matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Mpja kwa moja kwenye mada
Wazazi wengi wanakomaa kulipa ada kubwa na kujitoa muhanga kiuchumi ili watoto wao wasimame. Kusudi lililojificha nyuma ni ili mtoto wao akifanikiwa awasaidie kimaisha.
Wazazi wanavizia mahari za watoto wao wa kike. Wanapambana watoto wa kike waolewe na wenye uwezo ili na wao wanufaike na sadaka za mkwe.
Mzazi mmoja nimemuona hadi anafukuza mke wa mtoto wake akidai huyo dada anania ovu za kutaka kuchukua mali za mtoto wao.
Hii tabia kwa mtazamo wangu ni miongoni mwa chanzo cha umasikini.
Sisi watumishi tunaamini ni Jukumu la mzazi kuacha urithi kwa watoto na wajukuu wake na sio kuvizia urithi wa watoto wake.
Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
Mithali 13:22
Wazazi tubadilike. Tuanze kupambana kutafuta mitaji ya watoto wetu sio kusubiri mahali za watoto.
Tupambane kutafutia watoto makazi bora sio kuvizia waje watupe makazi bora.
Huu utegeaji unarudisha nyuma maisha. Simba anamuandaa mtoto wake kuwa mfalme wa nyika sisi tunaandaliwa kuwa chanzo cha mapato na unafuu wa waliotulea.
Hii haijakaa sawa.
Nini maoni yako.
Mtumishi Matunduizi.