Uchaguzi 2020 Ombi: Tume ya Uchaguzi tunataka mdahalo wa Wagombea Urais

Kukiwa na mdahalo, JPM hatakuwa na mengi kwani aliyofanya yanajitosheleza. Waliobaki ni kujikang'aga tu.
 
Je??
Leo huyu mlamba viatu vya wajumbe wa Ccm atathubutu kurudia hii kauli??
Au atabaki kama Mr Slowslow???

Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
 
Rais Magufuli atapokuwa anaongelea kujenga SGR, Mwalimu Nyerere Hydroelectric Power, masoko ya madini, kuingia uchumi wa kati, Bombardiers, hazina kujaa mafedha, kushusha kodi kwenye mishahara, kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi, kuthibiti rushwa kwa kiasi kikubwa nchini, ujenzi wa viwanda, wakulima kupata being nzuri (mfano korosho Mtwara), kuhamia Dodoma (jambo lililoshindikana tangu za Mwl. Nyerere) na kadhalika na kadhalika akina Tundu Lissu wataongea nini? Hatuwezi kumdhalilisha Mgombea Wetu wa CCM kuingia kwenye mdahalo wa watu WADOGO!!!
 
Kuna watu wanafikiri mdahalo ni sawa na kuifokea ccm/serikali.
 
Midahalo ya wagombea Urais katika nchi yoyote ile yenye mawazo chanya ni muhimu sana , na baadhi ya wadau nikiwemo mimi tuliomba tangu awali ili yale mazuri ya 1995 yajirudie , tukumbuke kwamba 1995 wagombea wa urais wa Tanzania akiwemo Lyatonga Mrema na Benjamini Mkapa walikaa kwenye mdahalo huku kila mmoja akinadi mipango yake .

 
Naungania na Kitila Mkumbo kwamba Midahalo kwa wagombea Urais ianzishwe ili wagombea tuwapime kwa Hoja zao.
 
Ni ya mwaka 2015..

Leo hii ataikataa..

Marehemu Ruge Mutahaba alisema hapa duniani anaogopa MUNGU na TEKNOLOJIA tu...
 
Magufuli akimkimbia Lisu kwenye mdahalo huu atazidi kujichimbia kaburi la kukataliwa na wapiga kura.

Kwa makusudi kabisa Lisu ametegeshea Magufuli hili zigo la kushiriki mdahalo wa wazi ama kukataa.

Naliita zigo kwasabb Magufuli akikubali kushiriki ni MSALA kwake maana yuko poor Sana ktk kujenga hoja. Hivyo ataabika vibaya mno kwenye mdahalo huo.

Na akikataa pia ni MSALA. Maana itaonekana anamuogopa mtu mdogo kama Lisu. Mbali na umri hata kwenda shule Magufuli ana madarasa mengi kuliko Lisu (ana PhD) na ni rais.

Sasa watu watajiuliza iweje unamkimbia na kumuogopa mtu kama Lisu? Itampunguzia na kumshushia personality kwa wapiga kura.

My take:
Mwaka huu ccm mmelokoroga na mtalinywa. Hali yenu tete Sana.
 
Sina hakika kama anamuogopa ila nachojua hatokuwa na mda wa ziada wa kushiriki kitu ambacho hakiko kwenye ratiba yake
 

Sidhani kama kuna mwanasiasa wa Tanzania aliwahi kwenda kwenye kipindi cha Hardtalk zaidi ya Lissu. Kama ameweza kujibu maswali kwenye Hardtalk mdahalo wa Tanzania ni kazi rahisi sana kwake.
 
Hapa anapanga kuwa Lissu akatwe tu
 
Magu Hana muda na midahalo anawaonyesha kwa vitendo tu
Hao wagombea wengine ndio waende kwenye midahalo wakabembelez kura
Mtasema amemkimbia mpaka mtachoka mwisho was siku mtanyamaza mwenzenu anaendelea kuchapa kazi
 
CCM is a zombie land, and every person in it is literary brain-dead.
And unfortunately we all know you can't debate with a zombie.
 
Hehehe hi debate asije mtu akarusha ngumi bureee...

lakini TL aiitishe tu kwa kweli
Kila mtu awekwe kikaangoni...kutesa kwa zamu
A Sanity-Train has left these thugs a long time ago.
So it's okay to expect any decadence from them.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…