Orodha ya walioachwa Ukuu wa Wilaya

Orodha ya walioachwa Ukuu wa Wilaya

Ila hii nchi bana utaratibu wa kupata viongozi ni wa hovyo sana, kipindi flani nikiwa Mzumbe University- Morogoro tukaletewa mgeni rasmi mmoja hivi mdada ilikua ni siku ya 'ujasiriamali' pale chuoni. Mgeni rasmi alikua ni mkuu wa wilaya ya Mvomero ee bana yule mkuu wa wilaya sijui aliokotwa wapi akapachikwa kwenye hicho cheo. Uchangiaji wa kale kadem ilikua ni aibu kumsikiliza yani tangu siku hiyo sina imani na mwana ccm yeyote hata huyo mnamuita mama.
Halima okash huyo
 
Vyeo vimekuwa kama zawadi. Hatuna chujio la viongozi makini. Kuteua na kutengua kila wakati ni dalili ya wazi. Nimewahi kuwa kwenye vikao vya ndani na wakuu wa wilaya na wakurugenzi tofauti katika nyakati tofauti yaani mnatoka kikaoni hadi mnaulizana hivi ni mteuliwa wa rais au mwananchi wa kawaida.
Zifuatazo ni baadhi ya tabia zao;
1) kujikweza
2) hawazingatii muda kabisa vikaoni na hawataki mawazo mapya.
3) kuzungumza mambo ya chama na kusifia mabosi badala ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
4) wengi ni wasomi wa degree, masters, PhD lakini hawana content vichwani yaani mtu anaongea hadi unashangaa katokea wapi
6) wanapenda vitisho na kulazimisha utekelezaji wa mambo yaliyo kisiasa zaidi.
7) Wengi hawana ushirikiano na watu wa chini.
8) migogoro kati ya mkurugenzi, das, na mkuu wa wilaya yaani kila mtu anataka ukuu kwa wenzie.
9) alafu wengi wanaopangiwa post hizo huwa hawaendi na familia zao yaani huko wilayani maadili yao hadi unajiuliza mara mbili.
NB: badala ya serikali kutegemea viongozi walioandaliwa na chama cha siasa ijaribu kutafuta namna nyingine ya kuandaa viongozi watakaokuwa na sifa watakaohudumia watu wote bila uchama. Pia itazame watumishi wa serikali waliofanya vizuri kwenye maeneo ya kazi ndio wawe madisii, wakurugenzi, na vyeo vinginevyo hii italeta hata motisha kwenye utumishi wa umma kuwa kumbe kuna promotion na utambuzi wa mkuu wa nchi la sivyo chama kitaendeleea kukaa madarakani kikiwa na serikali dhaifu.
 
Tumewahi kutumia muda wetu mwingi sana kumkanya huyu jamaa , kwamba Cheo ni dhamana tu , Asikitumie kukomoa wengine , lakini akaweka pamba masikioni

Sasa matokeo yake ndio kama mlivyosikia , Karma haiachi mtu .

Kila Ubaya Utalipwa .
Wale waliounga juhudi kutoka Chadema wote mliowaombea kutoswa wamepeta bila kupingwa!
 
Back
Top Bottom