Nyundo na wenzake wakutwa na hatia, wahukumiwa kifungo cha Maisha Jela
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, imewahukumu kifungo cha maisha gerezani washtakiwa wanne maarufu ‘waliotumwa na afande’, baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti, mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam.

Ni katika kesi ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024 iliyokuwa inawakabili washtakiwa hao akiwamo MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu, Septemba 30, 2024. Pia, Mahakama hiyo imewataka kila mmoja kumlipa binti huyo fidia ya Sh1 milioni.

Pia soma
Mbona ile kesi ya mkuu wa mkoa aliyelawiti mwanafunzi hazisikiki tena?
 
Iwe fundisho kwa wengine,

Starehe ya madakika tu inafanya maisha yako yote yaliyobaki yaishie Jela,

Hata siku moja usikubali kutumwa kwenda kufanya jinai ili kumfurahisha mwingine au kwa malipo,

Ur life belong to you and life is too short,

Sasa hivi wanajuta ila ndio imeshakua too late.

WORD. Throwing life away for literally nothing.
 
Kesi imesikilizwa kwa haraka mno maana yake walishahukumiwa kabla haijasikilizwa, na wahanga wa ubakaji wengine nao kesi zao hazisikilizwi haraka hivyo sababu hawakurekodiwa video na kurushwa ktk social medias!!
Imefanywa hivyo ili kupoza joto la kisiasa,hao watatoka kwenye rufaa kesi Ina matobo mengi sana.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, imewahukumu kifungo cha maisha gerezani washtakiwa wanne maarufu ‘waliotumwa na afande’, baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti, mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam.

Ni katika kesi ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024 iliyokuwa inawakabili washtakiwa hao akiwamo MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu, Septemba 30, 2024. Pia, Mahakama hiyo imewataka kila mmoja kumlipa binti huyo fidia ya Sh1 milioni.

Pia soma
Kinachosikitisha Hawa jamaa hawakutumia Mafuta.
 
Wakikata rufaa hawa jamaa wanachomoka. Ila watawapiga High Court ili wakae ndani kwa muda hadi wafike CAT ni miaka minne hadi sita alafu watakutwa mashtaka hayakuthibitishwa bila kuacha shaka mwishowe watatoka.

Wajipange vzuri tu.
Inawezekana eti...na ukiwaza sana kwa jinsi mihemho ya jamii..hata kama kulikuwa na namna ya kuchomoka jamii isingewapokea..wakikaa miaka 3 na wanaweza shinda rufaa na jamii ikawa imesahau sahau
 
Sasa mpumzisheni Mama Samia mwenye kusimamia haki. Walikuwa wanamchafua kuwa serikali yake haitendei haki watu. Viva samia. Mitano tena. Mihimili yote iko fair fair fair fair
Bado afande aliyewatuma kina nyundo hao ni dagaa bado papa mwenyewe huyo naye akipata haki yake hapo sasa tutasema itakuwa fair
 
Wakikata rufaa hawa jamaa wanachomoka. Ila watawapiga High Court ili wakae ndani kwa muda hadi wafike CAT ni miaka minne hadi sita alafu watakutwa mashtaka hayakuthibitishwa bila kuacha shaka mwishowe watatoka.

Wajipange vzuri tu.
Unamaana gani kwamba hayaja dhibitishwa,yan pamoja na ushahidi wa video bado kuna shaka kama walifanya? Au ndio mambo ya wimbo wa shaggy it was'nt me ingawa dem wake kamfumania kwenye kamera

Kama sheria ndio ziko hivi,basi ni upuuzi
 
My Take
Kwa Hukumu hii Haki imetendeka.

Aliyewatuma yeye mbona kuko kimya? 👇👇
---
Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, imewahukumu kifungo cha maisha gerezani washtakiwa wanne maarufu ‘waliotumwa na afande’, baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti, mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam.

Ni katika kesi ya jinai namba 23476 ya mwaka 2024 iliyokuwa inawakabili washtakiwa hao akiwamo MT 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo ambaye ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu, Septemba 30, 2024. Pia, Mahakama hiyo imewataka kila mmoja kumlipa binti huyo fidia ya Sh1 milioni.
 
Unamaana gani kwamba hayaja dhibitishwa,yan pamoja na ushahidi wa video bado kuna shaka kama walifanya? Au ndio mambo ya wimbo wa shaggy it was'nt me ingawa dem wake kamfumania kwenye kamera

Kama sheria ndio ziko hivi,basi ni upuuzi
kwani wewe ejuaje ni wao kwenye video? Hujawahi kuona video za kuedit? Na hapo ndipo gap lilipo kwenye hii kesi. Kwa aina ya makosa kuna kosa limekosekana ambalo lilitakiwa liwepo ila sasa lazima kifaa kilichorekodi na kutuma lazima nacho kiwepo. Huo ndio mtihani uliokuwepo na hautaishi miaka mingi sana wataenda kutokea Mahakama ya Juu ya Rufaa
 
Back
Top Bottom