Genius Man
JF-Expert Member
- Apr 7, 2024
- 3,558
- 7,935
Inaonekana bado hujaelewa kama unatafuta kweli basi mimi nitakuambia yaliyo kweli sikiliza.Sasa mkuu kwa maelezo haya huoni kwamba biblia inatambua ubatizo kwa jina la Yesu Kristo na sio kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu?
Hilo jina la yesu ndio huyo huyo mungu wa sika wa yakobo na Ibrahim vyote ni vitu sawa hivyo hakuna hoja hapo unayotaka nikisema nimeamini kwa mungu wa mbinguni tayari nishamtaja huyo yesu.Wewe ndie unaekalili na kuaminishwa isivyo mkuu. Nionyeshe andiko katika biblia linalounga mkono hoja yako.
Mimi naanza na hili
Marko 16:16-18
16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
Hapana, nafikiri hapa unajizuia kuukubali ukweli, na kukataa moja kwa moja kazi ya Roho Mtakatifu aliyekuwa ndani ya mitume.Kubatizwa kwa Jina la Yesu maana yake ni kubatizwa kama Yesu alivyoagiza SIO kubatizwa kwa Jina moja la Yesu.
AminaUbarikiwe sana kwa ufunuo huo
Mathayo 7:22Mimi naweza kutoa pepo kwa jina la baba na mwana na roho kinacho angaliwa ni imani sio jina, ndio maana kuna watu wanaweza kutumia jina la yesu na pepo lisiondoke pia usikalili msingi ni imani, mungu ni mwelewa sana anasikia na atatenda kutokana na imani yako hata ukitumia mungu wa Ibrahim wa usaka na yakabo pepo litakimbia.
Habari Wakuu.
Nimekuwa nikifuatilia mafundisho mbalimbali katika makanisa kuhusu somo la Ubatizo (Baptize), kwa sehemu kubwa kila inaonekana kila kanisa Lina namna yake ya uelewa juu ya ubatizo.
Hoja yangu ni hii, Kama dini ya kikristo muongozo wake ni Biblia. Nipo tayari kutoa kiasi cha Tsh milioni 5 kwa atakaye nionyesha ni wanafunzi gani au watu gani katika biblia waliowahi kubatizwa kwa Jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
Ukisoma Mathayo 28:19 yesu aliwaagiza wanafunzi wake wakawabatize watu hivyo baada ya yeye kuondoka.Habari Wakuu.
Nimekuwa nikifuatilia mafundisho mbalimbali katika makanisa kuhusu somo la Ubatizo (Baptize), kwa sehemu kubwa kila inaonekana kila kanisa Lina namna yake ya uelewa juu ya ubatizo.
Hoja yangu ni hii, Kama dini ya kikristo muongozo wake ni Biblia. Nipo tayari kutoa kiasi cha Tsh milioni 5 kwa atakaye nionyesha ni wanafunzi gani au watu gani katika biblia waliowahi kubatizwa kwa Jina la Baba, Mwana na Roho mtakatifu.
Ni kweli kabisa, baada ya Yesu kuondoka ni watu gani ulio waona au kuwasoma kwenye biblia waliobatizwa kwa ubatizo huo wa kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu?Ukisoma Mathayo 28:19 yesu aliwaagiza wanafunzi wake wakawabatize watu hivyo baada ya yeye kuondoka.
Je unaona tofauti gani ya kusema kwa Jina la Yesu na kwa jina la baba , Mwana na Roho MtakatifuWapi katika Biblia tunaweza kuona wanafunzi au watu waliobatizwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Mathayo 28:19?
Sasa tuchambue kwa ushahidi wa maandiko:
1. Amri ya Yesu mwenyewe – Mathayo 28:19
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.”
Hapa Yesu mwenyewe anatoa agizo kwa mitume wake kabla ya kupaa mbinguni. Hii ndiyo amri kuu ya ubatizo, na inatajwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.
2. Utekelezaji wa agizo – Matendo ya Mitume
Watu wengi walibatizwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, lakini kwa jina la Yesu Kristo:
a) Matendo 2:38 – Siku ya Pentekoste
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo…”
b) Matendo 8:16– Watu wa Samaria
“…kwa maana alikuwa hajamshukia hata mmoja wao ila walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.”
c) Matendo 10:48 – Kornelio na watu wake
“Akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo.”
d) Matendo 19:5– Wanafunzi wa Yohana
“Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.”
Hoja ya Kulinganisha:
Ingawaje agizo lilikuwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, utekelezaji wake katika matendo ya mitume wote waliobatiza walitumia jina la Yesu Kristo. Hii imeibua mijadala ya kiteolojia juu ya kama “jina” hilo linawakilisha utimilifu wa Baba (Mungu), Mwana (Yesu), na Roho Mtakatifu ndani ya utambulisho wa Yesu Kristo.
Mwisho kwa Ushahidi:
Ushauri wa Kiutafiti:
- Hakuna maandiko katika Biblia yanayoeleza moja kwa moja kwamba mtu alibatizwa kwa kutajwa maneno “kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” wakati wa tendo la ubatizo.
- Hata hivyo, maandiko yako wazi kwamba agizo lilitolewa na Yesu mwenyewe kwa maneno hayo (Mathayo 28:19), lakini mitume walibatiza kwa jina la Yesu Kristo, wakiamini kuwa ndilo jina lililobeba mamlaka ya Utatu mtakatifu.
Tafsiri ya “jina” katika Mathayo 28:19 kama “Yesu” inatokana na fundisho la kuwa Yesu ndiye utimilifu wa Mungu katika mwili (Kol 2:9). Ndiyo maana ubatizo kwa jina la Yesu Kristo unaonekana kuwa ni utekelezaji wa ile amri ya Mathayo 28:19.
Niwekee mil 5 sasa na Ubarikiwe !
Baba sio jina walamwana sio jina wala roho mtakatifu.Mathayo 28;19
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Wapi katika Biblia tunaweza kuona wanafunzi au watu waliobatizwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu kama ilivyoandikwa katika Mathayo 28:19?
Sasa tuchambue kwa ushahidi wa maandiko:
1. Amri ya Yesu mwenyewe – Mathayo 28:19
“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu.”
Hapa Yesu mwenyewe anatoa agizo kwa mitume wake kabla ya kupaa mbinguni. Hii ndiyo amri kuu ya ubatizo, na inatajwa kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.
2. Utekelezaji wa agizo – Matendo ya Mitume
Watu wengi walibatizwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, lakini kwa jina la Yesu Kristo:
a) Matendo 2:38 – Siku ya Pentekoste
“Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina la Yesu Kristo…”
b) Matendo 8:16– Watu wa Samaria
“…kwa maana alikuwa hajamshukia hata mmoja wao ila walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.”
c) Matendo 10:48 – Kornelio na watu wake
“Akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo.”
d) Matendo 19:5– Wanafunzi wa Yohana
“Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.”
Hoja ya Kulinganisha:
Ingawaje agizo lilikuwa kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, utekelezaji wake katika matendo ya mitume wote waliobatiza walitumia jina la Yesu Kristo. Hii imeibua mijadala ya kiteolojia juu ya kama “jina” hilo linawakilisha utimilifu wa Baba (Mungu), Mwana (Yesu), na Roho Mtakatifu ndani ya utambulisho wa Yesu Kristo.
Mwisho kwa Ushahidi:
Ushauri wa Kiutafiti:
- Hakuna maandiko katika Biblia yanayoeleza moja kwa moja kwamba mtu alibatizwa kwa kutajwa maneno “kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” wakati wa tendo la ubatizo.
- Hata hivyo, maandiko yako wazi kwamba agizo lilitolewa na Yesu mwenyewe kwa maneno hayo (Mathayo 28:19), lakini mitume walibatiza kwa jina la Yesu Kristo, wakiamini kuwa ndilo jina lililobeba mamlaka ya Utatu mtakatifu.
Tafsiri ya “jina” katika Mathayo 28:19 kama “Yesu” inatokana na fundisho la kuwa Yesu ndiye utimilifu wa Mungu katika mwili (Kol 2:9). Ndiyo maana ubatizo kwa jina la Yesu Kristo unaonekana kuwa ni utekelezaji wa ile amri ya Mathayo 28:19.
Niwekee mil 5 sasa na Ubarikiwe !
Siri ni maana ya ubatizo .Mtoto anapozaliwa akamwagiwa maji ya mto,ikanenwa nakutenganisha na shetani Kwa maji haya,kazi kwisha,zingine mbwe mbwe tu,siri ipo ndani ya maji,na neno litamkwalo!
Kweli anajigawaBaba sio jina walamwana sio jina wala roho mtakatifu.
Mimi ni baba mimi ni mwana mm ni mjukuu.
Mungu akiwa yehovaa
Alipokuja ulimwenguni huyo huyo yehova akawa mwana. Emmanuel.
Tito 2:13
[13]tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
Anapoondoka nakurudi kama roho huyo huyo yehova anakuwa roho mtakatifu.
Izo ni ofisi za Mungu mmoja ambae ananafsi moja tuu.
Isaya 45:15
[15]Hakika wewe u Mungu ujifichaye nafsi yako, Ee Mungu wa Israeli, Mwokozi.
Na hii ndio sababu ukristo wakimadhehebu umeshindwa kuwashawishi wayahudi.
Kwa fundisho la kumgawa Mungu.
Isaya 9:6
[6]Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Yesu ndie yule Mungu BABA.