Nukuu toka kwa Rais Magufuli (QUOTES)

Wewe unaweza kumlaza mgeni chumbani unakolala na mumeo/mkeo. Elewa kuwa intelligence ya kila nchi ipo kazini anytime, anywhere. Mfano, wakiijua ramani ya jengo la ikulu lote ni hatari hasa kama baadae watapanga mission za kumuua kiongozi wa nchi au genge husika. Ili Osama auwawe na Marekani, walichukua data za kijasusi za eneo na jengo alilokuwa akiishi Osama hadi chumba alichokuwa analala na ratiba zake zote, then attack ikawa planned accordingly na wakamuua kweli.

Ingawa wajerumani na waingereza wana ramani ya ikulu yetu (coz lilikuwa ofisi kuu ya governor Tanganyika kipindi cha ukoloni.), but baada ya Mwl Nyerere kuchukua nchi, mpaka leo hii kuna marekebisho mbalimbali yamekwishafanyika, mengine yakiwa yanalenga zaidi usiri wa kiusalama.
 
Juzi akiwa dodoma aliwambia wanawake?

Mnahitaji nipanue kwa ukubwa gani?

Basi wana dodoma walivyo na ubongo wa majivu ni vicheko hadi balaaa..
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli

Hizi ni baadhi ya nukuu za Rais Magufuli baada ya kupokea ripoti madini:

-Kwa Mtanzania yeyote mwenye akili timamu anaposikia ripoti kama hii lazima apate uchungu

-Nafahamu wapo watu walitaka kuhatarisha maisha yenu, lakini walishindwa kwa sababu ya ulinzi imara

-Tanzania tuna karibu madini yote, unaweza ukayataja mpaka ukasahau.

-Watanzania tuna mali nyingi lakini tunazichezea mpaka shetani anatucheka huko aliko

-Tanzania siyo siri wapo watu wanakufa kwa kukosa madawa, wapo wakulima wanakosa hata pembejeo wakati mali tunazo.

-Inashangaza sana kampuni ya madini inafanyakazi nchini kunyume na sheria tena biashara ya matrilioni ya fedha.

-Ukiwa na mchungaji wako anasema ng’ombe wanatoa lita 1 tu kwa siku ukienda kuhakikisha kama ni ukweli, ni vibaya?

-Sisi viongozi tujiulize ni mara ngapi tunawadhalilisha wafanyabiashara wadogo wa Kitanzania wakiwa hawajasajiliwa?

-Nani atakayepewa ripoti kama hii akacelebrate? Wakati watoto wa maskini wanakufa.

-Siwezi kusimama pale mbele halafu naona haya yanafanyika nikae kimya, siwezi, nitaulizwa siku moja na Mungu wangu.

-Kuna mpiga kelele mmoja, tuli trac simu yake tukaona anatuma meseji anasema naomba data hii, naomba data hii.

-Hizi fedha zikienda hospitalini hawatatibiwa CCM tu hata CHADEMA watatibiwa.

-Kwenye ripoti ya kwanza, Kafumu amehangaika kutafuta data ili afanye mabadiliko ni ujinga mtupu

-Dkt. Kafumu alienda kumbembeleza Prof. Mruma ili afanye forgery ya Ripoti ya Kamati ya Kwanza

-Mapendekezo yote yaliyotolewa na Kamati hii nayapokea na nimeyakubali kwa asilimia 100

-Kuna Dkt mwingine wa Muhimbili tulimkamata Dodoma anataka kuishawishi kamati ibadili ripoti, tukamrudisha akatibu.

-Ukiwa msoma sio unakuwa mzalendo, unaweza ukasoma ukawa hata Profesa lakini usiwe mzalendo

-Hii kampuni inayoitwa Acacia waitwe kwanza walipe pesa zetu,Wakikubali na kutubu ndipo wafanyiwe registration

-Wahusika wote waliotajwa kwenye ripoti hii vyombo vya dola viwahoji na kubaini ukweli juu ya jambo hili

-Kazi hii ni ngumu, ni ngumu kweli kweli, lakini kama Mungu amenipa kuifanya i will do it

-Sawa sisi viongozi hawaturuhusu kuingia migodini, hata viongozi wa dini basi waruhusiwe kwenda kuombea hayo madini

-Naomba Sheria ya gesi ipitiwe, hata tukichelewa ni sawa lakini tuwe na sheria nzuri

-Hii nchi tumelogwa na nani? Basi viongozi wa dini tuombeeni mapepo yatoke

-Mtu unakuta ni Mbunge na Jimbo lake ni masikini lakini anakuja kutetea huu ujinga

-Spika nikakuletea hii mizigo, kwa wale watakaokuwa wanaropoka unaenda vizuri, ili wakiropoka nje mimi ntadili nao

-Spika, kwa wale watakaokuwa wanaropoka ropoka, watoe nje. Na wakiropokea nje i will deal with them, Ila siwatishi

-Prof. Oroso umetimiza wajibu wako hapa duniani, Mungu atakubariki sana.
 
Napenda sana kusoma juu ya Rais wetu mpendwa.. ni Rais Jembe haswaaa.. amevunja historia nchini kwa kusikilizwa na wana CCM wengi, pamoja na Wapinzani.. tena hao kizaidi.. Chaguo la Mungu..

Hii alisema imesaidia sana wanchi kuacha uvivu na kujitambua na kufurahia maisha yao ya kuishi kama binadamu.. usipo fanya kazi na usile

💚💛💚💛💚💛 💯
Magufuli oyeeeee
 
Back
Top Bottom