Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Mawazo yote yaliyotolewa ni mazuri
Ila Kuna wazo Moja nakushauri na hakikisha unalifanyia kazi,hata kama Kwa mtaji mdogo.
Fanya biashara ya NAFAKA,Fanya utafiti uone nafaka zipi dodoma zinauzika sana,na uhitaji ni mkubwa.
Jikite hapo mkuu,Utakuja kunishukuru baadae.

NAFAKA,NAFAKA,NAFAKA..mengine utafanya baadae, baada ya hiyo biashara kusimama.

Dm Kwa ushauri zaidi kuhusu biashara ya NAFAKA na....
 
Mimi kabla sijakupa ushauri naomba unifafanulie kwa namna ipi wewe, kama muajiriwa, ulivyoweza kusave 63m ndani ya miezi 8 tu.

Ili uweze kusave 63m ndani yra mieži 8, ni lazima ulikuwa unasave 8m kila mwezi.
 
Mimi kabla sijakupa ushauri naomba unifafanulie kwa namna ipi wewe, kama muajiriwa, ulivyoweza kusave 63m ndani ya miezi 8 tu.
Ili uweze kusave 63m ndani yra mieži 8, ni lazima ulikuwa unasave 8m kila mwezi.
Ni 64m mkuu, sio 63m.
Mshahara wangu kwa mwezi ni 14m, pamoja na marupurupu mengine mengi tu. Kuna uzi kwenye stories of change nimeelezea kwa kirefu nikiwezaje kufikia kulipwa mshahara huo.

Kwa wastani na save kila mwezi milioni 8 kupitia akaunti ya malengo. Nimejiwekea nidhamu kubwa sana ya kusave ambapo na save karibu 2/3 ya net-income yangu kila mwezi.
 
Asante sana mkuu. Wacha nifanyie utafiti hili la biashara ya NAFAKA kwa hapa Dom. Nitakucheki.
 
Mbuzi wanazaliana Jamani

Ila tu uwe na usimamizi makini

Vinginevyo mchungaji kila akienda machungani anauza mmoja
Asante kwa mawazo yako mkuu. Ila kwa nilichokiwaza ni kufugia kwenye ranchi. Ambapo mbuzi wanakula humo humo (kunakua na eneo la malisho humo humo ndani ya ranchi).

Hivyo, mbuzi hawatoki kupelekwa kokote. Ranchi inakua na camera eneo la kuingia/kutoka pamoja na fence kuntu.
 
Jamiiforums bwana, mtu ameamka na usingizi wake anatuletea ndoto za kumiliki mill 64, kwa kuangalia mwandiko wako tuu hamna company itaweza kukulipa salary ya 10mill kwa mwezi mtu kama ww ambaye hata kuzitumia hujui, je kuwa na akili ya kulipwa 10mill unayo?

Hii na kahawa iliyozidi tangawizi
 
Hongera sana kwanza kwa kukusanya hiyo 65m. Ushauri wangu kwanza achana na wazo la ku invest Dodoma.

Nenda Dar chukua viwanja viwili maeneo ya Goba au madale jenga apartment zako mbili hata za vyumba vitatu vitatu. Trust me unakula hela ukiwa umekaa.

Shida ya hizi investment zingine inabidi ukimbizane sana lkn investment ya nyumba ukishamaliza ujenzi hela inakukuta umekaa.
 
Ushauri wa bure...anza lodge vyumba 10.....au 15 ukiweza hela kila siku ina nguvu sana sana x 100....baada mwaka utaamua kuongeza au kwenda michezo watoto ....nzuri bila pressure! Baadae sana nenda vijumba kupangisha.....baada miaka 5 utatoa mrejesho.....Tafuta eneo zuri....!! Ongeza pesa kidogo ajili finishing .......all the best
 
Inawezekana mkuu. Kuna bwana mdogo tuu namjua yupo Airtel analipwa 12m na huwezi kumdhania. Kama ni mtu wa tech siyo ajabu hiyo
 
Goba viwanja balaa 20 x20 ni 20mil to 25mil .....acha apambane huko Dodoma....
 
Inawezekana mkuu. Kuna bwana mdogo tuu namjua yupo Airtel analipwa 12m na huwezi kumdhania. Kama ni mtu wa tech siyo ajabu hiyo
12mil telecom kawaida sanaa.....wapo weengiiiii sanaaa......wamekaa sana zaidi 10yrs ....kawaida sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…