Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

mkuu kama kuna na fursa za vibarua tunaomba tujulishane.,
 
Asante sana mkuu. Nitamfuatilia huyu jamaa wa Uganda, seems yuko mbali sana aisee.
Umbali sio muhimu ila ni kujifunza tu
Yaani wenzetu wana bahati na dual citizenship
Amekaa [emoji631] miaka 15 karudi nyumbani kuwekeza na leo anasambaza kuku na mbuzi na nguruwe Kampala

Ila sisi diaspora tunaambiwa ni watoto wa wakubwa daa
Kila alieko nje ni mkubwa kwa bongo

Ukianza usisahau kuleta mrejesho
 
..mkuu nikushauri kwenye investment yenye future business ya baadae.
1. Nunua future potential plots maeneo ya miji inayokua kibiashara kama dsm, mwanza, arusha(utalii)..hizo plots hakikisha unapata title deeds na ziwe maeneo yatakayo kuwa potential/hot cake ndani ya 10yrs kutoka sasa..endelea kufanya manunuzi ya hizi plots hata kwa miaka miwili ijayo ukichanganya plots za makazi na biashara.

2. Ukishakuwa na plots nyingi zenye title deeds sehemu mbalimbali kwenye hiyo mikoa potentials plan kuanzisha kitu kwenye baadhi ya hizo plots ambazo hutalipa rent. Pia unaweza kuzikodisha baadhi ya hizo plots kipindi hicho kwakuwa zipo potential areas.

3. Tumia title deeds/hati za baadhi ya hizo plots kuchukua mikopo bank kipindi utakachokuwa free kusimamia business unayotaka kuifanya maana by that time value za hizo plots zitakuwa juu sana. Pia unaweza kuuza baadhi ya plots kipindi hicho kwa bei ya juu na kufanya business.

4. weka utaratibu wa kufanya saving kwa kununua titled plots au USD(dollar) maana pesa yetu inashuka sana thamani na pia akiba ya Tshs inaliwa sana na inflation.

5. Biashara ni nzuri & imara ikitoka kwenye investment yenye mizizi na ya muda mrefu.
 
Jenga nyumba za kupangisha achana na magari mkuu
Bora kujenga lodge! Nyumba za kupangisha zina usumbufu mwingi kwenye kodi.

Labda upate eneo zuri, halafu ujenge appartments kwa ajili ya watu wenye uwezo, walau utapata kodi yako kwa wakati. Ila siyo vyumba vya elfu 50 mpaka laki 150! Huko utakumbana na wapangaji vichomi mpaka basi.
 
Habarini wakuu. Natumaini mnaendelea vizuri na maandalizi ya sikukuu.

Bila kuwachosha sana, nimeweza ku save jumla ya shilingi milioni 64 hadi sasa, kiasi hiki nimeweza kukisave kuanzia mwezi April mwaka huu kutoka kwenye mshahara wangu. Nipo mkoa wa Dodoma.

So far, nimefikiria kuwekeza katika mojawapo ya mambo yafuatayo:

1. Ninunue eneo la shamba kubwa maeneo ya Dodoma nje ya mji au Dodoma vijijini kisha nianzishe kama ranchi hivi ya ufugaji wa mbuzi.

Nimefikiria mbuzi kwa sababu kwa utafiti wangu wa muda mfupi nimeona kuwa mbuzi hawana complications nyingi kulinganisha na wanyama wengine wa kufuga, na pia kuna fursa zaidi kwa mbuzi nchini, na demand ambayo haijawa satsified.

Lengo la hii ni baadae niweze kuwa na kiwanda kabisa cha kuchinja na kuprocess nyama ya mbuzi, na kuweza hata kuuza ndani na nje ya nchi products za nyama ya mbuzi.

2. Nifungue park kwa ajili ya michezo ya watoto kwa Dodoma. Moja ya gaps ambazo nimeziona Dodoma ni kukosekana kwa eneo zuri la maana kwa ajili ya michezo ya watoto na watu kupumzika pia.

Hapa nafikiria ninunue eneo Dodoma then nilitengeneze vizuri na kuweka michezo ya watoto (indoor na outdoor) ya kutosha, pamoja na kutengeneza garden nzuri ya kuvutia kwa ajili ya watu na familia zao kupumzika na kupigia picha.

Kwa nje kwenye ukuta nawaza pia kuwe na frame kadhaa ambazo nitakodisha kwa watu waweke maduka ya vyakula, vinywaji, na vitu vya watoto.

3. Nifungue kiwanda cha maji ya kunywa yale ya kwenye dispenser kwa ajili ya matumizi ya majumbani na maofisini. Nimeona gap pia hapa kwa sababu makampuni yaliyopo hapa Dodoma kwa hii huduma hayatoshelezi mahitaji kwa kiasi kikubwa, mara nyingi sana unakuta yanapotea sokoni kwa muda fulani (no consistency of supply).

4. Ninunue kiwanja saizi ya kati maeneo ambayo sasa hivi ndo yanajengeka (eg Ilazo, NALA) halafu nipige vyumba vya low-cost (behewa style), niweke hapo vyumba kadhaa, then nipangishe nile kodi kila mwezi hata 50K kwa kila room. Baadae kadri ninavyopata mpunga zaidi, niongeze idadi ya vyumba zaidi na zaidi.

Wenye uzoefu wa biashara na ideas na mnaoifahamu Dodoma, niambieni hapo nianze na ipi kati ya hizo kwa mtaji huu nilionao (milioni 64), au hata idea nyingine ambayo sijaitaja hapo juu.

Mimi maisha yangu yote nimeajiriwa tu hadi sasa (nina umri wa miaka 35). Sijawahi kufanya buashara hata ya kuingiza shs 500. Nimeona ni bora pia niangalie upande huu wa business pia maana siwezi ajiriwa milele, na pia kama mjuavyo hizi ajira zetu, leo ipo kesho haipo hasa huku private sector.

Natanguliza shukrani.
Kama kweli upo ddm njoo ilazo hapa Kris corner Kisha anzA kupita pita ujifanye unauliziee Bei ya chumba Cha kupanga hz apartment

Bei Ni Mia nne Hadi Mia tano

Hvyo jitahidi uingie kwenye real estate na lodge kwa ddm umetoka vzr san

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kama kweli upo ddm njoo ilazo hapa Kris corner Kisha anzA kupita pita ujifanye unauliziee Bei ya chumba Cha kupanga hz apartment

Bei Ni Mia nne Hadi Mia tano

Hvyo jitahidi uingie kwenye real estate na lodge kwa ddm umetoka vzr san

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Nipo Dom, na hiyo mitaa unayoitaja nimepiga sana misele na kufanya tafiti.
 
Agiza viti ,meza, table cover ,table verse , moveables stage , Led light .
Tafuta store anza biashara ivyo vitu avitumii umeme .
Party and rental supplies. Hutojuta
Mkuu hebu fafanua kidogo wengine ndio tunakopi aidea hii manake unakuwa unanunua vitu kwa ajili ya kukodisha!!??
 
Jenga nyumba/vyumba/hostels then pangisha. Hii ni nzuri kwa wewe usie na uzoefu wa biashara.

Lakini pia ni asset na ina risks chache kwenye uendeshaji.
Baada ya hapo unaweza ingiza kichwa kwenye biashara nyingine.

Nje ya mada, jf watoe hivi vidubwasha vyao aisee.
 
Tatizo la nyumba unazika pesa na faida inakuja kuonekana baada ya miaka mpka 7,8 na kuendelea mbele hapo unadhani kibongobongo hiyo ni hasara chukulia nyumba ya M50 kali unapangisha 500k kwa mwenzi hapo Ela inarudi baada ya miaka 9 hapo ikiwa imepangishwa non stop na kitu ambacho hakiwezekani pia kodi nimechukulia kodi ya 500k ambayo ni kubwa ila kikawaida ni 200k mpka 300k.
Iko hv biashara ya real estate ipo vizuri. Unajenga unapangisha. Kisha unakopea hiyo nyumba unafanya biashara nyingine.
pesa ya kodi ndio marejesho yenyewe
 
Back
Top Bottom