CHADEMA ni wahuni, ushahidi ni wale waliojitoa CHADEMA kueleza wazi na kwa kina.
Lakini kinachotia kinyaa ni kukubali kutumika na mabeberu. Wameona kwa uchaguzi wa kawaida hakuna namna watapata hata wabunge 5, mbinu mbadala ni kutumika kuleta vurugu kisha mbinyo wa kiuchumi ili mataifa ya magharibi yalazimishe angalau serikali ya umoja Kama si ku engineer vurugu za kuitoa serikali halali itakayoundwa na Mh Rais atakayeshinda.
Ukitaka kujua move yao angalia Tundu Lissu alivyokuja kwa vurugu, matusi na uchokozi wa wazi kabisa. Tunaelewa anatafuta nini. Na ukichunguza kuna ushirikiano wa kampaign zinazoendana na lengo hili na vyombo vya habari hasa vya kimataifa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO's). Wachunguzi wa mambo wanaelewa namna ambavyo vyombo vya kimagharibi Kama CIA zinavyo tumia "covert actions" kwa vyombo hivi ili "ku justify" malengo yao yaliyojificha ya kujaribu kuondoa utawala ambao hauungi mkono maslahi yao na kuweka vibaraka.
Uzuri serikali haiishii kuangalia uhuni wa karibu Kama kuchoma ofisi, bali kwenye move zao za mbali zilizojicha kama kampeni chafu ya habari za uongo za vyombo vya habari na taasisi zisizokuwa za serikali, ambazo ndiyo mara nyingi zinabeba agenda za moja kwa moja za mabeberu kupitia ufadhili wa "projects na programs" mbalimbali.
Hatua ya hivi karibuni ya serikali dhidi ya habari ya BBC na kituo cha haki za binadamu inapeleka salaam kwamba serikali inajua mbinu, malengo na mikakati yote wanayoifanya sasa hivi.
Viva Tanzania, viva JPM!