NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB kiukweli mnaboa ktk nmb mobile,huduma hazikamiliki hela inatoka ktk akaunti ya nmb,ukiwauliza wanakuambia mtandao,ila hela itarudi.shughuli ni hiyo hela kurudi ktk akaunti unaweza ukalia, halafu wanasisiiza watu wajihudumie, kwa style hiyo foleni itakuwepo miaka nenda rudi sababu watu wataogopa kujihudumia ukizingatia mtu anataka hela anashida nayo ataona ni bora akomae ktk foleni kuliko hizo jihudumie.

Liangalieni hilo.
 
Mbona watu huku hamzungumzii mikopo inayotolewa nmb! Je maafisa mikopo wanatoa huduma bila vikwazo? Je hakuna harufu ya rushwa katika upande huo?
 
NMB Tanzania, ATM zenu hazifanyi kazi kila ifikapo jioni na tatizo kuendelea hadi kesho yake hasubuhi, pia tatizo hilo siku za week end. je waweza kueleza tatizo ni nini?
 
Last edited by a moderator:
Mara nying huduma ya atm inazngua sana ktk baadh ya matawi yenu,mtu anakamilisha muamala lkn anaishia kupata rist bla hela kutoka, ndo nn hyo?? Mna2boa sana,,,,,,,, mfano MANONGA BRANCH-shinyanga, n shida 2pu
 
katika dunia ya ulimwengu wa sayansi na teknolojia ya kiwango cha juu kabisa na mambo mengi yakiwa katika almost 4th generation kuendelea kuwa na makadi yasiyo ya visa wala mastercard ni aibu.

Jaribuni basi kutupeleka wateja wenu angalau kwenye card tutakazoweza kutumia na kununua kwa card zetu katika masoko ya mitandaoni kama ebay, amazon na mengineyo bila wasiwasi.

Dunia ya leo imebadilika sana hebu jaribuni basi na nyie kwenda na hiyo kasi ya mabadiliko ili wateja wenu tuwe na mawanda mapana zaidi ya kitumia account zetu
 
Baadhi ya maofisa wa mikopo hawatowi mikopo bila rushwa, unawekewa vikwazo hadi utangaze dau mwenyewe ndo unapewa nafasi ya kuanza mchakato, halafu rushwa yenyewe siku hizi wanachukuwa cash yaani kabla mkopo haujatoka unaambiwa toa hela kwanza,je tutafika?

hasa Nmb tawi la kariakoo
 
Vipi mbona tumesikia Benki yenu ipo hatarini kufilisika?tujuzeni haraka tuje tutoe mijihela yetu.
 
Ombi katika Tawi la Nmb Mwenge (Sinza) wahudumu wa Bank Tellers ni wachache na sehemu ya Bulk pia mara nyingi haina mtu mpaka uitiwe baada ya dakika 20-30 ukiwa unasubiri.

Na kwa hali ya sasa juu ya bank kivamiwa ni hatari sana kwa mtu kukaa na hela nyingi ukiwa unasubiri huduma.
 
kuhusu mikopo. unakuta muda wa makato umeisha lakini nyie mnaendelea kukata tu.rekebisheni hiyo
 
Huduma zenu mbovu mno mpaka mnakatisha tamaa,unakuta customer care mhudumu Ni mmoja tu wateja mia kasoro,inaboa sana,kwa nini msiajiri wafanyakazi!
 
Kiukweli nimekerwa na utoaji wenu wa mikopo kwa wajasiliamali,
Cz wajasilia malimali wa Vijijini hamja wathamini kabisa
 
hivi ni kweli ili upewe mkopo NMB lazima ufungue fixed account jamani mbona bamk nyingine hamna halafu aina maana maana badala ya kukopeshwa mpaka niweke hela kwanza mnapoteza maana ya mkopo.
 
hiv hii huduma ya mikopo itarudi lin hapa NMB NGUDU mbona mko kimya sana? afu yule afisa mikopo mweusi(mjaruo) du anaongoza kwa RUSHWA ASEE
 
Mkuu NMB Tanzania,
Kuna app mliyotengeneza kwa ajili ya watumiaji wa android? Naona crdb, exim na wengine wanayo ila yetu sijaona.
 
Last edited by a moderator:
tatizo Ni Kubwa kimtandao NA kihuduma
mteja anapoangalia salio kwa NMB mobile mnakata fedha sana has a mteja akiwa alijisaji kwa cheap ya Voda.

badilukeni kuangalia salio kwa mteja cheap zote I we free nje NA hapo nahamishia fedha zangu mkombozi bank.

Dirisha LA mikopo rudusheni NA punguzeni Kiwango cha makato mana mnazidiwa ata bayport
 
Kitu kinachoniudhi katika mabenk, ni upungufu wa tellers kwenye madirisha ya kuchukulia au kuweka pesa. Utakuta watu wamefurika benk, madirisha mawili tu kati ya sita au nane ndiyo yanayofanya kazi.

Tena ninyi NMB kila miisho ya mwezi inakuwa kama hamuoni. Wafanyakazi wa serikali kama walimu wakivamia benk inaajaa lakini mameneja hawasomi ile hali ili waongeze tellers madirishani, wao wanapitapita huku na kule bila kustuka.

Inatakiwa mtu ukiingia benki ukikaa sana ni dakika 15-30, lakini mtu anamaliza masaa 3 mpaka 5 yuko benki kuweka elfu 10! Kuweni wabunifu arrrrrrrrooooooh.
 
Kuweka pesa kupitia mitandao yani ya Simu ilikua bule lakini kwa sasa mnakata sana ,ukifili foleni ugailisha kwena benk ila msingekua mnakata wateja wangeweka karibu kila siku has a wenye pesa chache
 
Back
Top Bottom