Ninaswali moja la kuuliza na ushauri pia. Nikianza na swali, ni hivi, nilifungua account ya mke wangu 2012 au 2013 katika tawi moja hivi hapa nchini, katika kipindi cha kusubiria card (ATM) usumbufu ukajitokeza hadi mke wangu akaanza kuwa mkali kwa wahudumu maana ahadi zilizidi sana ikabidi ni mtulize kumwambia awe mvumilivu.
Ilishindikana kabisa kuipata tukaambiwa tuanze upya kufanya utaratibu wa kuomba card kisa document hazionekani. tukajitahidi kuwaletea document walizohitaji ile karatasi unayopewa mara ya kwanza kama temporary lipo na linatumika kuchukua hela dirishani, ikatokea tumesafiri kwenda mkoa mwingine lile karatasi wakalikataa kuchukua hela, tukaamua kuachana nao ila hela ilibaki kidogo kama 70,000/-, je, naweza kupata hizo hela?
Ushauri wangu kwenu ni kuhusu bank statement kwenye NMB mobile, ipo shallow sana mistari mitatu minne halafu maelezo hayajitoshelezi, naomba ionyeshe fedha iliyoingia toka wapi na tarehe gani. kwa leo ni hayo machache.