Nini kinaendelea kuhusu Novena ya Mtakatifu Ritha wa Kashia? Mbona imebamba sana?

Nini kinaendelea kuhusu Novena ya Mtakatifu Ritha wa Kashia? Mbona imebamba sana?

Mimi niliambiwa na mtu nikabisha kabla hata sijaanza kuisali usiku nikiwa nimelala nikamuona huyo mama kavaa manguo marefu nilishangaa sana

Asubuh nikaenda kununua vitabu viwili vya novena kimoja mtakatifu Rita kingine mtakatifu Philomena

Ile nafika tu nyumban nikatokewa na kasichana kadogo kazuri kananambia kenyewe Nika mtakatifu Philomena

Niliogopa vibaya


Huyo mtakatifu Philomena ni baraa utakuja kunikumbuka ukibeep ana piga mda huo huo tena hakawii dakika hiyo hiyo
Wahi mirembe
 
asa ushindwe kuomba direct Kwa Mungu unaomba Kwa Rita hii imekaaje asee? Mimi naomba Kwa Mungu direct. Kila mtu na Mungu wake na Imani yake
Kuombewa na Watakatifu ni imani ya Wakatoliki, kama vile kuombewa na wachungaji, mitume na manabii kwa Waprotestanti. Kila mtu abaki na imani yake, kila mtu aombewe na anayemuamini 😂😂😂
 
MTAKATIFU NI MUNGU PEKE YAKE


Hao wengine ni Vibaka kama Vibaka wengine,ni mtu mpumbavu pekee anayemuona mwanadamu mwenzie Kuwa mtakatifu!
Uzuri wakatoliki hatunaga muda wa kubishana au kuutetea ukatoliki.
Unajipa makasiriko ya bure tu...
Si bora mtu anayewaza kuna watu wamejitahidi kwa ukamilifu kuliko mtu anayewaza kwenda kuoa mabikra 72...
 
MTAKATIFU NI MUNGU PEKE YAKE


Hao wengine ni Vibaka kama Vibaka wengine,ni mtu mpumbavu pekee anayemuona mwanadamu mwenzie Kuwa mtakatifu!
1Pet 1:15-16
bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
 
Hahaha Acheni haya mambo, Yesu mwenyewe alisema 'Alikuja kwa ajili ya wenye dhambi" sasa ikiwa Novena ni kwa wasafi, mbona unapoteza ladha ya kusali na Kuomba.

Tuna sali kwa kuamini sisi ni binadamu na siyo wakamilifu, tunatenda dhambi za kila aina, na kumbuka hakuna palipoandikwa au kusema kuangalia makalio facebook ni dhambi, ile ni burudani kama mwingine apendavyo beer, au kuangalia mpira. sasa walokole kila msicho kitaka nidhambi.

Tusihukumiane, tuache jukumu la hukumu libaki kwa Mungu, mimi na wewe hatujui ya rohoni/moyoni wala akilini, tunaona yaonekanayo kwa macho tu.
Ishi maisha ya toba kila siku hii ndio sifa ya kuwa mtakatifu na mwenye haki
 
Sijawahi kuisali novena ya mtakatifu Ritha Ila huwa napenda ya huruma ya Mungu. Na kwangu binafsi huwa inafanya kazi

Sala, sadaka na matendo mema. Hizi combinations ukizifanya huwa zina nguvu sana kiimani haswa wakati wa mfungo
 
Back
Top Bottom