NSSF kudhamini ndoa ya Billnas na Nandy: Kweli Rais Samia hili ndilo unalotaka kwa ajili ya watu wako? Siamini

NSSF kudhamini ndoa ya Billnas na Nandy: Kweli Rais Samia hili ndilo unalotaka kwa ajili ya watu wako? Siamini

Hamuwezi amini jamani Harusi ya NANDY NA BILLNAS, MAIN SPONSOR NI NSSF.

Kweli jamani kweli hivi leo hii tumefikia NSSF kudhamini harusi ya mtu binafsi... Kwa angle ya MARKETING... that wedding what is it going to do with the fund? Yaani fund inapata nini au ina vutia nini katika moja ya packages zake za MFUKO.?

Au hawa VIJANA wazazi ni vigogo kwenye mfuko?

THIS IS IRRITATING...

View attachment 2292838
Maharusi ni ma promota wa uuzaji wa nyumba za nssf huko kigamboni wakisaidiana na steve nyerere
 
Ukweli hilo shirika toka aondoke Dr. Dau halijawahi kuwa na ufanisi.
Nssf wakati wa Dau iliyumba hadi wakaenda crdb kukopa ili walipe mishahara, ni wakati ambao nssf ilipigwa kupita maelezo.

Dau ni mmoja ya watu wa hovyo kupita mfano hata phd yake ni fake
 
Nyumba zipi hizo,zile za ubora wa chini wametumia pesa ndg,material hafifu vijumba vidogo,wanataka uza mamilion Mia na kadhaa
Hujiulizi kwanini haziuziki na watu hawana mzuka nazo

Ova
Sasa tangu huko juu unasema OVA.
mbona unaendelea.

Anyway wewe yaelekea ni kilaza,
Sasa ubora wa nyumba una utafanya zisitangazwe?
 
Kwako mkuu Kijakazi, EVIGT amelisema kwa lugha nyepesi sana. Ni biashara baina ya wafanya biashara na kupanga ni kuchagua. Kama unaumia kwa NSSF kuchagua Bill Nass sasa huwo wako ni wivu na wivu ni maradhi makubwa ambayo dawa yake haijagunduliwa bado.
Mkuu NUMBER 10 dawa ya wivu(ambao Mara nyingi hupelekea husuda) ishapatikana kitambo sanaa mkuu wangu ni kujaribu tu kumsifia kumpenda na kuungana nae huyo unaemuonea wivu na ikiwezekana kumuombea dua njema haswa! Kwa hiyo mshauri huyo mkuu namna ya kutibu huo ugonjwa wake
 
Inaelekea hujui hata kazi za NSSF
Kwa taarifa yako huo ni Mfuko wa pension na hupo kisheria ambapo ni lazima Kwa kila mwajiri wa sekta binafsi apeleke michango kila mwezi.
Asipopeleka anashtakiwa
Mfuko huo upo pekeyake na wala hauna mshindani
Hakuna suala la wateja ni lazima kuchangia.
Kama NSSF wametoa fedha kudhamini hiyo sherehe ni ufisadi
Inaonesha we hujui chochote hebu tulia. We unafikiri hao wanapeleka tu michango bila kuelimishwa.. usichojua ni kuwa hadi TRA huwa wanadhamini matukio mbalimbali ili waweze kupata nafasi ya kutoa elimu kwa mlipa kodi
 
Awareness pia inaleta wanachama, kuna watu wana ajira lakini hawapo nssf na visingizio lukuki , hapa ndipo umuhimu wa kujitangaza na kuonyesha faida za nssf ulipo
Naelewa pointi yako ya awareness. Kwa mantiki io... ni bora kutangaza kwenye harusi au kwenye event zinazohusiana na kazi mfano matamasha ya wajasiriamali, mikutano ya makampuni n.k
 
Wateja 2000?? Sasa hivi kifuko ipo miwili tu PSSSF na NSSF .PSSSF kwa waajiriwa wa serikali na NSSF kwa kampuni binafsi.wala haihitaji promo yoyote anayeajiriwa private sector mfuko wake ni NSSF
We unafikiri wanapeleka tu bila kuelimishwa, unatambua kuwa kuna sector binafsi hawapeleki michango huko au wanapeleka michango ya baadhi ya watumishi?
 
Shame Mgmt of NSSF
Shame board of Directors
Shame Ministry responsible for Social walfare
Kulipa watoa jasho fedha zao ni kwa shida tupu, halafu mnafanya huu upuuzi?
 
Inaonesha we hujui chochote hebu tulia. We unafikiri hao wanapeleka tu michango bila kuelimishwa.. usichojua ni kuwa hadi TRA huwa wanadhamini matukio mbalimbali ili waweze kupata nafasi ya kutoa elimu kwa mlipa kodi
Embu acha kutetea upumbavu we we nitajie harusi ambayo ishawahi kudhaminiwa na TRA
 
Embu acha kutetea upumbavu we we nitajie harusi ambayo ishawahi kudhaminiwa na TRA
Akikujibu uni tag
Mijitu kama hiyo
Ndy inaendekeza maujingaujinga

Kwa hiyo TRA wadhamini harusi ya fulani ili kuwahamisha watu walipe kodi hehehe

Kwa hapo nssf pesa za wanachama wamezi fuja tu

Ova
 
NSSF walichangia nini kwenye hiyo Harusi? ukisema kudhamini hicho ni kitu kingine kabsaa, na kama ni udhamini basi wanufaika ni cloud media wala sio wanaHarusi, kwani wewe ukipeleka tangazo lako kwenye media yoyote wakati simba na yanga wanacheza mpira na wao wakalirusha kama ulivyotaka, je iweje baada ya hapo uanze kulaumu wachezaji au yule mwenye tangazo???
 
Hamuwezi amini jamani Harusi ya NANDY NA BILLNAS, MAIN SPONSOR NI NSSF.

Kweli jamani kweli hivi leo hii tumefikia NSSF kudhamini harusi ya mtu binafsi... Kwa angle ya MARKETING... that wedding what is it going to do with the fund? Yaani fund inapata nini au ina vutia nini katika moja ya packages zake za MFUKO.?

Au hawa VIJANA wazazi ni vigogo kwenye mfuko?

THIS IS IRRITATING...

View attachment 2292838
Ndugu yangu AbuuMaryam, hii ni nasaha kwa Mtawala au?
 
We unafikiri wanapeleka tu bila kuelimishwa, unatambua kuwa kuna sector binafsi hawapeleki michango huko au wanapeleka michango ya baadhi ya watumishi?
Kutopeleka michango Wala haihitaji kuelemishwa Bali ni kosa kisheria. Kila mwajiri ni lazima apeleke michango ya wafanyakazi
 
Kama ni kweli, basi tunarudi kusema kwamba Serikali inapambana kukusanya pesa lakini haijui hizo pesa zitumike wapi. Ndio maana watumishi wa taasisi nyingi za serikali wanajilipa pesa nyingi kuliko kazi wanazozifanya. Rais akistaaf anaendelea kulipwa vilevile pamoja na kujengewa Jumba la heshima. Na bado ataendelea kupata stahiki zake zote hata kama alijirisha na nafasi aliyo kua nayo.
Jana tumeona ule mV8 kama zawadi kwa kamanda. Lakini si yeye mwenye wajibu wa kulijaza mafuta.
Malipo kwa wafanyakazi ni makubwa ndio maana serikali inashindwa kumuinua kundi la walala hoi ambao ni wengi.
Hakuna jipya. Tusubiri Mungu mwenyewe atakavyo amua hatima ya nchi yetu na africa kwa ujumla, lakini kwa sasa wananchi wanahangaika kulisha matumbo ya watu waliopo madarakani
Mkuu kumpa fadhila cdf mstaafu sio jambo baya sana..
 
@FRANCIS DA DON umesikia hii

Ova
Kwamba kabla ya hii ndoa hapakuwa na hitaji la kubrand NSSF, ila baada ya hawa kutangaza kuoana ghalfla bin vuu, NSSF wakapata uhitaji wa kujibrand, how ridiculous an arguement that would be!
 
Back
Top Bottom