Nina Mgogoro kwenye ndoa, kila pesa anayopata Mke wangu anaenda kujenga kwao. Naomba msaada

Mleta uzi wewe ni fala, na umedanganywa na mkeo, na ameshakudanganya vitu vingi, na alitengeneza mazingira ya wewe kumuamini, kapata alichokipata sasa ni muda wako kuisoma namba, hiyo nyumba anayojenga ni ya kwake kala njama na mama yake kukutapeli, nenda wachunguze na hao watoto kama ni wako

Haya maneno ni ya mzee kitombile huwa hakosei, shauri yako....KATAA NDOA NDOA KWA AFYA YA AKILI NA MWILI.
 
Unafikiri ndio.ukioa wa hivyo utamkontrol!?

Atakuigizia tu muda ukifika atakuonyesha upande wa pili!!

Nakuambia siri wanawake wasomi huzitafuta ndoa kwa nguvu sana na huzipata wakishazipata ndio utashangazwa na sarakasi zao zao!!!
😂😂😂😂eti sarakasi zao🙌
 
Huu ni mwanzo wa maafa, Kila jambo huanza taratibu na likianza kukomaa manun'guniko huanza. Kumbuka kuna habari nyingi za watu kuumizana hata kufikia kutoana uhai sasa swala lako umelileta hapa je huko mbele unaona kinacho jiri? Upande wangu nahisi kuna ulemavu + damu. Uwe makini.
 
Wazee hawapo? Je hao washenga huna habari nao? Vipi kuhusu wazazi wenu? Usimweke mkeo humu ni sawa na wewe kuvua nguo mbele ya mkweo wa kike. Futa hii kitu ulio weka.
Huu hajafika kiwango cha kuitwa mgogoro ila ni mitazamo na kama Mwanaume umeshidwa kuongoza vyema sasa jifunze darasa la uongozi wa ndoa halafu rudi kuongoza familia. Jua resources ulizonazo na unazoweza kuwa nazo zigawanye sawasawa. Muonyeshe uongozi naye atafuata
 
Na yeye ajenge kwao, sio kwake. Akijenga kwake patakua pa wote. Ajenge kwao na sio kwake
 
Nami nakuunga mkono ktk hili nashangaa kuona wanaomuunga mkono mwanamke.
Kwa hili wanaume tumebaki wachache. Sikatai mwanamke kutuma fedha kwao lakini si kwa kiasi kikubwa kama alivyotuma mke wa mtoa mada.
Kwangu binafsi siwezi kukaa na mwanamke wa namna hiyo ni bora na kutokuwa na mke
 
Anafaa afunguliwe macho ya rohoni kabla hajatolewa roho na mtoa roho anae lala nae kwa kitanda 1.
 
Kama anajenga kwa pesa yake ni sawa,huo mkopo atalipa yeye..wewe pesa yako jenga hiyo yako,ingekua ni mimi ningemwacha ajenge kiroho safi
Umeona ee kama pesa ni yake amwache ajenge tu
 
Siku hiz hamna ndoa. Ni kusogezana tu muishi siku ziende ndio maana haya yanatokea. Mnapokua mume na mke ni mwili mmoja ki roho. Linapokuja mke anafanya yake bila mume kukubaliana, ndoa inakua ndiano.
 
Poleni sanaa
 
Na kugawa utelezi Kwa masela huu! Dadeki.
 
😂😂😂pole Mkuu,ndoa nyingi zimegeuka msiba sikuhizi....wanaume kwa wanawake wapo katika mateso makali sana
Dawa ni moja tu kuwazalisha halafu unamwambia ndoa itafungua tukizeeka!!Kwa sasa tuna nguvu tutasumbuana!!

Unamuacha njia panda TU!!
 
Sikilizeni nyie na ujinga wenu wewe na mkeo mnaandalia hao watoto maisha magumu na mtawapa tabu hapa duniani kwa ujinga wenu.

Kama mnapenda watoto wenu basi jengeni kwenu kama familia kwanza halafu ndio mfuata ndugu na wazazi...Mkianza kushindana hapo ndoa inavunjika watoto wanapata tabu kwa ujinga wenu.
 
Hela yake mwenyewe muwache atumie anavyotaka
 
Wachache wataelewa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…