Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.
Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.
Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.
Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.
Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.
=====
TAARIFA ZA AWALI:
"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri
Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "
Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.
Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?
CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?
View attachment 3321209
View attachment 3321207