NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Nmb kitengo cha mikopo hongereni saana kwa huduma zenu nzuri
 
Haya malalamiko tunajisumbua tu, sio kwamba hawayajui! Wanayajua sana na hapa wanatuchora tu tunavyopiga makelele. Complains zinawafikia kila siku na ni hizi hizi ila hawazifanyii kazi.

Wanatuinjoi tu hapa wahuni hawa!

CC NMB Tanzania
 
Last edited by a moderator:
Yaaani inasikitisha sana kuona watu wakipata kaz wanakuwa na viburi, dharau, uvivu, kupenda rushwa na ngono wakati kabla haujapata hyo kaz unakuwa unalalama hooo, jaman ajira ngumu mara unaanza kuomba Mungu sana n.k. Lakin ukishapata unageuka Mungu mtu, tunaumia sana aisee.

Haya mambo sio kweny mabank tu bali imeshakuwa fashion kila idara ya kuhudumia watu. Mi nilitaka kufungua akaunti NMB tawi la Bukoba mjin ila ilibidi niache baada ya kwenda customer care kuuliza taratibu alafu mhudumu anajibu kwa kiburi na dharau ndo nikaenda kufungua CRDB
 

yaani wa shy hapo manonga wanajiskia jamani
wana dharau,jeuri sijui wanajionaje hao watu hapo.

kwa kweli mtwara wanajitahidi sana
kwazo foleni tu hasa kipindi cha mshahara
 
nimesoma uzi wote,ponge na malalamiko watu wanayotoa lakn hamjibu kitu kwenye uzi wenu,hii ni dalili yq dharau pia, mpaka naona nikitoa malalamiko yangu ni kama nitakuwa najisumbua tu wala hakuna msaada
 
Nmb kitengo cha mikopo hongereni saana kwa huduma zenu nzuri

Mkuu HoPage ingekuwa vizuri ukataja branch nadhani ukigeneralize utawachanya watu maana kuna wachangiaji hapa wamelalamikia hicho hicho kitengo cha mikopo
 
Last edited by a moderator:
Bora yenu huko shinyanga,huku mwanza buzuruga plaza unaweza ukapiga mtu, kuna kijana mmoja anaringa utadhani bank yakwao anaongea nakuchat wakati kunalifoleni, wanatabia mbaya sana wakiina foleni ndogo namuda wakufunga umekaribia wanaondika wanamuacha mmoja ndio atuhudumie sujui lengo ni kupata malipo ya ziada au
 
nimesoma uzi wote,ponge na malalamiko watu wanayotoa lakn hamjibu kitu kwenye uzi wenu,hii ni dalili yq dharau pia,mpaka naona nikitoa malalamiko yangu ni kama nitakuwa najisumbua tu wala hakuna msaada
kama hawa tu wanachelewa kujibu malalamiko wategemea nini!
 
Kumbe na NMB ni wale wale. Sasa wanasubiri nini kuja kujibu hoja za watu?
 

Mi pia waliwahi kunipa nikaomba muhudumu ahesabu kwa mashine akagoma akanambia nihesabu mwenyewe akijua sitafanya hivyo nilipohesabu 10000 ikawa hamna
 
Atm zenu songea mjini nijanga mumezijenga hovyo.mtu anatoa pesa anaonekana na kila mtu

Idara ya mikopo rushwa imetawala bandikeni namba za simu kila tawi mle ndani ili mtu akiombwa rushwa awapigie namba ziweke ssehem wazi
 
Nmb mbona mnawasanifu wateja wenu? Mmefungua kauzi haka watu wakadhani mtawajibu kumbe mambo ni yaleyale! Badilikeni kwa kweli.
 
Hii ni hatua muhimu nawaponfeza.
1. Kuna watu hupiga simu wakijitambulisha kuwa ni wafanyakazi wa NMB lakini huulizia habari nyeti.
Changamoto ni kujua kama kweli ni wafanyakazi wa NMB.

Mara moja mwaka juzi niliibiwa kiasi fulani cha pesa kwa njia hii.
Naomba wafanyakazi wenu wasikae kituo kimoja zaidi ya miaka 5.

Wanazoea na kuanza uzembe. Hata rushwa kwenye mikopo inatokana na hili.

Pale Muleba kuna wafanyakazi wako pale miaka zaidi ya mitano. Wana lugha mbaya na wanakwepa wateja.

Mwisho NMB inajihusishaje na international trade? Omugishagwe@yahoo.
 

Vipi zile fedha zetu mlizotutoza kwa njia isiyohalali ya kukatwa shs 1000 wakati mtumishi/rafiki akiweka fedha kwenye account miaka ya nyuma, tena nikiwa nimekopa kutoka benki, lakini wanataka mimi mwenyewe nipeleke fedha beki. Je zile fedha mtaturudishia lini?
 
Kesho naenda kufunga akaunti yangu ya STANBIC hawafai pesambili!!
 
NmB Hai pale kuna jamaa mmoja anaitwa Dennis, kwanza mcheShi na kila mara mtani yani hadi unajiskia mwanafamilia. NmB muwaangalie hawa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…