo!!
we unaongelea Kua hawaiwezi tanzania ndo nilikua nakulinganishia hapo uone!! Anaweza kumsumbua mbabe wako naww anaweza akakusumbua
 
Mbona hauleweki unataka nini? Unataka Rwanda iwekewe vikwazo? Au unataka Rwanda ifukuzwe EAC au unataka askari wa Tanzania watoke DR Congo?
 
hapa shida ni kwamba hilo kundi la M23 ni la watusi asili ya Rwanda ,burundi na uganda wanatafuti kujitenga na DRC.kwa hiyo kagame anawatetea wenzake kama alnavyokiri kwenye hiyo clip
Kwenye M23 wengi ni Watusi wa Congo na katika matakwa yao hawasemi kuwa wanataka kujitenga na Kongo ila wanataka Haki zao za Kijamii na Serikali Kongo irudi kwenye Meza ya mapatano.

Uwepo wa Watusi wa Rwanda kwenye M23 ni kuwasaidia Jamaa zao jambo ambalo hata Wakongo wanasema wazi wazi kuwa watawasaidia Wahutu kurudi Rwanda na kama nilivyowahi kusema humu mimi nimetembea kwenye hiyo Neighborhood Watutsi wanachukiwa bila sababu na wakizubaa Second Genocide haiko mbali kwahiyo wasaidiane waseme Never Again!
 
Wanajeshi wetu wapo kusaidia ndugu zetu congo wapate Amani.

Hiyo ni KAZI yetu Tanzania.

We are the police of African continent.

Pk soon hutomuona tena.
For the status we are not the police of african continent, hatuko hata top 10 ya strong militaries in africa , na hatuna hiyo capacity for now
 
Hapo ni tpdf kukiwasha, kwa, akili, na kuiba jspo madini kidogo, kama tuliweza kuikomboa kusini mwa Afrika, hatushindwi Congo,
Pamoja na kukubaliana na 'perspective' yako sehemu kubwa, hali tuliyo nayo leo kama nchi usiitegemee kuwa kama ilivyokuwepo wakati ule.
Ndiyo, tunayo maslahi makubwa sana DRC kiuchumi; lakini uwezo wetu wa kusimamia maslahi hayo, uongozi wetu haunayo.
 
Wewe ni matusi unayeishi Tanzania, mhamiaji haramu
 
January Makamba alitoa taarifa February mwaka huu akiwasahihisha gazeti la Jamuhuri waliokuwa wakisifia jeshi la Tz kuwapiga M23 kwamba kikosi cha Tanzania ambacho ni sehemu ya SADC huko DRC hawapo kwa ajili ya kupigana na kundi lolote la waasi.
 
Rwanda na Tanzania ni mbingu na ardhi yule hawezi kupigana na jeshi la Tanzania watamchakaza vibaya sana
Nchi yenyewe sawa na mkoa wa Tabora
Vita sio rahisi hivyo kama unavyofikiri hata kama nchi ni ndogo kiasi gani, Angalia kule Ukraine urusi anavyotokwa jasho, angalia hapo Mashariki ya kati ambavyo Israel imekuwa ikipigana na mataifa makubwa ya Waarabu, Angalia Eritrea na Ethiopia. Mifano ni mingi sana.
 
January Makamba alitoa taarifa February mwaka huu akiwasahihisha gazeti la Jamuhuri waliokuwa wakisifia jeshi la Tz kuwapiga M23 kwamba kikosi cha Tanzania ambacho ni sehemu ya SADC huko DRC hawapo kwa ajili ya kupigana na kundi lolote la waasi.
Sasa ujue tatizo limeibukia hapo!
Fahamu vizuri mambo yanavyokwenda chini kwa chini kiasi cha serikali yetu sasa kurubuniwa na Kagame.
Ni Makamba huyo huyo alliyefanya ziara huko huko Rwanda mwezi huo huo na kukutana na Kagame na kutangaza ziara yake ilikuwa ni ya mafanikio makubwa. Usisahau Makamba ni wa kutokea maeneo hayo hayo kwa upande wa mama. Sasa kama Tanzania itakuwa imeamua kubadili 'objectives' za SADC na aliyewaalika huko; basi tujiandae nasi kufunga vilago kama walivyofanya Kenya.
Hata hivyo, naona M23 bado hawaamini kuwa 'mission' yetu imebadilika, maanake jana/juzi tu wametulipua na kuondoa uhai wa vijana wetu watatu. Pengine bado hawaelewi kwamba tumebadili mawazo baada ya kukutana na 'sponsor' wao mkuu, Kagame.
 
Asiyeona hatari iliyopo kwetu juu ya mgogoro huo atakuwa kipofu wa akili.
Huo mgogoro huko DRC Mashariki uko kwa karibu miongo mitatu sasa, haujawahi kuwa na wala hauna madhara yoyote ya maana kwa Tanzania.
 
Acha story nyingi za vijiweni, ingia mtandaoni usome mwenye kuhusu SAMIDRC.
 
EEEeenHeeee! Na ni juzi tu Kagame kajigamba juu ya uwezo alionao wa kupambana na yeyote!

Tuache utani, labda siku hizi tuwe tumelegea sana, lakini Rwanda siyo nchi ya kujigamba kupambana nasi hata kidogo.

Ni kweli kuhusu hiyo mifano uliyotoa hapo, lakini kila mmoja unazo sababu zake. Afghanistan huwezi kamwe ukailinganisha na Rwanda. Ukraine hajamtoa kamasi mrusi. Kishapoteza asili mia 20 ya eneo la nchi yake, licha ya kupewa misaada ya kijeshi na waliomtumia kama chambo, na hadi leo haionyeshi kuwa Ukraine anayo matumaini yoyote ya kuibadili hali inayomkabiri bila ya kukubali mazungumzo. Hicho pekee ndicho kilichobaki sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…