Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Huyu mama kafika mbali sanasasa..anataka kutubagua kidini..
Na wanasiasa wataenda kanisani kupata baraka na huduma za kiroho?
Hapana huyu mama adhibitiwe mshenz sana
Kabisa tukianza kubaguana kidini tayari hapo kuaanza kunukia vita ya kidini sababu ya upumbavu wa huyu Mama anaeamimi kukaa kimya ndio namna ya kusolve matatizo ya jamii..... Hana busara kabisa na amejawa na tamaa ya uongozi
 
Nmeona sehemu umeandika utoto na kutishia mtu. Kubishana kwa hoja ndo mpango mzima humu JF siyo kutishana kwa vioja.
Nipo jukwaa la siasa sasa miaka 15, mtu kama tuna interact mara ya kwanza naweza vumilia matusi yake.

Katika muda huo kuna watu humu tumeshakubaliana bila mkataba rasmi kuvumiliamiana humu kwa mihemko ya hoja.

Otherwise mchangiaji mpya anayeanza kwa kunitukana uvumilivu ni mara mbili tu anaenda kwenye ignore list.

Kukusolewa sawa nipo tayari, ila matusi tu no.
 
Ubaya wa JPM umeendelezwa na Samia, sio kwamba ubaya wa Samia ndio unafuta maovu ya JPM. Hata kama alikua hafanyi yeye, kukaa kimya huku maovu yantendeka means alikua anasupport.
Sasa kuendeleza kwa Samia mbona kelele zipo mojakwamoja kwa JPM?
 
Mama ameamua kufuata mkondo ule ule wa Jiwe. Amekuwa, amekomaa na kurithi tabia zile zile mbaya na mbovu.
Usisahau tu, wakati jiwe akiwapoteza wakosoaji wake, mama alikuwa msaidizi wake mkuu.

Huyu amekuwa mbaya kuliko hata marehemu. Marehemu hakuwahi kujeruhi kiongozi wa dini, wala hakuwahi kumwua mgombea yeyote kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa. Huyu kayafanya yote, na idadi ya waliopotezwa ni kubwa kuliko wakati wowote.
 
Sasa kuendeleza kwa Samia mbona kelele zipo mojakwamoja kwa JPM?
Maana ndio muasisi, alionyesha kuwa inawezekana. Kama asingefanya hata Samia angekosa confidence ya kuendeleza maana asingekua na precedence.
 

Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.

Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.

Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.

Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.

Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.

=====
UPDATES:

Polisi wadai kumshikilia mmoja: Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

=====
TAARIFA ZA AWALI:

"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri

Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "

Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.

Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?

CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?

View attachment 3321209

View attachment 3321207
 
Duu. Ila huyu Maria Sarungi wa chadema kumbe ana close link na huyu Pad Kitima kulielekeza pasivyo Kanisa la Roman Catholic la Tanzania ku support kufanikisha uhaini wa Tundu Lissu? Kama ni kweli basi ni jambo jema kwani hatutaki yatutokee yaliyotokea Rwanda ambako Kanisa hili lilitumika kwa kiasi kikubwa kuchochea moto uliotokea.


Shetani jingine hili hapa. Hili lazima litakuwa ni miongoni mwa hayo yanayoua na kuteka watu.

Mungu wetu tunaomba laana dhidi ya watumishi waaminifu wa shetani kama huyu kama huyu asiye na akili ajiitaye Dr. Akili
 
Huwa nawasmbia watu, jpm ndio muasisi wa haya mambo, alikuja kuchora blueprint, na ndio wanaifuata.
Hili si la chadema anymore
No no no Alipopiga Mzee Warioba mbele ya camera Magufuli alikuwa Rais?

Huu ni mfumo
 
sheitwaani mkubwa.
usiyejua historia ya ukombozi wa afrika.
Unamjua Askofu Desmond Tutu wewe.
Tafuta historia yake na hakuwahi kuambiwa aache kuchanganya dini na siasa mwehu wewe
Usichanganye Ukombozi wa Afrika na mambo ya kis.. nge.
 
Ndugu yangu MAXENCE MELLO mmiliki wa JAMIIFORUM unatukosea sana JF Members. Haiwezekani tetesi zenye nia mbaya kama hizi ukaendelee kuziacha tu zikienea kwa kasi kwa mwamvuli wa JF.

@moderators ondoeni hii thread hapa jamvini
Wewe tulia nyie ndo msiojulikana!
 
Acha uongo mbona mimi mkatoliki na sijauwawa? Huyo Padre tunamjua ni mwana Chadema ila anajificha tu kwenye upadre hata baadhi ya Maaskofu walishaanza kumshitukia.
kwaiyo wanachadema ndo wauwawe au ?
 
Back
Top Bottom