Ni hawataki kuja kufanya kazi na mijitu mijizi, mizembe na michafu
Walifanya kazi zamani na wale watanganyika waliostaarabika miaka ile baada ya ukoloni
Kwa sasa wao ni kufanya shughuli zao na kuwaajiri nyinyi mafwafwa ya siku hizi mpelekeshwe kama punda
Sio kweli
Mkoloni alikuwa akibagua watu wote Tanganyika
Mfano hata makazi na sehemu za biasjara kulikuwa na uzunguni ,uhindini na uswahilini
Hivyo wao pia walikuwa wahanga .Hivyo wakati wa kupigania uhuru wahindi pia walijiunga na harakati za kumtoa mkoloni
Alipoondoka wahindi walikubali kuwa sehemu ya serikali na si kuwa walitaka walikuwa na biashara zao na viwanda wakati huo wao.walikuwa ndio wasomi wengi.Wakakubali kusaidia nchi kwa muda ikae sawa kisha warudi nafasi zao
Ndio maana kipindi hicho hadi waziri wa afya Nyerere ilibidi amuombe Padre Daktari l Stirling mkatoliki mzungu ashike sababu katoliki wao walikuwa wazoefu kwenye mahospitali na Tanganyika haikuwa na wasomi wa fani ya afya wakubwa
Viwanda ,fedha akampa uwaziri muhindi mwenye biashara na Viwanda Amir Jamal
Kwenye serikali walikuweko wengi sana tu
Walikaa kwa muda wakarudi kwenye biashara zao.
Serikalini wengi hawaonekani kwa sababu hao watu weupe wahindi na waarabu biashara zao huendeshwa na familia nzima sio mtu mmoja .Kila mtu awe mtoto hupewa kitengo cha kuhudumia.Tofauti na sisi weusi unakuta mzazi ana biashara hata tano.mfano ana mashamba,ana malori,ana mabasi ana mashine za kusaga ana biashara ya maduka unakuta ni yeye tu anazurura kote kusimamia na watoto anao na mke au wake anao.Wenzetu tofauti.Na wanapenda hilo kuwa sehemu muhimu ya family business kuliko kuajiriwa Serikalini
Tofauti na waswahili baba unamkuta ana biashara mfano ya Hospital watoto wake wanaenda kusomea ubwana shamba waajiriwe Serikalini kama afisa kilimo
Sasa unakuta nafasi za ajira zinagombewa na watoto maskini na watoto wa wafanyabiashara wakubwa waswahili ambao kwa hali ya kawaida walitakiwa wabaki kwenye family business za wazazi wao .Ndio unakuta mzazi mswahili mfanyabiashara mkubwa akifa na biashara inakufa sababu hakuna mtoto yuko.tayari ku risk kuacha kazi yake ya ajira hata kama ina kipato kidogo aende kusimamia biashara asiyoijua kabisa sababu alikuwa hashirikishwi inakufa wakati ya wahindi na waarabu inaendelea tena kwa kasi kubwa
Mifano mtu.Kama ASAS baba yao alikufa siku nyingi mwanzilishi wa hiyo kampuni lakini ona watoto wanavyoipaisha kampuni
Ukija Azam mzee Bakheresa kazeeka sana watoto ndio wameshika kampuni inaenda vizuri mno
Uje kampuni ya Dewji Mzee Dewji alishataafu kuendesha kampuni sababu ya uzee kamwachia mwanawe Mo Dewji angalia Mo Dewji anavyoipaisha kampuni
Waswahili tungeiga wahindi na waarabu kwenye family business hakika tatizo la ajira Serikalini lisingekuwa kubwa kana sasa hivi watoto wa wafanyabiashara wangekuwa kwenye biashara za wazazi wao wakiziendesha na kuzipaisha ajira Serikalini zingebaki kwa watoto wa wengine wasiotoka familia za wafanyabiashara na pia ingesaidia biashara za waswahili kudumu na kupanuka kwa mawazo mapya ya kizazi kipya