Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Sasa mambo yanakwiva!

Sidhani kama viongozi wa dini watakaa kimya kwa hili jambo.

yalianza hivi hivi hatimaye ....

Hakuna aliyesalama.
shetani hajawahi kuwa na urafiki ndivyo ilivyo CCM.
Mbwa wa Samia wapo kazini.
 
Hii ni hatari kubwa sana, ni Habari mbaya sana hii.
Endapo kama Habari hii ni ya kweli, basi Serikali inapaswa kufanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha kwamba inauthibitishia Umma kwa vitendo kwamba yenyewe Kamwe haihusiki kwa namna yoyote ile na shambulizi hilo.
Serikali inapaswa ifanye hivyo kwa UAMINIFU MKUBWA ili kuondokana na mashaka yoyote yale kutoka kwa Umma.

Ikumbukwe kwamba: Watu bado hawasahau kabisa kuhusiana na suala la Marehemu Mzee Kibaona suala la jaribio la Mauaji dhidi ya Tundu Lisu ambaye yupo mahabusu gerezani sasa hivi.

Hata kama tukio hilo limetekelezwa na Maadui zake binafsi huyo Padre Kitima, bado Serikali ndiyo itakayoshewa kidole zaidi. Hii ni kutokana na Ukweli mchungu Sana kwamba Mazingira halisi yaliyopo hivi Sasa hapa Tanzania Kati ya na Padre huyo na Watawala yanaonekana kuwa 'yamekorogeka vibaya sana.'
Very bad timing for the execution of such a satanic action!
Hiyo ni kauli ya mwanaccm.
Screenshot_2025_0501_065414.jpg
 
Duu. Ila huyu Maria Sarungi wa chadema kumbe ana close link na huyu Pad Kitima kulielekeza pasivyo Kanisa la Roman Catholic la Tanzania ku support kufanikisha uhaini wa Tundu Lissu? Kama ni kweli basi ni jambo jema kwani hatutaki yatutokee yaliyotokea Rwanda ambako Kanisa hili lilitumika kwa kiasi kikubwa kuchochea moto uliotokea.
Kwahio Maria Sarungi hata kama ni mkatoliki asiwe karibu na kanisa? What are you trying to prove here?!
 
Iwe kweli iwe uongo .
Samia asipoondoka Madarakani hii nchi itaangamia .

Analeta siasa za Udini.

Anafadhili watu wa kujibu hoja za kitaifa wa misingi ya dini.

Watu wanasema wizi wa kura hauleti maana ya uchaguzi na ni dhambi kwa Mungu na kujenga taifa la watu wenye hila na kukosa uzalendo halafu wanaibuka waislam wanaleta hoja za kijinga kabisa eti mashehe mbona walifungwa . Yaani wameifanya dini y kiislam ionekane ina watu wasiojali hata uumbaji wa Mungu zaidi ya mambo ya siasa za CCM.

Watu walioumbwa na Mungu wanauawa na kupigwa na kusingiziwa kesi za uongo halafu ,Samia anahonga waislam waseme kuwa ni sawa na dini yao inaruhusu .

Rasilimali zilizoumbiwa Wataganyika Ili wazitumie na walikaa nazo kabla hazijaja siasa na dini za wageni leo zinauzwa kiholela ,pesa zinazopatikana badala ya kujenga barabara za kisasa na kuzuia uhalifu na ajali badala yake Samia anahonga Mashehe wenye uroho ili waseme ni sawa na dini inaruhusu kwa sababu tu rais ni muislam afanye anachotaka kiwe kizuri sawa au kibaya sawa ataamua yeye mwenyewe kama vile Mungu ,

Leo hii tumeanza kuona zile siasa za kina shehe Faridi za chuki za kule Zanzibar zimeanza kuja Tanganyika kwa kasi . Shehe Mwaipopo anajenga itikadi za Chuki dhidi ya ukristo . Wakristo hawajawahi kuleta siasa za chuki zaidi ya kuionya serikali itende haki.
Hata kama Wananchi wataandamana kwenda Kisutu inawahusu nini Mashehe ?Kwani watu wanaandamana kidini au kisiasa ? Ni lini watu wameandamana kwenda kwenye makao makuu ya Bakwata ? Ni lini watu wameandamana wakiwa na mabango ya kupinga uislamu ?
Je, Samia amewekwa na waislam au na Katiba ya Nchi .?
Itikadi za kidini zimekua zikileta madhara makubwa kwa Wakristo kuumizwa na makanisa kuchomwa moto .
Kule Zanzibar 99% ya watu wote ni waislam na serikali yote ni ya waislam , hiyo 1% bado inapigwa vita na kumwagiwa tindikali na kuchoma makanisa moto wakati haina madhara yoyote kwa Waislam, roho mbaya tu ya hawa na dini yao ya isiyojali haki na utu .

Waislam wamesahau kuwa hakuna kiumbe kilichoswali kwa kusujudu kama Shetani mpaka akawa ndiye baba wa sigdah usoni .
Lakini Mwenyezi Mungu hakufurahishwa na swala zake kwa sababu ndani yake palikua na hila na uovu .

Kama waislam wao adui yao ni ukristo bila kujali kuwa mtu amewakosea nini basi wajue Wakristo ni watoto wa Mungu wanaochukizwa na uovu unaotendwa na yeyote bila kujali ni dini gani au ana cheo gani na hawachomo moto msikiti wala kumwagia shehe tindikali bali watakemea kama wanavyomkemea baba wa sigdah Shetwani .

Samia hafai kuwa Rais wa Tanganyika yenye watu wa dini tofauti na wa makabila tofauti .
Amekua na kulelewa katika imani na jamii yenye ubaguzi mkubwa kwa wakristo na watu weusi wenye vichogo.

Huyu mtu walimpaje umakamu wa Rais Mwanamke kutoka kwenye jamii ambayo mwanamke haruhusiwi kuongoza wala kushikana mikono na Mwanaume ?
Mtu ambaye tangu utoto amekulia kwenye imani ambayo haithamini kabisa ukristo na hata uislam wa watu wa Tanganyika anauona kama haujatimia . Leo anapewaje aongoze jamii hiyo ?

Hivi kweli kwa akili yake anaona ni Sawa kabisa kukaa kimya na kuacha hoja za Wasomi wa kiwango cha juu kabisa duniani wa Kanisa Katoliki zijibiwe na Wapumbavu na wajinga na malofa kama Shehe Mwaipopo , Mstaafu wa polisi kutoka Kivu Mu7i7o , Steve Nyerere na vijana wa hovyo kwenye mitandao kutukana na kuwatisha Mababa Askofu wenye Elimu na waliofanya tafiti dunia nzima kwenye masuala ya kijamii kisiasa na kiuchumi . ?

Rais hatoi tamko badala yake naye anatoa tamko linalofanana na hao wapumbavu kama Shehe Mwaipopo. Yaani Rais anasikiliza hoja za Maaskofu anazijibu kwa kutumia hoja za stevu Nyerere ,Shehe Mwaipopo na Chalamila (aliyetaka wanyonge wazalishe wake zao wenyewe kama hawana pesa ).

Yaani badala ya Rais kutafuta suluhu anaongeza mpasuko kwa kusifia walioua na kupiga watu na kutukana maaskofu na kutoa rushwa kwa Makundi ya kidini yanayowatukana na kuwatishia maaskofu.?


Kikwete aelewe tu kuwa mgombea wako hafai atatuharibia nchi; ukisema kuleta mgombea mwingine ni labda atokee mchawi .😂😂😂😂
Sasa ni wazi Mchawi ameshatokea na amelogeka haoni hata anapokwenda .Hajui hata kula na Kipofu.
Makongamano na vikao vyote alivyoruhusu vifanyike hazingatii kabisa maoni yake eti yeye ni chura kiziwi . Amazika maskio kwa akili ipi na elimu ipi inayomfanya asisikilize maoni ya Wasomi na watu kama Jaji Warioba na Jenerali Ulimwengu na Tundu Lisu ?

Taani hasikilizi ushauri na maoni ya Mababa wa makanisa na manabii na mitume wa Mungu badala yake anasikiliza ushauri wa mapolisi kama Mulilo wanaotaka kutumia risasi na marungu tu hata kuua mbu kwenye paji la uso wa mtoto mchanga .

Duniani kote polisi wanapotuhumiwa kufanya kazi kinyume cha utaratibu wa kisheria inaundwa tume ya kuchunguza ili kujenga Imani ya vyombo vya dola kwa wananchi .
Nyerere alifanya hivyo na Mwinyi akajiuzulu, Kikwete alifanya hivyo na pia bunge lilifanya hivyo kwenye Oparation Tokomeza.
Rais Samia yeye anasema kifo ni kifo tu , anaona waache wafe wametaka wenyewe . Wanaichezea dola . Tena anatokea Waziri wa Mambo ya ndani na kupongeza kupigwa kwa viongozi waliokwenda kusikiliza kesi . Eti walisema wanakwenda kukinukisha mahakamani ?

Yule Bashungwa sijui ni kabila gani la Tanganyika au ni wale wageni waliopewa madaraka ya juu. Yaani Heche alisema wafunge vitambaa vyeupe na waende kwa amani leo hii Bashungwa analewa damu za watu anasifia mauaji eti walitaka kufanya fujo . Je,Mtu akitaka kufanya fujo anauawa ?
Kazi ya FFU ni kutuliza ghasia sio kuua wafanya ghasia . Je pale palikua na ghasia gani wakati viongozi wa Chasema walikua kwenye magari na sio maandamano ?

Rais kiziwi hawezi kamwe kuongoza nchi ?
Rais Mwenye hekima wakati mwingine ni kama muamuzi au hakimu au jaji anaamua kwa hekima isiyoumiza wengine .
Mfalme Sulemani ni mfano wa Mtawala mwenye Hekima maana alihukumu kwa Haki bila kutumia nguvu ya kuua wengine na alitawala dunia na mali zote .
Umetema madini san. Kuna watu wanaichukulia poa sana amani. Washukuru haatuna matukuo ya visasi. Vinginevyo kuna watu watatumia hizo tehama kufanya kazi kutokea majumbani kwao.

Amani ni tunda/zao la haki.
 
Kwa jinsi Padri alivyotema madini yaliyonyooka kama rula dhidi ya hawa watawala magaidi, kulikuwa na kila dalili lolote huenda kumkuta.

CCM na serikali yake ni laana.
Serikali zote duniani zinatisha ukizikosoa unapaswa ujiandae na kujipanga kwa lolote hasa serikali za Afrika.Shekh Ponda Mbona alikoswa na Risasi kabisa , Ila sina maana na hili pia likawa swala la kisiasa .Ila ni kwamba ukiwa mkosoaji au kufuatilia fuatilia mambo ya kisiasa watu kukufanya kama soka ni swala la kawaida.
 
Huwa nawasmbia watu, jpm ndio muasisi wa haya mambo, alikuja kuchora blueprint, na ndio wanaifuata.
Hili si la chadema anymore

Unalinganisha vitu viwili tofauti.

Magufuli alikua mzalendo
Magufuli alichukia sana MAFISADI .
Magufuli hakua mnafiki .
Magufuli watu waliandamana mpaka Centrol polisi na kuimba mapambio hakuvunja watu miguu wala kuua waandamanaji .
Gwajima , Bagonza, Mwingira na askofu Shoo na kanisa Katoliki walimkosoa sana Magufuli . Wengi baadae walimwelewa nia yake ya kulinda rasilimali za nchi . Na alijua kila kitu kuhusu wanasiasa feki wa upinzani ndio maana alisema anataka upinzani wa kweli sio ule uliokua unatumiwa na genge la mafisadi akiwemo Mbowe na rafiki yake JK.

Kosa la Magufuli ni hotuba zake za kizalendo zilizokua zinawafanya watu wawachukie Mafisadi na ile hotuba ya msaliti iliyowafanya wabaya wa Kisu kumpiga risasi .

Lakini Magufuli hakua mnafiki .

Huyu ni mnafiki. Aliahidi mwenyewe Reform ,uvumilivu na maridhiano . Unajua madhara ya mkuu wa dola asiye na msimamo na kile anachokisema na kujitahidi ?
Hivi Samia angesimamia msimamo wake wa reform na maridhiano leo nchi ingekuwa hapa tulipo ?
Kwanza angeshinda kwa kishindo maana mpaka wapinzani walikua wanampenda hasa wanawake leo mpaka ndani ya CCM haaminiki ndio maana wanatumia nguvu tena ili angalau asije akapoteza kiti kwa presha na kuchanganyikiwa maana akiachwa achuane na wanasiasa mahiri atachanganyikiwa kabisa .
 
Mi kufikiri kwangu ni tofauti,hata CDM wanaweza fanya hilo tukio ili tu ionekane ni Serikali.
1.Lengo kuichafua serikali.
2.Kutafuta huruma kwa wananchi kwa Kudai serikali inashambulia hadi viongozi wa dini.
3.Kuikosanisha serikali na madhehebu ya kikatoliki hasa katoloki yenyewe.
Tusianze kuinyooshea serikali kidole.
 

Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.

Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.

Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.

Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.

Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.

=====
TAARIFA ZA AWALI:

"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri

Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "

Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.

Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?

CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?

View attachment 3321209

View attachment 3321207
Tunalilitafuta mwishowe tutalipata tu.
 
Back
Top Bottom