Nini kinaendelea kuhusu Novena ya Mtakatifu Ritha wa Kashia? Mbona imebamba sana?

Wahi mirembe
 
asa ushindwe kuomba direct Kwa Mungu unaomba Kwa Rita hii imekaaje asee? Mimi naomba Kwa Mungu direct. Kila mtu na Mungu wake na Imani yake
Kuombewa na Watakatifu ni imani ya Wakatoliki, kama vile kuombewa na wachungaji, mitume na manabii kwa Waprotestanti. Kila mtu abaki na imani yake, kila mtu aombewe na anayemuamini 😂😂😂
 
MTAKATIFU NI MUNGU PEKE YAKE


Hao wengine ni Vibaka kama Vibaka wengine,ni mtu mpumbavu pekee anayemuona mwanadamu mwenzie Kuwa mtakatifu!
Uzuri wakatoliki hatunaga muda wa kubishana au kuutetea ukatoliki.
Unajipa makasiriko ya bure tu...
Si bora mtu anayewaza kuna watu wamejitahidi kwa ukamilifu kuliko mtu anayewaza kwenda kuoa mabikra 72...
 
MTAKATIFU NI MUNGU PEKE YAKE


Hao wengine ni Vibaka kama Vibaka wengine,ni mtu mpumbavu pekee anayemuona mwanadamu mwenzie Kuwa mtakatifu!
1Pet 1:15-16
bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
 
Ishi maisha ya toba kila siku hii ndio sifa ya kuwa mtakatifu na mwenye haki
 
Sijawahi kuisali novena ya mtakatifu Ritha Ila huwa napenda ya huruma ya Mungu. Na kwangu binafsi huwa inafanya kazi

Sala, sadaka na matendo mema. Hizi combinations ukizifanya huwa zina nguvu sana kiimani haswa wakati wa mfungo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…