Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawa NMB bure kabisa mi nshalalamika nshatuma e mail saana!! Kipindi naomba mkopo niliupata lakini ilibidi nihonge!! Sidhani kama ntakopa tena NMB, na msipojiangalia TPB atachukua wateja wenu. NMB itabak benk ya kuchukulia mishahara tu.
Malalamiko yangu ni NMB Shinyanga branch. Hamna customer care, wana mapozi sana kuchukua statement tu unaweza ukakaa hata masaa 3, wafanyakaz wako busy kwenda kunywa supu, sometime teller mmoja yaani kero tupu.
Ila ukiwa na vibuku tano tano wanakusaidia kupotisha slip kwa nyuma!! Kwa nini nihonge ili niwekewe hela fasta. Kwani mkiweka matteler madirisha yote mtakufa?? Kwa nini muentertain biashara ya kujuana?? Nmeandika barua kwenye suggestion box ila hamna changes.
Nmb Manonga Branch ni kero!! Hapo bado Kero za ATM
kama hawa tu wanachelewa kujibu malalamiko wategemea nini!nimesoma uzi wote,ponge na malalamiko watu wanayotoa lakn hamjibu kitu kwenye uzi wenu,hii ni dalili yq dharau pia,mpaka naona nikitoa malalamiko yangu ni kama nitakuwa najisumbua tu wala hakuna msaada
Nilisajili Account yangu ikiwa na vielelezo vyote per BOT requirements
Wame block account yangu bila maelezo ya
kutosha. Nimepeleka details zangu upya, hii ni wiki ya pili hazijafanyiwa kazi.
Ukichukua pesa dirishani utabambikiwa noti za mia tano tano mpaka utakoma! Imagine nilipewa Tshs 500,000 katika note za 500!
NBC ipo ICU kweli!
Mi pia waliwahi kunipa nikaomba muhudumu ahesabu kwa mashine akagoma akanambia nihesabu mwenyewe akijua sitafanya hivyo nilipohesabu 10000 ikawa hamna
Ndugu wana JamiiForums,
Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.
Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.
Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:
1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:
Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe Siri)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.
4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom