Operesheni Unfollow Wasanii wote Mitandaoni ambao hawasimami na Wananchi kwenye Haki

Sasa hii inasaidia nini kuiondoa CCM madarakani? Watanganyika sijui mtashituka lini.
 
Aisee niliichukulia poa ila ipo serious sema wabongo wanasahau sana kesho tu watamrudia Mwijaku
Wakisikia tu habari ya umbea kumuhusu Mwijaku wataibuka huko
 
Wasanii wa bongo wote njaa wanafeki life ukitaka kujua ngoja wakiugua wanategemea huruma ya chama thus ni lazima wajiuze so huwezi linganisha na wasanii wa nchi hizo wao hawaishi kwa kujiuza.
Wa kike zaidi ya udangaji Wana kipato gani,hao wa kiume bila upididi kipi wanachoingiza kutwa lazima wawe machawa tu
 
Soko ndilo uamua wakihamasisha hayo mambo watamuuzia nani.
Soko litaka mambo ya uchawi, ngono,mpira,udaku.
 
Mnawaonea tu hao wasanii.

Unajua matokeo yatakayo tokea ikiwa leo hii Diamond atasimama against serikali? Kama wamefanya yale kwa Gwajima watafanya nini kwa Diamond, Kusaga na Majizo and the like?

Na je, Wananchi watasimama na Hao wasanii pindi serikali itakapo wageuka?

Watanzania wengi wanataka kupiganiwa haki zao, wao wakiwa safe behind keyboards wakati huo wewe unateseka kupambana na mamlaka.

Gwajima kaongea, kawasemea, kapaza sauti, Amezongwa na serikali, Watanzania wapo kimya nyuma ya keyboard wanalalama badalala ya Kukinukisha mpaka serikali iombe pooo. Ndo unataka wasanii wasimame na ninyi au matajiri kama akina Mooo? SIO KITU RAHISI
 
Ndio akili zenu zilipo ishia
 
Naunga mkono hili azimio la kizalendo, Tusihishie kwenye kujiondoa kwenye kurasa zao

-Twende mbele zaidi, kwa kipindi cha miaka mitano (5) ijayo.

-Tuache kuwa wateja wao, wa kununua kazi zao, kuudhuria matamasha yao, Kuacha kuangalia kazi zao.
-Tuache kununua bidhaa/huduma kutoka kwenye biashara zao.
-Kuacha kununua huduma/bidhaa ambazo wao ni mabalozi, na washirika wao wa kibiashara.

Mimi nimejiondoa kwenye kurasa zote za wasanii ,wanasiasa ,waandishi na wafanyabiashara wenye kuunga mkono udhalimu. Hata wewe unaweza
 
Wabongo hii hatuwezi.. tunaogopa virungu vya maafande, but ndo njia nzuri ambayo ikitumika inaleta output mapema.

So wacha tupambane mitandaoni tu
never say never we might get to that stage
ipo siku tutatembea barabarani nakuhakikishia hio siku itafika watanzania wasijipuuze wakati utafika
 
Hamna haja ya ku unfollow.....bali tumia hapo hapo katika platforms zao kuweka ujumbe wa no reforms no election.
 
Mimi na suggest isiwe tuu, ku unfollow bali pia, kureport account zao, na pia unsubscribe youtube zao na kote, kuto ku like posts zao zozote, na kutokununua bidhaa zao kwa wafanyabiashara wasanii na hata wale wasio wasanii bali hawatutetei, pia kuto kuangalia clip zao mitandaoni na kuangalia nyimbo zao youtube, wala kusikiliza nyimbo zao kwenye platforms zozote zile
 
Nilitabiri ili toka mwaka jana. Naona muda umewadia
 
Ndio akili zenu zilipo ishia
Tatizo siyo nyie ni umri Unasumbua.

Wote CCM na NRNE lengo lao kuu ni kushika madaraka. Kila mmoja akipiga hesabu anamuona mwenzie atapata wapi. Akina TAL wanaamini kama mamlaka ya Samia yakiondoshwa na uchaguzi ukawa wa huru na haki, watatoboa. Je, wakiingia ikulu nani atafaidi kwa keki ya Taifa? Jibu ni wao na watoto wao.

CCM wanaamini kuwa bila nguvu za kikatiba alizo nazo Samia sasa Hivi, uchaguzi ukiwa huru na haki, hawatoboi. Ambao ni Ukweli mtupu.

Je, sisi wapigakura watatuachaje. Kwa kuwa TAL hata siku moja hajawahi sema ni nini atatufanyia akiingia ikulu ili sisi tuangalie vikwazo vya yeye kuingia ikulu ambayo ni NRNE, ili tufaidi. CCM wao wapo ikulu muda wote huu ila hakuna mabadiliko. Tupo njia panda. Suluhisho ni kupigania mgombea binafsi si chama
 
Ata kenya ilianza hivhiv watu kuimizana mitandaoni. Wakafata Live huko twiter na Tiktok kilichofata n barabarani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…