Nukuu toka kwa Rais Magufuli (QUOTES)
“... Baada ya tetemeko wako watu walisingizia kwamba chakula hakuna.... Kwani tetemeko linakula chakula!?!?
Ina maana migomba yote ilikua ndani ya nyumba!?!?.....”
 
"Kuna chuki inayopandikizwa nchini kwa misingi ya tofauti za vyama. Nchi tuliyokabidhiwa na wazee wetu haikujengwa kwenye misingi ya namna hiyo"

Edward Lowassa
Bukoba Mjini, Kagera
15 Januari 2017

"Rais amesema hatoi chakula, mimi nimejadiliana na chama changu tumeona tufanye mpango wa kuwatafutia watanzania chakula. Hata kama ni cha kuomba nje ya nchi ninaamini dunia itatusikia"

Edward Lowassa
Bukoba Mjini, Kagera
15 Januari 2017

"Baada ya uchaguzi wenzetu walitarajia tutafanya fujo kudai ushindi wetu. Walijiandaa kutupiga na kuumiza watu wetu na hata ikiwezekana kukifuta kabisa chama chetu lakini tuliwashinda. Na ushindi haukuwa kwenye kura tu bali hata kwa kuzuia vijana na watu wetu kuingia mitaani."

Edward Lowassa
Kemondo, Kagera
15 Januari 2017

"Rais wa Marekani aliyechaguliwa ni mtu ambae haeleweki lakini sala yangu ni kwamba aje Afrika kukamata viongozi wote wanaovunja haki za raia."

Edward Lowassa
Bukoba Mjini, Kagera
15 Januari 2017

"Mashirika makubwa ya dini yamethibitisha ya kuwa kuna uhaba mkubwa wa chakula lakini serikali bado inaendelea kukana tatizo hilo. Narudia, namuomba rais atafakari kwa upya kauli zake kuhusiana na swala hili."

Edward Lowassa
Kemondo, Kagera
15 Januari 2017
 
Kweli siasa ni kama kamali. Ukishindwa leo unajipanga upya kucheza kesho kwa matumaini kwamba utashinda. Na mr Lowasa nae ndiyo mategemeo yake kuwa ipo siku atashinda uraisi.

Ajipe moyo. Lakini kwa hiyo kauli ya kwamba alishinda akapokonywa ushindi hapo anakosea sana. Kwani anapaswa kujua kwamba hata yeye anaweza kushindwa na siyo kwamba ni lazima yeye ashinde.
 
Akiwa Zanzibar alitaja hadharani kura alizopata..mbona hukukanusha? Acha kujitoa ufahamu wewe....
 
Kweli siasa ni kama kamali. Ukishindwa leo unajipanga upya kucheza kesho kwa matumaini kwamba utashinda. Na mr Lowasa nae ndiyo mategemeo yake kuwa ipo siku atashinda uraisi.

Ajipe moyo. Lakini kwa hiyo kauli ya kwamba alishinda akapokonywa ushindi hapo anakosea sana. Kwani anapaswa kujua kwamba hata yeye anaweza kushindwa na siyo kwamba ni lazima yeye ashinde.
siasa ni kama kamari hasa adui yako akiwa mropokaji, unajificha sehemu unambip tu unasubiri aropoke na wewe unaenda kuitumia ile kauli kumsambaratisha na kumuachanisha na wananchi. kama askofu wa mwanza ambayo wanamuabudu mtu fulani hivi, amesema kanisani kuw akiongozi anayesema hakuna njaa anatakiwa kuombewa, na ni askofu wa katoliki, nini kimebaki hapo sasa?
 
Huu mwenendo wa viongozi wa kisiasa na serikali kwenda kutoa matamko kanisani ni hatari sana. Baadae italeta sura ya udhehebu na matatizo mengine. Kanisani ifanyike ibada si sehemu ya kulipuliana mabomu ....Kanisa la Tanzania wawe makini na siasa makanisani.
 
siasa ni kama kamari hasa adui yako akiwa mropokaji, unajificha sehemu unambip tu unasubiri aropoke na wewe unaenda kuitumia ile kauli kumsambaratisha na kumuachanisha na wananchi. kama askofu wa mwanza ambayo wanamuabudu mtu fulani hivi, amesema kanisani kuw akiongozi anayesema hakuna njaa anatakiwa kuombewa, na ni askofu wa katoliki, nini kimebaki hapo sasa?
 
Pamoja na kauli za Rais Magufuli lakini hakuna kiongozi anaweza kulinganishwa na Rais Magufuli kwa dhamira yake ya vita dhidi rushwa.
Mzee Lowassa apumzike Tanzania inataka kiongozi aina ya Rais Magufuli.
 
Pamoja na kauli za Rais Magufuli lakini hakuna kiongozi anaweza kulinganishwa na Rais Magufuli kwa dhamira yake ya vita dhidi rushwa.
Mzee Lowassa apumzike Tanzania inataka kiongozi aina ya Rais Magufuli. Mwacheni Mheshimiwa Rais Magufuli atusafishie nchi.
 
Back
Top Bottom