Wadau wa JF ,
Mbona swala hili ni jepesi sana halafu linapewa uzito hivi ,kadri mnavyolijadili ndivyo hawa watu wanaonekana wamefanya marketing strategic sahihi zaidi hili hamlijui tuuu.
Hapa NSSF hawapo kutangaza watu kujiunga na shirika, wanachotangaza ni mradi wa nyumba uliopo kigamboni, kujiunga NSSF utajiunga tu as longer as umepata ajira sekta binafsi hili halina mjadara, Wao kwa sasa wameweka tension kwenye huo mradi wa nyumba, sasa wakatumia nafasi ya ndoa ya hao wasanii kufanya promotion ya nyumba zao, tatizo lipo wapi?, kumbukeni hawa wasanii wamejiajili na deal kama hizi ndio moja ya faida ya kujiajili,, NSSF wanafanya biashara na wasanii nao wanafanya biashaara, sasa wafanya biashara wakikubaliana kufanya jambo lao,ujue kila mmoja kaona faida ipo ndani yake, mfanyakazi endelea kufanyakazi kwa kuwa ni wewe binafsi umeona faida ya kazi yako na wao watapata faida ya biashara zao.
Kupanga ni kuchagua..................