Nini kinafanya Wazazi walio wengi kumpenda mtoto mmoja zaidi kuliko wengine?

Hongera mkuu ila kuna yule mmoja unampenda zaidi kidogo japo haipo wazi kwa sababu unatambua na hasa kwa experience yako ya nyuma.
 
MAma yangu anawapenda watoto wa 3 mimi nilipendwa na baba yangu sana alipokufa nililia sana niliona ndio mwisho wangu sasa hivi nipo na yuda ambaye ni bi mkubwa na mayuda wenzake
 
Fafanua kwanini alibadilisha
 
Yeah hii naona inakuja automatically.
Mama yangu anatupenda wote ila.. baba alikua na love sana na watoto wa kike

Mama yangu ana love sana na watoto wa kiume

Mimi pia na watoto wa kiume wawili mmoja anamaliza standard seven mwakani

Nina bint yangu kafanana na mama angu nakapenda sana 2years age

Pia na kijana wa 1 years age huyu mzee wangu kabla hajafa alimpa jina la kimila kama mbarikiwa/ mteule / mrithi wa ukoo
 
Pole sana kaka, mama alipitiliza sana kwenye huo upendo kwa kaka yako. Na ipo hivyo kwa familia nyingi tuu.

Mithali ninasema mtoto mpumbavu ni mzigo kwa mama. Msamehe tu ubure mama yako. Na hongera kama unalea watoto wako kwa usawa.
 
Upendo wa mzazi hauambatani na vitu au mwonekano au tabia, ni pure love.Kuna mtoto watu wanapata baada ya kuangahika sana, wengine kipindi kigumu n.k
Hakika kaka. Upendo wa mzazi haufananishi na kitu chochote.
 
Kwa uzoefu wangu, nimeona mara nyingi watoto wanaokuwa wamepitia matatizo wakati wa kukua kwao mfano magonjwa sugu, uzazi wa shida sana, kunusulika mimba kuharibika, au kazaliwa kipindi cha ufakara kwenye familia na kukosa mahitaji muhimu kulinganisha na wenzake hao mara nyingi huwa wannapendwa zaidi....wazazi huwa wanaona ni kama kuishi kwao ni bahati.
 
Ni kweli japo binafsi nimejitahidi kuwapenda wote

Labda huko mbele ya safari nikisikia wameanza kupanga mipango ya kunitanguliza ahera ili wapate kugawana Urithi
Wazazi hupenda watoto watiifu Mimi ni MTIIFU mnyenyekevu sana kwa wazazi na sikuwai kuwa na scandals mbaya

Juzi kati mama akiambiwa na wife kua now nakunywa pombe pia na mchepuko mama ALIPO piga simu alinifokea sana nahakika Navyo mjua anaweza kukupiga mpaka akakun'gata/ kuuma na meno

Napenda kua mtu mzurii siku zoteee na pia lazima watoto wetu tuwakunje angali wabichi
 
Sahihi kabisa

Wazazi hupenda watoto watiifu

Ukiwa na mambo mengi, sio rahisi kupendwa kihivyo
 
Hakika hii inatokea in nature na huo mfano wa mdada kazama kwa bad boy nineona sana
 
Sawa sawa mkuu. Upendo umetokea automatically.
 
Yeah mimi kati ya watoto wote nane ndio nafanana na b mkubwa kuliko wote wengine ni mzee , nahisi ndio sababu
 
Inakuwa ni mchanganyiko wa sababu inatofautiana kwenye familia moja na nyingine.
 
Dah mfano ulio hai na unaishi. Ila jamaa amekuwa na mwisho mbaya. Na mara nyingi wazazi wao wakifariki huwa wanaumia sana watu wa namna hiyo.
Alikuwa kipenzi cha mama! Ukitaka umlize mkumbushe enzi zake. Kitaani walimbatiza jina Sajenti Chotta akisikia hivyo atacheka mpaka jino la 32
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…