Kwa kazi isije kuwa unafanya kazi kwa wahindi unasema nawe unakaziMakazini kuna vita nyie??
Kila nako enda kufanya kazi vita inanizidia nipo sehemu ya tatu sasa kote vita hizi zimenishinda maadui zangu wananishinda….
Nadhan ni kwasababu ya personality yangu.
Mi si mtu wa kujipendekeza
Sina shobo
Nafanya kazi yangu naenda nyumban
Lakini game inaonekana ina mbinu nyingi na chafu zaidi.
Wakongwe mnipe mbinu
NB: kama huna kazi au hujawai ajiriwa uwe msikilizaji
Nipo kwenye same situation nayazoom makundi yote mawili.Nilifanya kazi sehemu moja hivi kulikuwa kama kuna makundi mawili yenye ushawishi pale kazini,
Kazi zinaenda lakini,kuna u team A na B
Mimi,walishindwa kunijoin team yoyote maana kila team ni kama unapokea invitation lakini na decline
Kwa hiyo hizo team zote zikaanza kunijadili,kwa pamoja uku mimi nikiendelea na kazi heshima kwa kila mtu mpaka mlinzi getini,salamu kila mtu,majukumu kwa asilimia 100%
Mpaka pale kazini mimi ndiye nilikuwa mfanyakazi ambae naweza kuwasiliana na kila kundi,baadae nilikuja realize wale wengi walikuwa ni ajira zao za kwanza hawajui haya maswala ya makazini huwa yanakuwaje
Hata Mimi nakumbuka watu wanasema ongea na madam, utaishi vipi ukitoka hapa, utarud kijijini,Nilikaa siku mbili bila kulala vizuri usiku baada ya mkataba wangu kuisha na boss kukataa ku-recommend tu niongezewe
Lakini sasa naamini pengine pale sikuandikiwa...nilipewa ushauri wa kwenda Bagamoyo kwa mtaalam lkn nilikataa, wengine wakasema niende kwake boss nikamuombe, pia niligoma..sababu kazi nying nilifanya mimi na boss alkuwa kilaza tu
Mungu kanipa serikalini na malipo mazuri kweli
Ehwatu bana
Hii iko sana , dawa ni moja tafuta mtandao ulio juu ya boss wenu anaepelekewa taarifa ngoma drooHapana sina kosa ila mara nyingi ni watu wanatengeneza maneno na skendo, watu wanaojipendekeza kwa maboss ndo wanatupaka matope
Tafuta mtu avunje mayai yalioandikwa kiarabu mlangoni kila wiki mara moja
Halafu wewe pita yakanyage kama huyaoni
Watakuogopa tu
Nakubalijaribu kuangalia unakosea wapi ujirekebishe ukijiona huna kosa kuwa bize na mambo yako utawashinda
Kuna mijitu mingine ,hata ukifanya hivi bado kuleta chokochoko tu, unakua sehemu majitu yanafikili upo pale kuchukua nafasi zao kumbe wewe upo na malengo tofauti, aya dawa yao kama upo na ushahidi ni kuyachana live na boss kama ndo mpokea majungu mfuate mweleze seriously, wakati mwingi woga uliopindukia makazini ndo husababisha yote.Out shine
?
Maana yake unapoenda kazini au upo sehemu , usiwaoneshe kuwa wewe ni smart kuwazidi wenzako.
Hii itakueletea mgogoro wewe na workmate zako.
Unachobidi ni kutimiza majukumu yako Ila usiwafanye wajue kuwa unawafunika hii ni hatari hasa katika Jamii zetu za kiswahili.
Hapa mkuu umeandika hoja , haya mambo yasikie tu, kama hujayapiatia, kunanyakati itakulazimu kutumia njia ya kibabe ili wajinga wa namna hii kwenda nao sawa ,Pole sana ndugu.
Ni kweli kabisa kuwa chuki na fitina katika maeneo ya kazi ni jambo lisilo epukika, Mara nyingi, unaweza kujikuta unachukiwa bila sababu na wafanyakazi wenzako. Wengine huenda mbali zaidi na kukufitinisha kwa bosi au msimamizi wenu wa kazi, wakilenga kuharibu sifa yako mbele ya uongozi na wafanyakazi wenzako.
Kwa mtu ambaye hajawahi kupitia hali kama hii, huenda asielewe uzito wake. Lakini hali hii ipo na inaumiza hasa pale unapojitahidi kujenga maisha yako, kuwa na bidii kazini na kuwa na msimamo thabiti wenye kufuata mambo yako pekee. Pale unapokuwa mtu wa kazi, mwenye mipango, na mwonekano wako ukawapita wengine — basi tegemea mapambano makubwa. Lakini, tambua kuwa hupaswi kuacha. Simama imara. Pambana hadi ushinde.
Nimewahi pitia Hali hii kazini kwangu,
Nilifanya kazi kituo kimoja, kisha nikaamua kubadilisha na kwenda kituo kingine. Nilipowasili, baadhi ya wafanyakazi wenzangu wa kiume walinionyesha ukaribu wa ajabu: walitaka nikawaone au tuonane mara kwa mara, walinipigia simu baada ya kazi kuniomba tukutane tupate Moja baridi, shida ikawa mimi ni mtu nisiyependa mazoea. Sipendi kutembea hovyo pasipo sababu, na huwa mchaguzi sana watu ninaofanya nao ukaribu.
Siku zilivyoenda, hali ikabadilika. Licha ya wao kuwa na elimu kubwa, walikuwa wakiniona kama mshindani kwa sababu ya kipato changu kizuri. Wakaanza ugomvi na maneno ya kejeli. Kilichoniokoa ni kujiamini kwangu na misimamo yangu thabiti.Niliwajibu kwa maneno yenye msimamo mkali sana,"Mimi si mtu wa kuyumbishwa. Ukija kwangu kwa heshima, nitakuheshimu. Ukija kwa dharau, tutaelewana kwa lugha hiyo hiyo."
Walikuwa watatu dhidi yangu mmoja, lakini walikubali kuwa sina mchezo. Leo hii tuko sawa, japokuwa sijawahi kuwa na mazoea nao tena.
Ushauri wangu kwako:
Simama kama mlima. Usitetereke kwa maneno au vitendo vya watu wanaokosa kuelewa dhamira yako. Siku moja, hao hao watatambua thamani yako na kukusifu kwa kuwa mtu mwenye misimamo
isiyoyumbishwa.