Nchi nyingine, watu maarufu na Mastaa usimama na Wannchi linapokuja swala au jambo la maslahi ya wananchi kwa ujumla. Huko South Africa, Nigeria hata hapo kwa majirani zetu Kenya wasanii wengi husimama na raia na mara zote wamekuwa mstari wa mbele kuwapigania au kuwazungumzia wananchi endapo maslahi ya wananchi yakienda ndivyo sivyo. Hii imekuwa hata kwenye mataifa makubwa kama Marekani, Ulaya na sehemu nyingi za Dunia.
Lakini kwenye hii ardhi ya Nyerere mambo uwa ni tofauti kabisa, wasanii wengi hawasimami na raia au wananchi bali wao usimama na serikali au wanasiasa linapokuja jambo linalohusu mustakabali wa taifa au maslahi ya wananchi. Ikumbukwe hawa wasanii wamekuwa maarufu kutokana na hawa wananchi ambao wamekuwa wakisalitiwa mara kwa mara.
Huko Twitter imeanzishwa Kampeni ya ku-unfollow watu wote maarufu ambao wako kimbelembele na mambo ya siasa za chama tawala au viongozi wa chama tawala, na kuwatelekeza raia ambao kimsingi wao ni waliowapatia umaarufu na si serikali. Panga hili la ku-unfollow mastaa na wasanii pia limemkuta Millard Ayo ambapo mpaka sasa kapoteza wafuasi zaidi ya 300k baada ya Kampeni hii kuanzishwa.
Kampeni hii imelenga mitandao ya Instagram, Facebook, Twitter mpaka YouTube.... unfollow msanii yoyote ambaye ni chawa na si mtu wa kutetea Raia. Wasanii Wamesahau kama followers wao ndio sisi raia ambao wamechagua kutusaliti.
Unfollow wasanii wote ikiwemo wachekeshaji na kila mtu ambaye kapata umaarufu lakini hataki kusimama na raia badala yake amechagua kuwa chawa wa siasa za chama tawala