Orodha ya Watanzania maarufu waliokufa bila kujenga nyumba

Sawa sawa mzee! Asante kwa ufafanuzi Mohamed Said
Licking...
''Akija mzee Mohamed Said hapa mtatibuana!! Ile nyumba nadhani ilikuwa ya mzee muislam mmoja hivi.''

Bahati mbaya sana.

Hapakuwa na haja ya kunikejeli mimi na wazee wangu chembelecho, ''Muislam mmoja.''

Wazee wangu waliishi na Nyerere kama ndugu.

Mwalimu Nyerere kadi yake ya TANU ni No. 1.
Kadi ya TANU ya Ally Sykes ni No. 2 na ndiye aliyemwandikia Nyerere kadi yake.

Kadi ya TANU ya Abdul Sykes ni No. 3.
Kadi ya TANU ya John Rupia ni No. 7.

(Ingawa Abbas Sykes anasema kadi No. 7 ni yake).
 
Wala sikuwa namaanisha kejeli kwasababu mara nyingi huwa nasoma mabandiko yako humu kuhusu historia ya Nyerere na wazee wa kiislam waliomsaidia! Sikuwahi kuwaza kama Nyerere aliweza kujenga nyumba ile kwa miaka ile tena Magomeni!
Tuko pamoja mzee
Mohamed Said
 
Licking...
Baada ya kuacha kazi ya ualimu Nyerere alikwenda kukaa nyumbani kwa Abdul Sykes.


Nyumba ya Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey na Sikukuu ambayo Nyerere aliishi 1955.
Nyumba hii wakati ule haikuwa hivi hii ni picha ya 1980s baada ya kufanyiiwa ukarabati kugeuzwa duka.
Katika miaka ya mwanzoni 2000 nyumba hii ikavunjwa ikajengwa nyumba hiyo hapo chini:



Mwalimu Nyerere alipohama kwa Abdul Sykes akahamia Maduka Sita nyumba aliyotafutiwa na TANU:


Nyerere akiingia nyumbanin kwake Maduka Sita Magomeni 1955
Daily News 15 November, 2021 ilichapa picha ya nyumba ya Nyerere ya Magomeni aliyojenga 1958 na kusema kuwa mikutano yote ya siri ilikuwa ikifanyika hapo.

Si kweli.
Mikutano yote ya siri kuhusu harakati za kuunda TANU ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes hata kabla Nyerere hajafika Dar es Salaam.




 
7.....Le Mutuz
 
Jenga nyumba wewe acha porojo,yaani uwe na miradi yote hiyo alafu ushundwe nyumba ya 30 kijijini kwenu,basi utakuwa hujitambui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…