Nyongeza ya mishahara TUCTA wamasema wamepokea malalamiko, watatoa tamko

 

Attachments

  • 1658517400940.png
    75.5 KB · Views: 9

Huo ndiyo ukweli wa mambo, labda umeajiriwa miaka ya karibuni ambapo hujui kanuni za nyongeza ya mishahara. Wapo waliopewa hiyo asilimia 23.3 Tatizo vijana wengi watumishi waliposikia nyongeza itakuwa 23.3% walidhani ni kila mfanyakazi atapokea hiyo nyongeza!

Dah! Mbona Serikali ingesimamisha huduma zingine zote na TRA wangekuwa wanakusanya mapato kulipa mishahara tu! Aftersll kabla hamjashituka kwa hiyo mishaha kwani waraka wa hiyo mishahara hamkuletewa kabla?
 
Sielewi mjue yaani adi Azana ilipigwa akanyamaza kiimani alafu amesema uwongo mbona simuelewi

Wewe ndiyo hujaelewa! Hiyo asilia 23.3 ilikuwa ni kwaajili ya kima cha chini! Kama unakula kima cha chini na hujaongezewa hiyo asilimia, chapu chapu mpigie Mwigulu Lameck Madera Nchemba!
 
Usidhani umejifocha humu kwa kutoa kashfa kwa Mamlaka,sheria ya makosa ya mitandaoni haijafutwa..

Kwa hiyo wewe kibwengo ndio unajua saana Mwigulu kuliko Rais si ndio?

Acha kuropoka mambo usiyoyajua utakuja kula hasara ya mazima.
Tulia wewe cheti FEKI, bi mkubwa akila spana uko jet kweli kuja ku defend 😂😂😂 Chawansic investigator
 
Unakwama wapi? Katiba itaweka mifumo ya checks and balances ambazo sasa hivi inafanywa na UVCCM. Wamekuingizia mawazo yao mgando kuwa kama hii Katiba mbovu haisimamiwi vema tusiandike Katiba Mpya ya Wananchi kwa sababu hiyo?Kweli hapo upo serious Ndugu?
 
Usidhani umejifocha humu kwa kutoa kashfa kwa Mamlaka,sheria ya makosa ya mitandaoni haijafutwa..

Kwa hiyo wewe kibwengo ndio unajua saana Mwigulu kuliko Rais si ndio?

Acha kuropoka mambo usiyoyajua utakuja kula hasara ya mazima.
Mmh
 
Heri kusema ukweli kuliko kuendekeza siasa...ni vigumu sana ukiwa na miradi mikubwa miwili ya Umeme na reli ujaea na uwezo wa kuongeza mishahara wafanyakazi wanavyotaka.nina uhakika hii miradi ikikamilika serikali itakuws ba uwezo wa kulip kiasi chochote pendekezwa
 
Sie wengine hatujui hesabu kwa wanao jua toeni maelekezo, 150,000 kwa 23% ongezeko lake linakuwa kiasi gani?.

Sent using Jamii Forums mobile app
150,000 X 23.3 ni 3495000 kisha gawa kwa %100
wapata hiyo 34950

Serikali ya Tanzania ikikusanya kodi ipasavyo na kudhibiti vyanzo vingi vya mapato ina uwezo wa kumpa mfanyakazi wa kima cha chini 900,000 kwa mwezi.

Lakini wafanyakazi haohao wenye kipato cha mshahara wa kima cha chini wataka waibe mapato ya serikali kisha wadai ongezeko la mishahara.

Hivyo, kupandishwa mishahara ni kutokana na serikali kujaa mapato yake.
 
Binafsi natoa Pongezi kwa Watumishi wa Serikali kuongezewa Mishahara baada ya Miaka takriban Sita bila nyongeza yoyote ile.

Pambaneni sasa Wafanyakazi kwa kuchapa kazi kwa bidii sana.
Naona sasa Mnalamba Asali.

Tulieni sasa mchape kazi.
 
Heri JPM hakuwa mwongo. Alisema wazi kwamba kwa wakati ule hataongeza mishahara ila kuna siku ataongeza pesa nyingi zaidi.
Hakika leo nimemkumbuka JPM, bora kuambiwa ukweli kuliko hadaa. Kila kitu kimepanda bei kwa kauli za hadaa ... haya ngoja tuendelee kulamba asali
 
Huu ndio ukweli mchungu, maana hata hii iliyopo mtu anaikanyaga na vyombo vya kuilinda vinafumba macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…