dgombusi
Senior Member
- Sep 3, 2017
- 141
- 200
Kingine ni kwamba kama ni kweli una ndoto za maana na una nia ya kweli ya kuzikamilisha basi hakuna faida wala umuhimu wowote wa wewe kuolewa kwa sasa. Panga muda wa ku-work on your dreams, utakutana na mtu mnayeendana mitazamo on the way au ndani ya hiyo timeline.
Ni kweli kabisa. Anapokuwa katika njia ya kutimiza malengo yake, hasa akiwa kijana katika miaka ya 20’s, ni muhimu kuweka malengo ya jinsi atakavyoweza kuyafikia ndani ya kipindi hicho cha ujana.
Lakini, ni muhimu pia kukumbuka kwamba heshima ya mwanamke ni ndoa.
Kwa hivyo, anapokuwa kwenye harakati za kutimiza malengo yake, ni vyema ajitahidi kujichanganya na kutafuta mwanaume aliye katika uwanja(Field) yake.
Watakutana wakiwa na malengo yanayofanana au karibu, na hii itafanya kuwa rahisi kuingia kwenye mahusiano na mwanaume huyo, kwa sababu wote mna malengo na juhudi zinazoshabihiana.
Ikiwa watakubaliana kuingia kwenye ndoa, itakuwa rahisi kwa mwanaume kuheshimu na kuunga mkono maono yake, badala ya kuzuia au kukatisha tamaa malengo yake.