Nisaidieni kwa wote waliooa na kuolewa

Ni kweli kabisa. Anapokuwa katika njia ya kutimiza malengo yake, hasa akiwa kijana katika miaka ya 20’s, ni muhimu kuweka malengo ya jinsi atakavyoweza kuyafikia ndani ya kipindi hicho cha ujana.

Lakini, ni muhimu pia kukumbuka kwamba heshima ya mwanamke ni ndoa.

Kwa hivyo, anapokuwa kwenye harakati za kutimiza malengo yake, ni vyema ajitahidi kujichanganya na kutafuta mwanaume aliye katika uwanja(Field) yake.

Watakutana wakiwa na malengo yanayofanana au karibu, na hii itafanya kuwa rahisi kuingia kwenye mahusiano na mwanaume huyo, kwa sababu wote mna malengo na juhudi zinazoshabihiana.

Ikiwa watakubaliana kuingia kwenye ndoa, itakuwa rahisi kwa mwanaume kuheshimu na kuunga mkono maono yake, badala ya kuzuia au kukatisha tamaa malengo yake.
 
Hapo kuolewa nakuwa mke Kuna vitu sitavifanya nageuka kuwa wa ndani milele
Na ukisoma sana umri ukawa unazidi kusogea pia kuolewa sahau watu wapo sensitive sana na age kwa sasa , ila yote ya yote ni makubaliano yenu tu ndani ya ndoa maana kuna waliokutana vyuoni wakaona wakiwa bado wanasoma na wakafikia malengo pia .
 
Umri kusogea sioni kama ni ttatizo
 
Bado tu malengo mdada atasahau

Hapana ,akipata mtu sahihi wa kumboost atatimiza malengo yake tena mapema sana ,tumeona wanawake wengi ,wametimiza ndoto zao za kusoma kwa kusomeshwa na wapenzi/waume zao ,kufunguliwa biashara ,kununuliwa magari etc
 
We unamsomesha mpenzi wako tuanzie hapo ...?!
 
Habari zenu,

Naomba kuuliza swali:

Hivi mdada aliye na malengo na ndoto za kutimiza maishani mwake je, akiolewa anaweza kuzitimiza ndoto zake au ndo milango itakuwa imefungwa mazima ya kufikia ndoto zake na kubadilishwa kuwa mke na mama wa watoto
Jambo la kwanza lazima ujue role a mwanamke katika ndoa.

Mwanamke katika ndoa ni msaidizi wa mwanaume, anakuja kumsaidia mume wake kutimiza kusudi au kile ambacho Mungu ameweka kwa huyo mwanaume, kwahiyo mwanamke hawezi akaendelea na mpango wa ndoto zake, labda hizo ndoto zake ziendane na kile cha mwanaume
 
😂😂😂Dah
 
Unamaanisha kusudi ambalo limewekwa kwangu Mimi na Mungu napaswa kulisahau nifoucus na lake?!
 
Hapana ,akipata mtu sahihi wa kumboost atatimiza malengo yake tena mapema sana ,tumeona wanawake wengi ,wametimiza ndoto zao za kusoma kwa kusomeshwa na wapenzi/waume zao ,kufunguliwa biashara ,kununuliwa magari etc

Unamaanisha kusudi ambalo limewekwa kwangu Mimi na Mungu napaswa kulisahau nifoucus na lake?!
Kama linaendana na la kwake, sawa au kama mume wako akaamua kukiwezesha lakini kwa malengo kufanikisha la kwake hapo sawa, lakini sio wewe ukomae na ya kwako na yeye akomae na ya kwake hapo mnakuwa hamjaoana, na hamna maana ya huyo mwanamke kuolewa
 
Habari zenu,

Naomba kuuliza swali:

Hivi mdada aliye na malengo na ndoto za kutimiza maishani mwake je, akiolewa anaweza kuzitimiza ndoto zake au ndo milango itakuwa imefungwa mazima ya kufikia ndoto zake na kubadilishwa kuwa mke na mama wa watoto
Mkuu kwani malengo ya msingi ya mke katika ndoa ni yapi, sio kuwa mke wa mtu kamili, kuzaa na kulea watoto??

Kama sio hayo, basi huyo mke abaki kwa wazazi wake atimize hayo malengo yake ya mfukoni!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…