Uchaguzi 2020 Ombi: Tume ya Uchaguzi tunataka mdahalo wa Wagombea Urais

Kila chama kifanye kampeni kwa Style yao. Hata upinzani haina msimamo thabiti kuhusu nini wanataka
Usiseme wapinzani; sema ACT na CHADEMA hawana msimamo thabiti kuhusu nini wanataka.
 
Japo watu wanaweza rushiana ngumi ila this would be soooo nice.Kama nchi naamini we really need it.,

Pascal Mayalla tusaidie Mkuu kwani lazima iratibiwe na NEC?...kama kuna uwezekano wa independent body/person kuifanya itanoga mnooo

nakumbuka debates za US na UK zinavyokuwaga motoo
 
Mdaharo Uwe wa kingereza

Mataga njoo huku mpinge Mdaharo,

Nyie mataga si Mna stiglers, sgr, flyover, bombardier mnaogopa Nini?
 
Kuna mmoja hapo atakimbia walah nakwambia mkuu
 

Uoga wa nini? nenda masaa mawili tu ongea na Watanzania! mnasema Tanzania tunataka iwe kama Ulaya wakati viongozi waoga hata kuongea. Uraisi wa kifalme lakini kwenda mbele ya Watanzania kusema na kulinganisha hoja kwa hoja imekuwa woga. Wewe ndiyo ungetakiwa kumshauri aende kusema aliyofanya mengi!!!!
 
Kwanini kusiwepo na mdahalo wa saa 8 kwa wagombea wote wa kiti cha uraisi maana najua JPM anavitu vya kuongelea ndani ya miaka yake mitano kama Raisi, na wengine watasema wanataka kuchaguliwa ili iweje?.
Kwa mmoja wa wagombea Mdaharo utaishia kwenye self introduction, "PhD in ze mafuta of korosho"
 
Mdahalo MUHIMU,ndo tupime sera zao kuhusu sisi wananchi sio kuingiza watu bila kupima weledi.
 
Watu uwezo wanao sema shida ni kwamba wameminywa hawana uhuru wowote kwenye nchi yetu ukitaka jua hilo angalia mchakato wa Urais vyombo vya habari vinavyopendelea.
Nani ata u moderate huo mdahalo? Sijaona chombo chochote cha habari chenye huo uwezo
 
Wakuu naona sasa imeshakubalika mdaHalo lazma uwepo na ni full kimombo mwanzo mwisho, hamna mambo ya kuchanganya kimangati wala cjui kimasai, kisukuma
 
Wakuu naona sasa imeshakubalika mdaHalo lazma uwepo na ni full kimombo mwanzo mwisho, hamna mambo ya kuchanganya kimangati wala cjui kimasai, kisukuma
Kwanini kimombo? Wapiga kura hawakijui kimombo kwanini utumie lugha ambayo hata wewe mwenyewe labda huijui vizuri. Binafsi nimeishi nchi ya waingereza zaidi ya chaguzi 7 sijawasikia wakifanya mdahalo kwa kijerumani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…