Nisikilizwe nishauriwe ukweli mtupu nisije kujuta maisha yangu yote

Habari za muda humu

Nitasema ukweli Kama Kuna hukumu Basi nihukumiwe wote tunakosea Hakuna mkamilifu

Nachoitaji ni ukweli mchungu hata kama utaniuma ni sawa ilimradi nisiharibu maisha yangu maana Naona kama shetani amedhamiria kuniharibia maisha

Nimeshaleta story ya Kijana wangu wa kisukuma humu mkanishauri nikashupataza shingo

Huyu mwanaume tuna miaka 3 sasa tangu 2024 na Nina miezi 7 toka nianze kuishi nae..Tulikutana nikiwa na 24 yeye aliniambia ana 27( alinidanganya now ana 35)

Amenitoa nyumbani kwetu kanipeleka mkoa anaoishi yeye(kanda ya ziwa) ndugu zangu wanajua Niko nafanya kazi kumbe nimewekwa kinyumba na msukuma

Amenifungulia Biashara ninayoiendesha mwenyewe kwani aliniambia nitafute wazo la Biashara yeye ataniwezesha ametimiza inaendelea vizuri na yeye hausiki na chochote kwenye hiyo Biashara na ananihudumia vizuri

Changamoto
Tulikuwa na ugomvi mzito tangu mwezi wa 6 baada ya kugundua ana mke (amemlipia mahari wamezaa watoto wawili kwa msukuma ukishalipiwa mahari ni mke tayari)
Ukweli nimeumia sana maana sikutegemea Kama ningekutana na kitu Kama hiki
Lakini mwenzangu yuko kawaida kabisa Kama Hakuna kilichotokea anasema ni kawaida kwao kuoa mitala nitulie Mimi ndio mke mdogo yule atabaki kwenye nafasi yake Kama mke mkubwa na Hakuna anaeachwa

Hii hali inaniumiza Kila nikifikiri mekuaje nimejiingiza humo
Halafu yeye hajali yaani kama Hakuna kilichotokea

Sasa Kuna ex wangu nili soma nae shule tukaachana zamani hiyo kwasababu za umbali amerudi anataka kunioa nawaza nimuache tu huyu nirudi kwa ex au nikae nae tu hivyohivyo

Nishauriwe jamani msianze kunichamba na maneno ya kejeri 🥺🥺
Baki na huyo msukuma wako,hayo mambo ya kuwa na mke msameheane na muanze maisha kwa amani na furaha.Usiogope mini pia nipo Mwanza ukitaka ushauri niambie
 
Samahani wewe una wake wawili au na wewe msukuma??
 
Kwake kutoa mahari anataka hata kesho lakini hata familia yangu utachukuliaje Hilo suala Kama nitakubali
Maisha ni yako.

Kama yuko serious, muambie amuweke wazi na mke mkubwa, ikiwezekana awakutanishe.

Kisha huyo mke mwenzio kwa muda wako jenga naye ukaribu akupe uhalisia wa huyo mume wenu.

Kama atakuwa ana uwezo wa kuwaoa wote wawili, basi kubali.
 
Acha mali za watu nenda kaolewe na huyo ex wako maana msukuma amekujali kila kitu huoni thamani acha izo biashara kaolewe
 
kwa hiyo mkuu unamshauri aondoke navyo huwezi jua roho ya mutu pengne anaweza akaondoka navyo then ikamletea madhara mbeleni kama hataki kuishi naye atenane naye tu au ww unaonaje
Kesi yake ngumu kwa kweli. Lakini kabla hajachukuliwa kwao rasmi hakutambulishwa ukweni?

Lakini kama akiamua kuondoka anaweza kutumia hiyo sababu ya kutoambiwa tangu mwanzo na akaeleweka ila sasa ili kusiwe na misunderstandings ni bora aache kila kitu akichofanyiwa na msukuma yaani hiyo biashara aliyofunguliwa na assets zingine akizinunuliwa kama zipo.

Maana hayo makabika ya kanda ya ziwa kukucharaza mapanga ni dakika 0 tu
 
Maisha ni yako.

Kama yuko serious, muambie amuweke wazi na mke mkubwa, ikiwezekana awakutanishe.

Kisha huyo mke mwenzio kwa muda wako jenga naye ukaribu akupe uhalisia wa huyo mume wenu.

Kama atakuwa ana uwezo wa kuwaoa wote wawili, basi kubali.
Mmmh ameshasema anaweka mambo sawa kila kitu kitakuwa kwenye mstari sasa hivi anataka aniweke vizuri kiuchumi niweze kujisimamia
 
Kesi yake ngumu kwa kweli. Lakini kabla hajachukuliwa kwao rasmi hakutambulishwa ukweni?

Lakini kama akiamua kuondoka anaweza kutumia hiyo sababu ya kutoambiwa tangu mwanzo na akaeleweka ila sasa ili kusiwe na misunderstandings ni bora aache kila kitu akichofanyiwa na msukuma yaani hiyo biashara aliyofunguliwa na assets zingine akizinunuliwa kama zipo.

Maana hayo makabika ya kanda ya ziwa kukucharaza mapanga ni dakika 0 tu
😒😒
 
Habari za muda humu

Nitasema ukweli Kama Kuna hukumu Basi nihukumiwe wote tunakosea Hakuna mkamilifu

Nachoitaji ni ukweli mchungu hata kama utaniuma ni sawa ilimradi nisiharibu maisha yangu maana Naona kama shetani amedhamiria kuniharibia maisha

Nimeshaleta story ya Kijana wangu wa kisukuma humu mkanishauri nikashupataza shingo

Huyu mwanaume tuna miaka 3 sasa tangu 2024 na Nina miezi 7 toka nianze kuishi nae..Tulikutana nikiwa na 24 yeye aliniambia ana 27( alinidanganya now ana 35)

Amenitoa nyumbani kwetu kanipeleka mkoa anaoishi yeye(kanda ya ziwa) ndugu zangu wanajua Niko nafanya kazi kumbe nimewekwa kinyumba na msukuma

Amenifungulia Biashara ninayoiendesha mwenyewe kwani aliniambia nitafute wazo la Biashara yeye ataniwezesha ametimiza inaendelea vizuri na yeye hausiki na chochote kwenye hiyo Biashara na ananihudumia vizuri

Changamoto
Tulikuwa na ugomvi mzito tangu mwezi wa 6 baada ya kugundua ana mke (amemlipia mahari wamezaa watoto wawili kwa msukuma ukishalipiwa mahari ni mke tayari)
Ukweli nimeumia sana maana sikutegemea Kama ningekutana na kitu Kama hiki
Lakini mwenzangu yuko kawaida kabisa Kama Hakuna kilichotokea anasema ni kawaida kwao kuoa mitala nitulie Mimi ndio mke mdogo yule atabaki kwenye nafasi yake Kama mke mkubwa na Hakuna anaeachwa

Hii hali inaniumiza Kila nikifikiri mekuaje nimejiingiza humo
Halafu yeye hajali yaani kama Hakuna kilichotokea

Sasa Kuna ex wangu nili soma nae shule tukaachana zamani hiyo kwasababu za umbali amerudi anataka kunioa nawaza nimuache tu huyu nirudi kwa ex au nikae nae tu hivyohivyo

Nishauriwe jamani msianze kunichamba na maneno ya kejeri 🥺🥺
RUdi ex wangu tujenge maisha.
Note: hata mimi ni msukuma lakini.
 
Back
Top Bottom