NSSF kudhamini ndoa ya Billnas na Nandy: Kweli Rais Samia hili ndilo unalotaka kwa ajili ya watu wako? Siamini

NSSF kudhamini ndoa ya Billnas na Nandy: Kweli Rais Samia hili ndilo unalotaka kwa ajili ya watu wako? Siamini

Kwenye sherehe hawawezi kuweka tangazo mkuu, lakini ipo hivi wameanza kwa kwenda kununua nyumba ili wakaishi huko hawa wanandoa na waandishi wa habari wakawepo na ikatangazwa kwenye taarifa ya habari ya usiku katika vyombo vyote vya habari, hili ni TANGAZO moja wapo.
Baadae kwenye kila harakati zao za maandalizi ya harusi zilizokuwa zinarushwa kwenye mitandao ya kijamii ya baadhi ya vyombo vya habari na kwenye account za watu maarufu kulikuwa na hashtag ya #NSSF, mkuu mpaka hapa kuna haja ya ku justify kwamba haya ni MTANGAZo!!!!!???

Yaani Nandy na billnass watoe hela zao mfukoni na kununua nyumba ya NSSF na hapo hapo wakubali NSSF wajitangaze kwenye harusi yao bure bure tu.

Nandy na billnass ni brand ile harusi wameifanya biashara. Nssf pale amemwaga mahela ama ametoa nyumba bure ndipo akakubaliwa ajitangaze kwa kutumia harusi. Yaani clouds wampost nssf bure bure tu. Hadi bwana harusi anawataja nssf kama wadhamini ukumbini ni sababu ya mkataba wa uzamini

Humu jamiiforums msifikiri tumejaa mazuzu tu
 
Kuna Mdau hapa ameongea vizuri sana kwamba usianze kuhoji kabla haujafahamu hata kwa nini NSSF, any ways wengi mmeandika mambo meengi sana na mimi ngoja nichomekee yangu kidogo, navyofahamu kwa logic ndogo tu, Hawa NSSF Hawakudhamini Harusi ya Billnass na Nandy, lakini wao walichukua Fursa ya airtime kutoka Clouds Media Ambao walikuwa na issue yao ya Mkeka Mpya na nikingalia hata kwenye Mention zote hata nyie mkienda tazama mtakuta wameandika Mkeka Mpya wa Billnass na Nandy umepewa nguvu na hao wote waliotajwa hapo, hivyo kwa akili nyepesi NSSF wamechukua fursa hiyo kutoka Clouds Media group ili nao wapate kufanya promotion kama nyumba na kuendelea kuwakumbusha watanzania kuwa kuna fursa ya kujiwekea akibia wao wenyewe kupitia uchangiaji wa hiari, na haya siyasemi mimi bali nimeyasikiliza mimi mwenyewe na mpaka jana Mtu wa Clouds Mussa yule alisema pia kukumbusha kuhusu watu kujiwekea akiba, Hivyo basi ni vema tukaelewa kuwa hawa NSSF hawakudhamini Harusi lakini walitumia airtime ya Clouds na ubunifu wa Mkeka mpya ili wapate kuzungumzia masuala yao. Wazee muwe mnafuatilia mambo vizuri naweka nukta kam hivi.
 
Hamuwezi amini jamani Harusi ya NANDY NA BILLNAS, MAIN SPONSOR NI NSSF.

Kweli jamani kweli hivi leo hii tumefikia NSSF kudhamini harusi ya mtu binafsi... Kwa angle ya MARKETING... that wedding what is it going to do with the fund? Yaani fund inapata nini au ina vutia nini katika moja ya packages zake za MFUKO.?

Au hawa VIJANA wazazi ni vigogo kwenye mfuko?

THIS IS IRRITATING...

View attachment 2292838
Hebu sikiliza Hapa ndio utaelewa vizuri pia Babu

 
Hii nand na nass wameamua kufanya biashara na wataingiza pesa nyingi kutokana na hili hawa ni celebrity so wana impact kubwa Sana Kwa jamii. Ndugu mwwnachama tafadhal Kuwa mpole
Hawa jamaa wa NSSF mi naweza sema niwajanja sana aisee, mnakumbuka katika issue ya Malkia wa Nguvu pia, walitumia mbinu kama hii kuwafikia kundi ambalo pia linatakiwa kuwa na Hifadhi ya Jami, yaani sekta isiyo rasmi hivyo kama utaratibu wa kawaida nao walichukua package ya Airtime na kuwafikia watu kibao yani, Na leo hii katika Mkeka mpya wa clouds Media ndio maana utaona wamechukua airtime tena, kwanza ukiangalia Hata ile Harusi ilikuwa na kamati yake Mc wake kila kutu chake, sema ubunifu wa Mkeka mpya na segment yao katika Radio TV na Mitandao ya kijamamii ndio NSSF Nayo nahis wakajichokeka hapo hapo kutembelea nyota hiyo, ila kwa ujumla mimi sijaona walipodhamini Harusi ila walichukua fursa ya Mkeka mpya ya clouds kusemea mambo yao mbalimbali, jamani hapa mjini ujanja kuwahi, ndio maana mmeona na makampuni mengine nao wamejitokeza.
 
Ndoa ni kitu kizuri na katika kila dini hili tendo linakubalika...kama NSSF wamesponsor au wametia nguvu basi mimi kama mmoja wa mwanachama wa NSSF naliafiki 100%

Hongera Billnas
Hongera Nandy

Maneno vitu simple i got love from my people- Chafu pozi
Yote haya unaandika huku umening'iniza kaynday sofani sebuleni kwa shemeji yako?!
 
😂😂😂 inachekesha na kufurahisha kwa kweliii !!! Kwa hiyoo hapo kwa tafasiri nyingine ni wanachama wametoa mchango wa harusi sio ? 😂😂😂
 
Kama ni kweli, basi tunarudi kusema kwamba Serikali inapambana kukusanya pesa lakini haijui hizo pesa zitumike wapi. Ndio maana watumishi wa taasisi nyingi za serikali wanajilipa pesa nyingi kuliko kazi wanazozifanya. Rais akistaaf anaendelea kulipwa vilevile pamoja na kujengewa Jumba la heshima. Na bado ataendelea kupata stahiki zake zote hata kama alijirisha na nafasi aliyo kua nayo.

Jana tumeona ule mV8 kama zawadi kwa kamanda. Lakini si yeye mwenye wajibu wa kulijaza mafuta.
Malipo kwa wafanyakazi ni makubwa ndio maana serikali inashindwa kumuinua kundi la walala hoi ambao ni wengi.

Hakuna jipya. Tusubiri Mungu mwenyewe atakavyo amua hatima ya nchi yetu na africa kwa ujumla, lakini kwa sasa wananchi wanahangaika kulisha matumbo ya watu waliopo madarakani
Mkuu Umeandika kwa uchungu sana, Hawa viongozi mbweha wanataka yawapate ya Sri Lanka ndio watatia akili
 
Nssf wakati wa Dau iliyumba hadi wakaenda crdb kukopa ili walipe mishahara, ni wakati ambao nssf ilipigwa kupita maelezo.

Dau ni mmoja ya watu wa hovyo kupita mfano hata phd yake ni fake
Unaongelea kipindi Cha Mwendazake mkuu.
 
Back
Top Bottom