Acheni kujidanganya nyie hakuna cha hofu ya Mungu wala nini binadamu akiamua kugeuka atageuka tu!, si Mungu si shetani atamsimamia binadamu ni utashi wake binafsi leo anaweza kusema ndio kesho anaweza kusema sio!.
Kama unaoana na mtu kisa anahofu ya kitu fulani basi jua bado unasafari ndefu!, maana hofu ya hicho kitu ikiondoka utasaga meno!.
Kwa kiumbe kinachoitwa binadamu hakuna kitu permanent siri ya vitu anavyovitaka yeye maishani ni siri yake tu!.
Ishini mguu ndani mguu nje, mkifanikisha malengo yeni hiyo ni heri kwenu.
Ukweli ambao hamtaki kuusikia ni huu "Binadamu hababaishwi na kitu kinachoitwa hofu ya Mungu, akiamua ku kengeuka atakengeuka tu".