Operesheni Unfollow Wasanii wote Mitandaoni ambao hawasimami na Wananchi kwenye Haki

Hii ndiyo dawa yao ,hatuwezi kusapoti serikali na machawa wao katika mauaji ,kutesa watu , kuumiza watu na ubakaji wa demokrasia ,...Hii itasaidia sana
 
Hii sasa ni balaa kwani kawakosea nini?
Wasanii wamepewa umaarufu na wananchi, ila hawataki kurudisha fadhila kwa wananchi kwa kusimama nao kwenye haki hususani kwenye Dunia hii ya utekaji na wananchi kuonewa... wasanii wamekuwa wakichagua upande wa watawala, wanasahau sisi ndio tumewafanya kuwa na mali na umaarufu walionao
 
Tatizo huwa mnarukia mambo. Faida Msanii anayoipata ccm na kwa wananchi ni tofauti. Mfano Diamond kama si JK 2010, angelikuwa domo bado. Msanii ni mtafutaji ujue.

Faida ya NRNE ipo kwa wale wanaotaka kuchukua nchi ili nao watoto wao wafaidi kama Ridhuwani au sasa Abdul. Sijaona katika Tanzania mtu anayepambana aende Ikulu awakomboe mimi na wewe. Hata hawa waliopo na NRNE ni wale wale.
 
Unfollow halafu comments ni NO REFORM NO ELECTION POPOTE HADI KIELEWEKE
 
Na yule yule, acha watu wafanye kile mioyo yao inawatuma
 
Kila njia itayoleta MABADILIKO ya Kidemokrasia,Haki na Maendeleo nchini itumike...

Napendekeza Walk to Work..wote tuwe tunashuka Magomeni,Salender, TAZARA, Bandari, Boma ,Kivukoni...tunapiga mguu to City Centre n Kariakoo huku tukisema NO REFORMS, NO ELECTION
 
Wabongo hii hatuwezi.. tunaogopa virungu vya maafande, but ndo njia nzuri ambayo ikitumika inaleta output mapema.

So wacha tupambane mitandaoni tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…