Niwaombe watu wa dini wakae mbali na siasa za Afrika

Tume mnaziunda nyuma ya mikamera majibu ya hizo tume nyuma ya pazia, (mifukoni), mwaka unao fuata CAG anaibua tena ufisadi, kikikiki

Kumbe ufisadi ni jadi kwa CCM hauwezi kudhibitiwa nafahamu fika kwenye watu wengi huwezi kukomesha wizi
 
Swala la maendeleo ni swala la wageni ni la nchi na raia wake. Mgeni anazo interests na agenda zake. Kama mwarabu kajenga msikiti kwanini wewe usijenge shule za watoto wenu? Kama mwarabu kakujengea Uwanja mkubwa wa mpira wewe jenga hospitali zenu sasa. Ni upuuzi kusubiria maendeleo kutoka kwa wageni; tumia pesa kutoka kwa watalii kuchimba chuma yenu mkauze na kutengeneza majembe mlime.
 
You're not aware of voting process in Tanzania

Kwa tume hii ambayo imejifungia ambayo katu haisikilizi maoni ya wananchi

Je kwa akili zako hiyo ni tume ya wananchi

Silence surrenders public responsibilities
XI na Putin wana muda gani kwenye Urais wa nchi zao? Je, unaonaje mambo yao?. Narudia tena na tena kuwa sio katiba na tume huru itakayotutoa hapo tulipo, bali utashi na uadilifu wa viongozi na uchapakazi wa kupindukia wa wananchi mmojammoja na vikundi. SIOOO KATIBAAA WALA TUMEEEE. Kuna nchi hata hazina katiba lakini mambo yao yamenyooooka kwa kutumia kanuni, sheria na utamaduni wao tu basi.
 
Waarabu hawajawahi kufadhili hii nchi katika chochote unasema tuwajaribu ? Sikuelewi ? Ukizunguzka Tanzania nzima wanaowatesa wafanyakazi ni waarabu, wahindi na wachina. Unawajaribu kivipi watu wasio na ubinadamu. Wazungu ndio wanaongoza kwa kuleta maendeleo na kulipa na kuwekeza hapa nchini. Waarabu wamefanya nini hapa Tanzania hakuna shule, chuo wala hospitali waliojenga.
 
Mnadanganywa na wanasiasa China asingekuwepo hapa alipo bila kuruhusu wawekezaji kutoka marekani. Wao ndio waliwapa skills wachina na ku boost research zao. Kwa sasa hatuendelei kwa sababu tunakumbatia wahindi na waarabu(GSM, Dewji na Rostam n.k ) nyuma ya kivuli cha uraia wa tanzania. Hatuna haja ya kusubiri wazungu ni kuhamisha huu upendeleo tunaowapa hawa wawekezaji waliopo sasa tuwape watu makini. Na haya makamopuni tuyape masharti ya kutengeneza ajira ili kuinua watu wenye skills . Nimeshatoa mfano wa china huko juu.
 
Tume mnaziunda nyuma ya mikamera majibu ya hizo tume nyuma ya pazia, (mifukoni), mwaka unao fuata CAG anaibua tena ufisadi, kikikiki

Kumbe ufisadi ni jadi kwa CCM hauwezi kudhibitiwa nafahamu fika kwenye watu wengi huwezi kukomesha wizi
Nadhani tuwekeze nguvu nyingi zaidi wapinzani wengi wawe wabunge na madiwani kabla ya kupoteza muda kwenye urais. hata hivyo wananchi hawana imani tena na wapinzani kwa tabia yao ile ya kwenda kuunga juhudi. Yaani wananchi wamepambana katika hali ngumu sana hadi ukaenda mjengoni, lakini ghafla unawasaliti na kwenda kuunga juhudi. Mifano yao ni mingi sana; Msigwa, Prof, Nasari, Kafulila, Dr. Slaa, ................ . Eti Slaa karudi tena atufanye sisi wajinga tena tumpeleke bungeni.
 
Tatizo la kuunga juhudi ni njaa na kurubuniwa ili kujiimarisha kiuchumi
Mfano unadaiwa benki wanataka kuchukua dhamamana, (nyumba), huna hela na kunakuwa na mazingira fulani ya Sinto fahamu utafanyaje hapo usiwashangae wanao unga juhudi kuna mambo mengi kuna kunyamazishwa pia
 
Huna hoja nzzito. Kwani hawa Barrick ni wasandawe? Yule Williamson tuliyempa mgodi wa almasi Mwadui ni mhangaza? Yule Richmond ni mtu wa wapi?
Waarabu hawakupewa nafasi hapa
Kama ni rahisi kwenda kuunga juhudi za CCM kwanini iwe vigumu kwenda kuunga juhudi za mabeberu ukiwa Rais? tutauza nchi tusipokuwa makini wallah.
 
Hili ndilo linasabaisha 'neocolonialism ' kwasasa tunatumia bidhaa zao na utalaamu wao wakibadilisha ama kusasisha inabidi muda wote ucheze kwenye Ngoma yao
 
ni ngumu sana kwa sababu zifuatazo;
1. Wanasiasa ni waumini kwenye makanisa au misikiti yao.
2. waumini wao wanaathirika sana na mambo ya siasa, huwezi kuona muumini wako anaumia ukakaa kimya.
3. wanasiasa, kuanzia Rais mwenyewe, huwa anawaendea kwenye majumba yao hasa wakati wa kampeni.
4. muda wote wakiisema vizuri selikali, hakuna anayesema wakae mbali, watapongezwa na kuonekana wema, ila wakikosoa serikali tu wanaonekana wabaya.
5. serikali inayoogopa kukosolewa ni serikali ovu. kama wewe ni msafi, kwa nini unaogopa wanaokurekebisha?
6. serikali za africa zimejaa rushwa, figisu, mauaji, utekaji, na uonevu, wanajilimbikizia mali ambazo zinatokana na kodi za hawa hawa waumini wao, watanyamazaje sasa wakati wao na waumini wao wanaibiwa? yaani mnataka muwaibie na wasiongee chochote wakiongea mnaona wanafanya jambo baya? kuna asiyejua kuwa ninyi wanasiasa ni wezi na waonezi?
7. waumini wao ni wapiga kura, hata ninyi wanasiasa mkitaka kupata kura huwa mnakuja kwenye majumba yao (kama nilivyokwisha sema), hivyo ni muhimu watu wa dini kuwaelimisha waumini wao kuchagua vizuri, wasije wakachagua shetani.
 
Kwa hiyo tanzania inagawa nafasi ? Barrick analipa laki tatu kama Mo dewji , Bakhressa na Murzah oil ? Basi achana na huyo Twiga cement analipa laki tatu kwa mwezi kama Dangote? Vodacom analipa laki nne kwa mwezi kama Airtel ? SBC Tanzania wanaomiliki Pepsi Tanzania wanalipa swa na Cocacola Tanzania ? Hizi ndizo tofauti ya Mzungu na Waarabu, Wahindi na Wachina. Mzungu ni mzungu tu tatizo tunakumbatia watu ambao sio. Kwa nini Barrick walivyotangaza kuuza mgodi kwa wachina Magufuli alijishusha na kuwalamba miguu wazungu ?Wachina walifanikiwa bila kuwaaalika Marekani ?
 
Kwani huu mfumo wa kisiasa uliopo ulianza na kina chifu Mkwawa? Huoni kuwa asili yake ni hao hao wakoloni? Elimu, afya, sayansi na teknolojia vilianzishwa na Mwanamalundi? Hoja ya uwepo wa Mungu imeletwa na wakoloni, lakini pia hoja kwamba hakuna Mungu imeanza na hao hao. Kwa hiyo ni kutofikiri vema unapowataka viongozi was dini kutojihusisha na siasa waliyoiasisi wenyewe huku Afrika.
 
2. waumini wao wanaathirika sana na mambo ya siasa, huwezi kuona muumini wako anaumia ukakaa kimya.

Acha hizo bhana; Mbona waumini wao wakiwa na njaa, wakikosa ada askofu anakaa kimya? hiyo haiumizi?
 
Kwa akili yako timamu unaona Nchi ipo sawa kabisaa? Na serikali yako ipo sawa? Kama jibu ni ndio basi nikwambie tuu bao lililokuleta duniani basi lingetoka kwa nyeto

NB:Asilimia ulizotaja kwamba wapo kidogo wanaoonewa ndio hao hao tunawazingatia ukitaka kujua nguvu ya watu wachache mdhuru/muue raia yoyote kutoka US,UK etc utaelewa vizuri nachomaanisha
 
Hawa ni wasshika tonge hata hivyo viongozi wa dini wamesoma kuliko wao

Wanaahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza na kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki)
Inafikia hatua sioni hata umuhimu wa elimu wanayopewa watanganyika wenzangu kwa sababu mwisho wao ni aibu😥😥😥
 
Inafikia hatua sioni hata umuhimu wa elimu wanayopewa watanganyika wenzangu kwa sababu mwisho wao ni aibu😥😥😥
Tunaongozwa na wapumbavu, Tanzania upumbavu ni kipaji, mpumbavu ni mtu aliyebobea kwenye jambo fulani lakini hawezi kulifanya kwa weledi wengi wao wanaahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data
 
Tuliza mshono veve.

View: https://youtu.be/-ZBynLezTz0?si=I8WUqY2mz2_9fBk6
 
Nchi haiko vizuri kulinganisha na nchi Gani, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Somalia, Sudan kusini au DRC? Wadanyanye haohao mazuzu wenzako aloo. Wewe ni nani utusemee kwamba tunapata tabu tz? Sisi wenyewe hatuoni? Eti hatuna akili ila nyie tu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…