Nini kinakuvutia zaidi katika simu janja(smartphones) kutoka kampuni ya Samsung?

Nini kinakuvutia zaidi katika simu janja(smartphones) kutoka kampuni ya Samsung?

Sisi wa Infinix hatuna tatizo la battery kabisa ,kama sumsung na ujanja wao wanashindwa kumanage chaji tu huo si ujinga sasa [emoji23]
Sio Samsung zote. Nyingine zinakaa na charge vizuri
 
Simu moja tamu sana hii
Screenshot_2022-12-24-23-27-34-15_92460851df6f172a4592fca41cc2d2e6.jpg
 
Habari ya muda huu wana jamvi la Jf?

Kama kichwa cha habar kinavyojieleza ningependa kila mmoja aeleze ni Features gani zinamfanya apende smartphone kutokea kampuni hii,

Mimi kwa upande wangu kuna ula feature ya private mode na smart silence zinazoptkana katik S series na Note series huwaga nazielewa sana japo zipo nyingi zinazonifanya Ninunue smartphone ya samsung

WEWE JE?
Google pixel ziko vzr hebu jaribuni
 
Hizo Features zote hazipatikani kwenye A Series halafu S na Note Series Ambapo ndo zinapatikana napo Betri Majanga [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Hapo ndo ninapochanganyikiwa kununua Samsung! ukitaka Battery chukua A Series ila sasa Ule unyama Haupo huko [emoji2297][emoji2297][emoji2297][emoji2297] Ukitaka Unyama Basi Battery Manyanyaso labda uwe na kuanzia S10
Uongo mkuu, me natumia Samsung A50 mbona ina features zote hizo, secure folder ipo, side key ipo, smart lock ipo, bixby ipo, pop up ipo, smart things ipo, samsung health ipo, samsung pass ipo, device care ipo, n.k
 
kutana na mtu mwenye Iphone 13 pro max au 21 ultra,mwambie azime data na kupunguza mwanga kama unavyofanya.

utagundua kumbe infinix yako haikai na charge.
Huzijui Infinix vzuri wewe ,kwa chaji tu hazijambo [emoji23] hayo mengine waachie watumiaji wake
 
Huzijui Infinix vzuri wewe ,kwa chaji tu hazijambo [emoji23] hayo mengine waachie watumiaji wake
Kinachofanya simu ikae chaji
1. Processor iliotumika
2. Battery ukubwa
3. Manufacturing process
4. Aina ya display etc.

Kama ulivyoambiwa juu ukutafuta Samsung yenye battery kubwa, processor ndogo na kioo chenye resolution itakaa na chaji kama Vile infinixi.

Kuna Samsung kibao zinakaa na chaji kuliko infinix.

1. M51 - hii inakaa na chaji sana sababu ya Battery lake kubwa 7000mah
gsmarena_580.jpg

2. A23 5G
gsmarena_601.jpg

3. A42 5G
gsmarena_437.jpg


Kwenye Gsmarena database Infinix inayokaa na chaji zaidi ni Zero 5G
gsmarena_550.jpg


Then Infinix note 11 pro
gsmarena_615.jpg


Waliobakia wote hawajafikia level hizo za ukaaji chaji.

Ukiangalia zero 5G pekee ndio angalau inafikia level za kina M51/A42 na A235G, tena sababu infinix wamejitutumua na kutumia processor ya kisasa yenye manufacturing process ya 6nm na core za Cortex A78.

Huyo ni Samsung ukikutana na Unyama wa Sony ndio unakutana na kitu kama hiki,

gsmarena_522.jpg


Hii simu nyepesi kabisa gram kama 160 tu ila inakaa na chaji balaa masaa 32 mfululizo unaweza angalia video tena za HD. Hivi vivideo vyetu vya quality ndogo inaweza toboa masaa 40.
 
Chief-Mkwawa naomba unisaidie sifa za simu ya Samsung Galaxy Z fold 4, gharama yake pia kwa Tanzania

Ikiwezekana na sifa za iphone 14 plus na bei yake,, natanguliza shukrani
 
Chief-Mkwawa naomba unisaidie sifa za simu ya Samsung Galaxy Z fold 4, gharama yake pia kwa Tanzania

Ikiwezekana na sifa za iphone 14 plus na bei yake,, natanguliza shukrani
Fold 4 ni ile simu ya kukunjua kama Kitabu,

gsmarena_023.jpg

gsmarena_026.jpg


Inakua na vioo viwili cha ndani na cha nje, cha ndani ndo hicho cha kufungua kinakuwa kikubwa kama Tablet na cha nje ndo kinakuwa kama cha kawaida.

Bei zake zinakuwa zimesimama kupita maelezo, milioni 4 mpaka 5.

Sema zipo Flip ambazo bei ni za kawaida kama flagship nyengine around 2m. Flip ipo hivi.

images.jpeg-28.jpg

Kwa wadada ambao hawana matumizi na kioo kikubwa na wanapenda Fashion Flip ina make sense zaidi.

Hizi ni Flagship vitu kama Camera, Perfomance, na hardware nyengine Quality ni kubwa ila ukaaji chaji ni average.

Kuhusu Iphone 14 plus unless unaipata bei rahisi ni vyema kununua Iphone 13 pro max, iphone 14 ambazo sio pro hawaku upgrade soc na zinamiss feature nyingi.

Bei zake hizi nazo ni around 2.5m
 
Back
Top Bottom