Operesheni Unfollow Wasanii wote Mitandaoni ambao hawasimami na Wananchi kwenye Haki

Operesheni Unfollow Wasanii wote Mitandaoni ambao hawasimami na Wananchi kwenye Haki

Sasa hii inasaidia nini kuiondoa CCM madarakani? Watanganyika sijui mtashituka lini.
 
Wasanii wa bongo wote njaa wanafeki life ukitaka kujua ngoja wakiugua wanategemea huruma ya chama thus ni lazima wajiuze so huwezi linganisha na wasanii wa nchi hizo wao hawaishi kwa kujiuza.
Wa kike zaidi ya udangaji Wana kipato gani,hao wa kiume bila upididi kipi wanachoingiza kutwa lazima wawe machawa tu
 
Zamani wasanii walitumia ubunifu wao kuchochea
1. Uzalendo
2. Kuchapa kazi kwa bidii
3. Kufundisha stadi za kazi
4. Kupongeza wapambanaji, TMK, East Coast, Wagosi wa kaya, etc
5. Kuhamasisha watu kujikinga maradhi ya zinaa kama kaswende na ukimwa, gono.
6. Kilimo
7. Biashara, umachinga

Siku hizi sasa
1. Ngono inahamasishwa wazi wazi.
2. Wanahamasisha ngono za kinyume na maumbile.......utasikia zama mtaroni, choo-toilet, Ukipata danga lipe kwa mpalange, temea mate iteleze kama nyoka.
3. Wasanii wa leo ni vichocheo vya ulevi, madawa, pombe, viroba utasikia Ntaka kulewa, Wacha nilewe, nijipe raha na gambe,


Wasanii wa sasa wabadilikex wahimize Uzalendo kwa Nchi na wananchi, wahimize uchapa kazi na sio udangaji na uvivu wa kutaka maisha mazuri.

Tuwaunge mkono lakini wasidumaze akili za vijana ambao ndio nguvu kazi ya kesho.
Soko ndilo uamua wakihamasisha hayo mambo watamuuzia nani.
Soko litaka mambo ya uchawi, ngono,mpira,udaku.
 
Mnawaonea tu hao wasanii.

Unajua matokeo yatakayo tokea ikiwa leo hii Diamond atasimama against serikali? Kama wamefanya yale kwa Gwajima watafanya nini kwa Diamond, Kusaga na Majizo and the like?

Na je, Wananchi watasimama na Hao wasanii pindi serikali itakapo wageuka?

Watanzania wengi wanataka kupiganiwa haki zao, wao wakiwa safe behind keyboards wakati huo wewe unateseka kupambana na mamlaka.

Gwajima kaongea, kawasemea, kapaza sauti, Amezongwa na serikali, Watanzania wapo kimya nyuma ya keyboard wanalalama badalala ya Kukinukisha mpaka serikali iombe pooo. Ndo unataka wasanii wasimame na ninyi au matajiri kama akina Mooo? SIO KITU RAHISI
 
Tatizo huwa mnarukia mambo. Faida Msanii anayoipata ccm na kwa wananchi ni tofauti. Mfano Diamond kama si JK 2010, angelikuwa domo bado. Msanii ni mtafutaji ujue.

Faida ya NRNE ipo kwa wale wanaotaka kuchukua nchi ili nao watoto wao wafaidi kama Ridhuwani au sasa Abdul. Sijaona katika Tanzania mtu anayepambana aende Ikulu awakomboe mimi na wewe. Hata hawa waliopo na NRNE ni wale wale.
Ndio akili zenu zilipo ishia
 
Naunga mkono hili azimio la kizalendo, Tusihishie kwenye kujiondoa kwenye kurasa zao

-Twende mbele zaidi, kwa kipindi cha miaka mitano (5) ijayo.

-Tuache kuwa wateja wao, wa kununua kazi zao, kuudhuria matamasha yao, Kuacha kuangalia kazi zao.
-Tuache kununua bidhaa/huduma kutoka kwenye biashara zao.
-Kuacha kununua huduma/bidhaa ambazo wao ni mabalozi, na washirika wao wa kibiashara.

Mimi nimejiondoa kwenye kurasa zote za wasanii ,wanasiasa ,waandishi na wafanyabiashara wenye kuunga mkono udhalimu. Hata wewe unaweza
 
Wabongo hii hatuwezi.. tunaogopa virungu vya maafande, but ndo njia nzuri ambayo ikitumika inaleta output mapema.

So wacha tupambane mitandaoni tu
never say never we might get to that stage
ipo siku tutatembea barabarani nakuhakikishia hio siku itafika watanzania wasijipuuze wakati utafika
 
Hamna haja ya ku unfollow.....bali tumia hapo hapo katika platforms zao kuweka ujumbe wa no reforms no election.
 
Nchi nyingine, watu maarufu na Mastaa usimama na Wannchi linapokuja swala au jambo la maslahi ya wananchi kwa ujumla. Huko South Africa, Nigeria hata hapo kwa majirani zetu Kenya wasanii wengi husimama na raia na mara zote wamekuwa mstari wa mbele kuwapigania au kuwazungumzia wananchi endapo maslahi ya wananchi yakienda ndivyo sivyo. Hii imekuwa hata kwenye mataifa makubwa kama Marekani, Ulaya na sehemu nyingi za Dunia.

Lakini kwenye hii ardhi ya Nyerere mambo uwa ni tofauti kabisa, wasanii wengi hawasimami na raia au wananchi bali wao usimama na serikali au wanasiasa linapokuja jambo linalohusu mustakabali wa taifa au maslahi ya wananchi. Ikumbukwe hawa wasanii wamekuwa maarufu kutokana na hawa wananchi ambao wamekuwa wakisalitiwa mara kwa mara.

Huko Twitter imeanzishwa Kampeni ya ku-unfollow watu wote maarufu ambao wako kimbelembele na mambo ya siasa za chama tawala au viongozi wa chama tawala, na kuwatelekeza raia ambao kimsingi wao ni waliowapatia umaarufu na si serikali. Panga hili la ku-unfollow mastaa na wasanii pia limemkuta Millard Ayo ambapo mpaka sasa kapoteza wafuasi zaidi ya 300k baada ya Kampeni hii kuanzishwa.

Kampeni hii imelenga mitandao ya Instagram, Facebook, Twitter mpaka YouTube.... unfollow msanii yoyote ambaye ni chawa na si mtu wa kutetea Raia. Wasanii Wamesahau kama followers wao ndio sisi raia ambao wamechagua kutusaliti.

Unfollow wasanii wote ikiwemo wachekeshaji na kila mtu ambaye kapata umaarufu lakini hataki kusimama na raia badala yake amechagua kuwa chawa wa siasa za chama tawala
Mimi na suggest isiwe tuu, ku unfollow bali pia, kureport account zao, na pia unsubscribe youtube zao na kote, kuto ku like posts zao zozote, na kutokununua bidhaa zao kwa wafanyabiashara wasanii na hata wale wasio wasanii bali hawatutetei, pia kuto kuangalia clip zao mitandaoni na kuangalia nyimbo zao youtube, wala kusikiliza nyimbo zao kwenye platforms zozote zile
 
Nilitabiri ili toka mwaka jana. Naona muda umewadia
 
Ndio akili zenu zilipo ishia
Tatizo siyo nyie ni umri Unasumbua.

Wote CCM na NRNE lengo lao kuu ni kushika madaraka. Kila mmoja akipiga hesabu anamuona mwenzie atapata wapi. Akina TAL wanaamini kama mamlaka ya Samia yakiondoshwa na uchaguzi ukawa wa huru na haki, watatoboa. Je, wakiingia ikulu nani atafaidi kwa keki ya Taifa? Jibu ni wao na watoto wao.

CCM wanaamini kuwa bila nguvu za kikatiba alizo nazo Samia sasa Hivi, uchaguzi ukiwa huru na haki, hawatoboi. Ambao ni Ukweli mtupu.

Je, sisi wapigakura watatuachaje. Kwa kuwa TAL hata siku moja hajawahi sema ni nini atatufanyia akiingia ikulu ili sisi tuangalie vikwazo vya yeye kuingia ikulu ambayo ni NRNE, ili tufaidi. CCM wao wapo ikulu muda wote huu ila hakuna mabadiliko. Tupo njia panda. Suluhisho ni kupigania mgombea binafsi si chama
 
Mnawaonea tu hao wasanii.

Unajua matokeo yatakayo tokea ikiwa leo hii Diamond atasimama against serikali? Kama wamefanya yale kwa Gwajima watafanya nini kwa Diamond, Kusaga na Majizo and the like?

Na je, Wananchi watasimama na Hao wasanii pindi serikali itakapo wageuka?

Watanzania wengi wanataka kupiganiwa haki zao, wao wakiwa safe behind keyboards wakati huo wewe unateseka kupambana na mamlaka.

Gwajima kaongea, kawasemea, kapaza sauti, Amezongwa na serikali, Watanzania wapo kimya nyuma ya keyboard wanalalama badalala ya Kukinukisha mpaka serikali iombe pooo. Ndo unataka wasanii wasimame na ninyi au matajiri kama akina Mooo? SIO KITU RAHISI
Ata kenya ilianza hivhiv watu kuimizana mitandaoni. Wakafata Live huko twiter na Tiktok kilichofata n barabarani
 
Back
Top Bottom