Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Nina uhakika hata wewe hu3lewi unachokisimamia kwenybhoja yako😭
Mkuu, huwa sibahatishi. Subiri utauona ukweli ukijifunua wenyewe mbele za macho yako. Usifumbe macho na akili, basi!
 
Tetesi za kushambuliwa kwa Padri Kitima na kuhusishwa kwa serikali hazipaswi kuchukuliwa kama ukweli bila ushahidi. Serikali haina sababu ya kumlenga kiongozi wa dini ambaye hana uhasama wowote wa moja kwa moja nayo. Katika mazingira ya sasa, si ajabu kuona tukio la uhalifu likigeuzwa ajenda ya kisiasa. Tuwe makini na propaganda, tusubiri ukweli ujulikane.
Ndio sababu serikali ilishauriwa mara nyingi kuchukua hatua kwa wanaoitwa wasiojulikana,wakaziba masikio.
Kama tukio hili ni la kweli basi kuna shida kubwa.
Matukio haya ya wasiojulikana ni kweli yalianzia kipindi cha Magu. Lakini kwa vile Magu aliwaheshimu sana watumishi haswa mapadri/maaskofu kanisa katoliki,hatukuwahi kusikia hao wasiojulikana wamewagusa.
Hata kipindi kile Baba Askofu Niwemugizi anatishiwa kunyang'anywa uraia,ni yeye aliyeingilia kati kwa kumpigia simu kuwa asiwe na wasi wasi.
Ni wazi wapo watu wanaojihusisha na ukatili kwa kujidai wanawalinda watawala wasikosolewe, na wao watawala kwa sababu wanazozijua wenyewe wameendelea kuwalea.
Zipo kauli za hatari zimewahi kutolewa na baadhi wa ya wanaccm, mfano ikitokea wakampoteza mtu anayekosoa viongozi wao polisi lisiwatafute,na bahati mbaya aliyeinuka peke yake kukemea alikuwa ni Dr. Nchimbi basi.
Polisi wenyewe walinyamaza kimya na hakuna kauli iliyotoka kwao kitu ambacho siyo sahihi.
Sasa kushambuliwa kwa Padri Kitima ambaye amekuwa muwazi kutoka akiwa makamu mkuu wa St Augustine mpaka leo.
Huyu hajaanza sasa labda awamu hii tu,huyu amekosoa awamu zote na anafahamika hivyo,alimkosoa mpaka JPM wakati wa janga la covid19. Wasi wasi ninauona kwa tukio hili ni kwamba linaweza kutafsiriwa tofauti yaani kwa kuwa Rais ni muislam na huyu aliyeshambuliwa ni mkristo tena Padri kanisa katoliki na Katibu wa baraza la Maaskofu, lazima litaleta hisia za udini kabisa.
Kitu ambacho si kizuri. Matukio ya kushambuliwa mapadri yamefanyika sana huko Zanzibar nyakati za nyuma na baadhi ya waislam wenye itikadi kali, na serikali kwa kujua uzito wa mambo ya kidini,nafikiri ni kipindi cha Kikwete aliwaalika wachunguzi kutoka nje ya Tanzania nakumbuka walikuwa FBI,ili angalau kuondoa hisia za udini kwa upande wa wananchi kwa watawala wakati ambao walikuwa waislam kama ilivyo sasa,na kweli ilisaidia kuiondolea lawama kwa vile serikali ilionyesha dhamira ya kweli na haina upande wa dini inaougemea pamoja na kuwa wao watawala wanatoka dini ya kiislam.
Ni majuzi tu, wakati wa juma la Pasaka tumewasikia maaskofu wakikosoa mapungufu kwenye mifumo ya uchaguzi,kukosekana Kwa haki lakini ikatokea walioibuka kuwajibu maaskofu ni baadhi ya viongozi wa dini ya kiislam na siyo serikali ambayo kimsingi ujumbe ulilengwa kwake.
Wakatoliki wana Sifa kubwa ya kuheshimu sana viongozi wao,na hii nafikiri ni kutokana na kanisa kuwa na mafundisho na sheria zake ambazo hufundishwa toka wakiwa watoto na ndio sababu huwezi kumsikia kiongozi yoyote wa serikali bila kujali ana cheo gani akipinga au kukosoa hadharani, waraka/ mahubiri/hoja za viongozi wao.
Sana sana utawasikia wakiibuka kina Makonda na wengine wasio wakatoliki basi.
Ni tofauti sana na madhehebu mengine ya kikristo, na hata dini zingine ambako siyo ajabu kumsikia muumini akimshushua kiongozi wake hadharani.
Na kitu kingine wakatoliki ni wengi sana kwa idadi kulinganisha na madhehebu au hata baadhi ya dini zingine kwa pamoja.
Kama ni la kweli kuwa Padri Kitima kashambuliwa basi, serikali ina kazi ya kufanya kwenye hili,wasipuuze kabisa,hili lina athari kubwa likipuuzwa.
 
Muhusika si ana julikana 😅hawa jamaa wana akili ndogo kabisa wanafanya mambo kitoto acha Rwanda aendelee kutu dharau
 
Hao washenzi waliomshambulia padri wanazidi kumfanya yule wa enzini aonekane ni dikteta katili kama yule aliyetwaliwa. Sijui kwa nini anaruhusu hili litokee wakati anajua litamchafua vibaya na kuonekana wazi ni dikteta mpevu. Uvumilivu wake umefika ukomo anaona kama noma na iwe noma, anaanza kushambulia wenye hoja kinzani juu ya mambo muhimu ya siasa za nchi
 
Kama ccm wamehusika na huu upuuzi, kanisa katoliki linatakiwa kuchukua hatua na kutoshiriki chochote na CCM.
Ccm ndio wahusika wakishirikiana na policcm. Hakuna mwengine aliyefanya hayo.
 
Imeandikwa;..... 'Nitampiga mchungaji na kondoo watatawanyika'.

Kwenye lile sanduku la kura sidhani kama kondoo watatia mguu.
 
Kikubwa ni watu kuweka tuhumu na dhana bila ushahidi, wakati kiusalama hata adui anaweza kusoma mchezo na kufanya tukio ambalo ana uhakika wewe utakuwa mtuhumiwa namba Moja ili afaidike.

Sasa naona watu moja kwa moja wanaanza kutupa lawama za Bure.
Mpwa uko sahihi sanaaaa tena sana tatizo unajua liko wapi mpwa? Kuna watu walitoa nafasi ya haya kufanyika
 
Yule alipewa majina mabaya yote kwakua aliziba njia za ulaji na siukatili km wanaoufanya wakutosikiiza wanyonge
 
Duu. Ila huyu Maria Sarungi wa chadema kumbe ana close link na huyu Pad Kitima kulielekeza pasivyo Kanisa la Roman Catholic la Tanzania ku support kufanikisha uhaini wa Tundu Lissu? Kama ni kweli basi ni jambo jema kwani hatutaki yatutokee yaliyotokea Rwanda ambako Kanisa hili lilitumika kwa kiasi kikubwa kuchochea moto uliotokea.
Kila propaganda semani ila ukweli utabaki ukweli. Ccm ndio wavunaji amani wa mwanzo. Leo hii kila mtu awe mpiga debe wa ccm kisa kulazimisha kupendwa.
 
Tetesi za kushambuliwa kwa Padri Kitima na kuhusishwa kwa serikali hazipaswi kuchukuliwa kama ukweli bila ushahidi. Serikali haina sababu ya kumlenga kiongozi wa dini ambaye hana uhasama wowote wa moja kwa moja nayo. Katika mazingira ya sasa, si ajabu kuona tukio la uhalifu likigeuzwa ajenda ya kisiasa. Tuwe makini na propaganda, tusubiri ukweli ujulikane.
Ccm ndio wahusika wa hayo kwasababu kila mwanaccm anayepanda jukwaani hutolea maneno viongozi wa dini kisa kudai haki. Hili nakubali kwa 10000% kaam ccm na serikali ndio wahusika.
 
Watu waliishasema sana humu, haya mambo yakizoeleka, itakuwa kama dhambi ya utengano, itaendelea tu Na nobody will be safe, yaani hata hao wanaofanya hivyo hawako safe pia, mfumo ukiwatema au wakajichanganya ni yaleyale tu.Magufuli aliishawahi sema kuna wastaafu wanawashwawashwa imagine. SEMA HILI TAIFA HALINA VIONGOZI WAZALENDO KABISA..
 
Back
Top Bottom